Sunday, July 7, 2013

*DKT SALMIN NA DKT SHEIN WAUNGURUMA KIBANDA MAITI ZANZIBAR LEO


 Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (Komandoo) Dk.Salmin Amour Juma, alipokuwa akiwasalimia na kuwahutubia katika Mkutano wa hadhara

Kibandamaiti Mjini Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar.

Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja,katika Viwanja vya Demokrasia Kibanda maiti mjini Zanzibar,katika mkutano huo ulizungumzia uwepo wa Serikali mbili kwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania.
Wanachama wa CCM wa maskani ya Kisonge wakishangilia katika Mkutano wa hadhara uliofanyika leo na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,Uwanja wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar. Picha na Ramahan Othman,Ikulu.

*RAIS WA ZANZIBAR*RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kikundi cha ZAYDAT &BASMA GROUP cha Chukwani Zanzibar,TatuSuleiman,wakati alipokuwa  akiangalia bidhaa Mbali mbali za vikundi vya Ushirika kutoka Zanzibar vilivyoshiriki katika maonesho ya sabasaba ya kibiashara katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa  Bana Enterprises Company Limited SAID OMAR SAID, kampuni ambayo inajishuhulisha na utengenezaji wa fanicha za Mti wa Mnazi,wakati alipotembelea maonesho ya sabasaba ya kibiashara katika viwanja vya
mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa,wakati alipowasili katika Mabanda ya Taasisi yake (Mfuko wa Fursa sawa kwa Wote),alipotembelea maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katikaviwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  akipata maelezo wakati alipokuwa
akiangalia Bidha mbali mbali za Akima mama kutoka Mkoani Kagera katika maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katikaviwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akitoa ushauri kwa wasimamizi wa  kampuni ya Nguo ya Arusha chini ua usimamizi wa Mkurugenzi wake Anuj Shal,(kulia) wakati wa maonesho ya sabasaba ya kibiashara yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

*RAIS KIKWETE ANOGESHA TAMASHA LA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA DAR


Rais kikwete akifungua tamasha la matumaini hivi sasa uwanja wa Taifa,jijini Dar.Picha zaidi zitawajia hapo baadae kidooogo.
Waimba injili Ambwene Mwasongwe (kulia) na Edson (kushoto) wakiimba sambamba katika Tamasha la Matumaini 2013.
Edson akishambulia.
Ambwene Mwasongwe naye alikuwepo.
Sehemu ya mashabiki wakishangilia burudani

*TAASISI LA STARKEY HEARING FOUNDATION YAWATIBU WALEMAVU WASIOSIKIA


 Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani (American Football) Rays Lewis akimpa  Rais Dkt. Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha. Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo.
 Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing Foundation  Bwana Bill Austin Starkey akimhudumia mtoto Lissa Frank(9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mkoani Arusha leo.
Waasisi wa Taasisi ya Starkey Foundation Bwana Bill Austin Starkey(kulia aliyeinama) na Mkewe Tani Austin(Wapili kushoto) pamoja na mhudumu kutoka hospitali ya Seliani(kushoto) wakifurahi baada ya mtoto Lissa Frank(9) kuweza kusikia vyema baada ya kupatiwa matibabu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mjini Arusha leo. (Picha na Freddy Maro) 

BASI LA SUMRI LAUA TISA LAJERUHI 53 KATAVI.


Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kusabisha watu tisa kupoteza maisha na kujeruhi abiria wapatao 53 katika mto Iku uliopo katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
 Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 wakati basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema  kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu.
  Mganga mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Dr Emanuely Kamgobe alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kudumbukia mtoni ambapo dereva huyo alitoka  na kukimbilia kusikojulikana.
 Alifafanua kuwa juhudi za uokoaji zilianza kufanyika usiku huo huo ambapo majeruhi 53 waliokolewa na maiti tisa za wanaume watatu na wanawake watano na 
mtoto mmoja wa kike ziliopolewa katika maji 
 Alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri isipokuwa majeruhi watatu walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa kwa matibabu zaidi na kufafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kuliongoza gari, ubovu wa gari na wembamba wa daraja 
 Afisa Mwandamizi wa SUMATRA mikoa ya Rukwa na Katavi, David Chiragi alisema basi hilo lilikuwa limeiba njia kwani leseni yake inaliruhusu basi hilo kufanya safari za Sumbawanga Kirando na siyo Sumbawanga Mpanda kwa mujibu wa leseni iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu 
 Alisema hata upana wa daraja ilipotkea ajali hiyo ni mdogo sana ambapo vipimo vinaonesha daraja hilo lina upana wa mita 3.5 (tatu na nusu) tu wakati basi lina upana wa mita nne na nusu hivyo kujenga mazingira ya ugumu wa dereva kulenga daraja inapotokea msukosuko wa aina yoyote hasa wakati wa usiku na hivyo kuwataka wakala wa barabara mkoani Katavi kuangalia namna ya kupanua daraja hilo na kuboresha eneo hilo 
 Alisema katika kipindi cha Januari hadi July 2013 zaidi ya ajali tisa zimetokea katika daraja hilo zikihusisha magari makubwa saba na madogo mawili kutokana na madereva kushindwa kumudu magari yao na kulenga daraja hilo 
 Alisema pia basi hilo lina makosa ya kutembea nje ya ratiba, kuiba njia na kuzidisha abiria hivyo ofisi yake imechukua hatua ya kuvunja safari za mabasi ya kampuni ya Sumry za mchana na badala yake mabasi yote yataondoka Sumbawanga na Mpanda majira ya asubuhi pekee.

*NMB CHAPCHAP AKAUNTI YAWA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA


 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika Banda la benki ya NMB lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja ufunguliwa akaunti yake papo hapo na kupewa kadi ya kutolea pesa kwenye mashine muda huo huo.
 Baadhi ya Wateja waliofurika katika moja ya gazebo la NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB  katika Viwanja Vya Sabasaba wakifunguliwa akaunti ya ChapChap ambayo mteja ufunguliwa akaunti hiyo akiwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupewa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo na kwa gharama ya Shilingi Elfu kumi tu
 Wateja waliofika katika Moja ya gazebo lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB katika viwanja vya sabasaba wakipata maelezo mara baada ya kufungua akaunti zao za ChapChap na kukabidhiwa kadi zao za kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo kwa gharama nafuu ya shilingi Elfu Kumi tu.
 Afisa mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Bw Respecious Denis akitoa maelezo ya akaunti ya Chapchap kwa Mteja aliyemaliza kufungua akaunti hiyo mara baada ya kufika kwenye moja ya gazebo la Benki ya NMB lililopo katika Viwanja Vya sabasaba mapema leo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiwahudumia wateja waliofika katika gazebo la Benki ya NMB lililopo nje ya Banda la Benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti ukabidhiwa kadi yake ya kutolea pesa kwenye mashine za NMB papo hapo
 Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakiendelea na zoezi la kuwafungulia akaunti ya Chapchap wateja waliofika katika moja ya gazebo la Benki ya NMB kwaajili ya kufungua akaunti  ya Chapchap Kulia Ni baadhi ya Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB wakijiandaa kwaajili ya kumpiga Picha mteja aliyefika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap.
 Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Maana Katuli akimpiga picha mteja aliyefika katika Banda la NMB kwaajili ya Kufungua Akaunti ya Chapchap ambapo mteja akimaliza kufunguliwa akaunti anakabidhiwa na kadi yake ya kutolea pesa papo hapo
 Wateja wakipata maelezo ya kutosha kutoka Kwa Maafisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB
 Mteja akichukuliwa alama za vidole na mmoja kati ya maafisa mauzo ya nje wa benki ya NMB waliokuwa wakimuhudumia wakati mteja huyo alipofika kwaajili ya kufungua akaunti ya Chapchap
Afisa Mauzo ya Nje wa Benki ya NMB Batuli Suna akichukua alama za vidole vya mteja alifika katika banda la benki ya NMB kwaajili ya Kufungua akaunti ya Chapchap katika Maonyesho ya 37 ya Kibiashara ya Kimataifa. 

