Tuesday, October 30, 2012

*AZAM WAMWANGUKIA KOCHA WALIOMTIMUA, NI BAADA YA KUMTIMUA KOCHA MPYA ALIYECHAPWA 3-1 NA SIMBA

Kocha aliefukuzwa Boris Bunjak
Aliyekuwa Kocha wa Azam Stewart Hall
 KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.

Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.

Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu

Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.

Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).

Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.

Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine. 

Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
  

*GODFREY NA UPENDO WAMEREMETA

Bwana harusi Godfrey Mng'anyi akipozi kwa picha na mkewe, Upendo, wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanandoa hao walifunga ndoa yao katika Kanisa la Manzese. Bwana harusi ni mfanyabiasha na Bi Harusi ni mjasiliamali katika Ofisi yake ya Stationary.

Sunday, October 14, 2012

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA MAHUJAJI JIJINI DAR JANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
 Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. 

Tuesday, October 9, 2012

*MWANAFUNZI ALIYEFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE AKIWA WODINI


Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato hicho akiwa wadi namba 7B  katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo jana, baada ya kulazwa kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe ambapo hivi sasa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Saturday, October 6, 2012

*RICK ROSS ALIVYOPAGAWISHA USIKU WA SERENGETI FIESTA LEADERS CLUB

  Msanii wa muziki kutoka nchini marekani, Rick Ross, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha kubwa la Serengeti Fiesta, lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Mbali na msanii huyo pia walikuwapo wasanii kibao wa muziki wa Bongo Flava kutoka Bongo na nje ya Bongo.
 Msanii AT, akishambilia jikwaa na mnenguaji wake wakati wa tamasha hilo.
 Sehemu ya umati wa mashabiki wa Tamasha hilo, waliobahatika kujitokeza kushuhudia mashambulizi.
Sehemu ya mashabiki wakiburudika.

Tuesday, October 2, 2012

*THOMAS MASHALI KUKIPIGA NA BONDIA WA UGANDA SIKU YA NYERERE DAR


Na Mwandishi Wetu


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Bondia Medi Sebyala wa Uganda, litakalofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Mratibu wa Pambano hilo linalosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO, Regina Gwae, amesema mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Mashali anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vema nchini. 

“Huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda Ulaya, ukaikimbia Afrika Mashariki, hivyo tumeona tumpe pambano Afrika Mashariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa,” alisema Regina. 

Aliongeza kuwa, mazungumzo na bondia Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo ili ausaini baada ya kuupitia. 

“Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, huwezi kuacha kuwataja Mashali na Sebyala,” alisema Regina. 

Regina alisema wanataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala naye ni mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia mahiri nchini Fransis Cheka na Rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti. 

Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye kuvutia wakiwemo mabondia chipkizi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Jonas Segu,  mabondia wengine watakacheza utangulizi  watatangazwa baadaye watakaosindikiza mpambano huo.

 Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.