Saturday, July 6, 2013

* MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM LEO


 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipozungumza nao leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika ukumbini hapo kuzungumza nao leo.
Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao.

*WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAFURIKA KUSHUHUDIA TAMASHA LA FILAMU LA GRAND MALT


Wananchi waliofurika katika Tamasha la Filamu la Grand Malt linalofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
********************************
 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWANZO MWISHO! Leo ni leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, wakati kutakapofungwa rasmi Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima.

Huku wasanii wote mashuhuri wa filamu wakitarajiwa pia kufanya vitu vyao jukwaani, kazi kubwa itakuwa kwa burudani kali zitakazotolewa wakati wa kufunga tamasha hilo.


Mbali na hilo, pia kutakuwa na shindano kali hatua ya fainali ya kusaka wakali wa kurap pamoja na kukata nyonga, ambao nao watajiondokea na kitita kikubwa cha fedha.

Akizungumzia hilo, Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema kutakuwa na mambo makubwa zaidi uwanjani hapo na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kile kitakachoendelea.


 “Kila kitu kipo tayari na wasanii wote wakali wa filamu watakuwepo ili kutoa burudani kwa mashabiki waliofika hapa, huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa,” alisema.

Baadhi ya wasanii wa filamu wanaotarajiwa kuwepo ni Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’, Shamsa Ford, Ritchie Ritchie, Steven Jacob ‘JB’, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Hashim Kambi na wengineo wengi.

 Akizungumzia hilo, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona tamasha hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akitaka mashabiki kufurika Nyamagana leo kuona kile kinachoendelea.

“Hapa Mwanza tumeshuhudia vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kuona mashabiki walivyolipokea tamasha hili, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Katika mashindano ya kurap na kucheza katika kila eneo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na Sh 200,000 wa pili Sh 100,000 na watatu Sh 50,000.

Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika leo, huku wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.

Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

*MLINZI WA MAKAO MAKUU YA CUF MUHARAMI ABDALLAH SHAABAN TANGANYIKA AMEZIKWA LEO


 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfankazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail
 Sehemu ya waombolezaji
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji wengine.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea.

*WAMASAI KUTOKA MKOANI ARUSHA WATEMBELEA BANDA LA AICC LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM.


.Katibu Mhitasi wa Arusha Intarnational Confrerence Centre. Joyce Mollel (kushoto) akiwaonyesha baadhi ya akinamama wa kikundi cha Masai cha Munduli Arusha shughuli wanazotoa, wakati akimama hao walipotembelea katika banda lao lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Wednesday, July 3, 2013

*NBC BANK & AFRICAN FIRST LADIES SUMMIT AFRICA, MKURUGENZI WA NBC ATOA SOMO


 Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa  Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD),  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.
 Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.  
Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa  Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo. 

*JUMLA YA SH.MILIONI 3, 250,000 REDD'S MISS TEMEKE 2013 KUJINYAKULIA ZAWADI ZA


Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo sambamba na wasanii watakaotumbuiza siku hiyo Ben Paul na Luiza Mbutu wa bendi ya Twanga pepeta ambapo shindano hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili kushoto ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tz Albert Makoye.

Luiza Mbutu, akizungumza wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.
*****************************************
MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika keshokutwa siku ya Ijumaa Julai 5, mwaka huu, ataondoka na zawadi nono zenye jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo, yaliyofanyika mwaka huu.
Mshindi huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni 3,250,000.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha Sh.800,000 pesa taslim na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.
Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa mafanikio makubwa.
Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super Bokilo na Charles.
Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa,  Hyness Oscar, Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo .                                                                 
Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym & Spa, 100.5 Times FM na Kitwe General Traders. Mbali ya wadhamini hao pia Redds Miss Temeke imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu na mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu hasa kwa upande wa zawadi.
Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
BMP Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka wa 18 sasa, inatanguliza shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kuandaa Miss Temeke kwa ufanisi katika muda wote huo, shukrani sana.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions