Friday, June 27, 2014

MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA VIPI CCM ITAWABWAGA, ASHANGAA KUAMBIWA ANA MASLAHI BINAFSI KUWATETEA MAMALISHE

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo-
Jun 27, 2014

NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.
Amesema, uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.
Mtemvu amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo, mjini Dar es Salaam.
"Wapinzani baada ya kuona kuwa hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona wanavyotapatapa, mara eti huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia kwenye chaguzi, kuweka mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini hata wafanyeje CCM itawabwaga tu", alisema Mtemvu.
Mtemvu alisema, pale ambapo wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au udiwani ni pale ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.
"Ikifika acheni mambo ya kuanza mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi ambayo husababishwa na baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka wagombea kwa lazima, tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani hawapati hata kiti kimoja cha cha mtaa", alisema Mtemvu.Mtemvu aliwataka wana-CCM pia kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka nafasi ambao wana fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi kuwa wagombea kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.
Aliwataka mtu anapowajia kwa fedha kuzipokea na kuzila, lakini wakati waanapofikia maamuzi muhimu kwenye uchaguzi wahakikishe wanachagua yule wanayemfahamu kwa thati kwamba anao uwezo wa uongozi.
Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana fedha, hivyo watu wa aina hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.

Mtemvu alisema kiongozi mwenye uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote yupo na watu na anajali maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni wake tu.



"Mfano ni kama hivi tunavyofanya sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara tunapigania wanyonge, juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe hovyo, japo baadhi ya watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti nina maslahi binafsi, khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu kama siyo uzushi ni nini?" alisema Mtevu. 

U.S. EMBASSY DAR ES SALAAM CELEBRATES THE 238th ANNIVERSARY OF AMERICAN INDEPENDENCE.

United States Ambassador to Tanzania Mark B. Childress (left) and Tanzania’s Minister for Natural Resources and Tourism Lazaro Nyalandu toastthe 238th anniversary of American Independence and the bonds of friendship between the two countries.  Minister Nyalandu joined scores of Tanzanians, members of the diplomatic corps, and other distinguished guests at a colorful Independence Day reception at the U.S. Embassy in Dar es Salaam on June 26, 2014. (Photo courtesy of the American Embassy)

        U.S. Embassy Tanzania
                    Press Release

June 27, 2014
U.S. Embassy Dar es Salaam Celebrates the
238th Anniversary of American Independence
In celebration of the 238th anniversary of American Independence, United States Ambassador to Tanzania Mark Childress hosted a colorful reception at the U.S. Embassy grounds on June 26 in Dar es Salaam.  The event focused on four iconic cities in the U.S.: Boston, Los Angeles, Chicago and New Orleans, and finished off with a fireworks display.  The guest of honor from the Government of Tanzania was Hon. Lazaro Nyalandu, Minister for Natural Resources and Tourism. 
Addressing an audience of approximately 500 guests, Ambassador Childress remarked that both the United States and Tanzania stand for liberty, justice and prosperity.  At his first Independence Day celebration as the U.S. Ambassador to Tanzania, Ambassador Childress pledged to further strengthen the friendship between the two nations.  More specifically, Ambassador Childress said he will work closely with the Government and People of Tanzania to address the problem of wildlife trafficking.
In his remarks, Hon. Lazaro Nyalandu congratulated the American people on the occasion of their Independence Day, and remarked on the birth of the relationship between the U.S. and Tanzania with the close friendship between the late Mwalimu Julius Nyerere and the late President John F. Kennedy.  Minister Nyalandu also commended Ambassador Childress for his commitment to wildlife conservation, and pledged to ensure Tanzania does all that is within its powers to combat the problem of elephant poaching.
The United States’ Independence Day, commonly referred to as Fourth of July, is celebrated to commemorate the adoption of the Declaration of Independence on July 4, 1776, announcing the separation of America from Great Britain.

BALOZI IDDI AFUNGUA MSIKITI WA IJUMAA WA KIJIJI CHA MAMBOLEO BAADA YA KUFANYIWA UKARABATI

  Balozi Seif akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Kiboje Mamboleo mara baada kuufungua msikiti wao wa Ijumaa uliofanyiwa matengenezo makubwa.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza Hassanali akielezea mikakati ya kamati ya ujenzi wa misikiti, Madrasa na maskuli nchini ilivyopania kuendeleza malengo yake.
*********************************************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezikumbusha Kamati za Misikiti hapa  nchini kuendelea kuwa imara kwa kutowaruhusu watu wanaopenda kujipenyeza ndani ya kamati hizo kwa nia ya kuanza kutoa madarasa ya uchochezi na kuwagawa waumini kimadhehebu.
Alisema uimara huo ndio njia sahihi itakayoilinda misikiti hiyo na wimbi la vurugu na migogoro ambayo hatiae husababisha mmong’onyoko mkubwa wa  ukosefu wa maadili  katika jamii za kiislamu.
Akiufungua msikiti mpya wa Ijumaa uliofanyiwa matengenezo makubwa katika Kijiji cha Kiboje Mambo leo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema msikiti ni taasisi yenye mchango mkubwa wa kuutangaza ukweli dhidi ya unafiki pamoja na mambo ya kheri kwa jamii ya Kiislamu.
Balozi Seif alisema katika kuihuisha nyumba ya Mwenyezi Muungu  Msikiti ni vyema kwa waumini hao mbali ya kutekeleza vipindi vya sala lakini pia ni vyema wakaendeleza madarasa hasa kipindi hichi kinachokaribia cha  mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kujifunza masuala ya dini yao.
Alisema waumini wa dini ya  Kiislamu wanaotekeleza ibada zao na kusimamisha sala katika vipindi vitano kwa siku hupata baraka na neema ya kuwa wageni wa mola wao aliyewaumba.
“ Nani miongoni mwetu hataki kuwa mgeni wa mola wake mara tano ? Kama jawabu ni ndio basi tuhakikishe tunaswali mara tano kama tulivyoamrishwa na mola wetu. Na zile Baraza la manzese zisiwepo tena hapa mtaani penu“. Alisisitiza Balozi Seif.   
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi wananchi wa maeneo hayo hasa vijana kuachana na maasi ya unywaji pombe kiholela ambayo huchangia vitendo vya wizi wa mazao na mifugo katika maeneo mbali mbali nchini.
Alisema hivi sasa jamii imekuwa ikishuhudia mmong’onyoko mkubwa wa utamaduni wa Kiislamu na kupelekea kuibuka kwa vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa watoto na wanawake kijinsia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi watu wenye kupenda kunywa pombe kuachana na tabia hiyo inayozototesha hata afya zao na badala yake waelekeze  juhudi zao katika kilimo cha mazao ya biashara na chakula kwa lengo la kujijengea hatma njema ya baadaye.
Aliipongeza Kamati ya uendelezaji wa ujenzi wa misikiti, madrasa na maskuli Nchini kwa uamuzi wake wa kuufanyia matengenezo makubwa msikiti huo wa Kiboje Mamboleo ambao ulikuwa katika hali mbaya.
Balozi Seif alielezea imani yake kwamba waumini wa msikiti huo wataendelea kuutunza na kujiepusha na migogoro ya kugombania uongozi ambao hatiae huzaa chuki na hasama zisizo kwisha kwa kipindi kirefu.
“ Misikiti sio sehemu ya kutangazwa sera za siasa kama Viongozi na wahutubu katika baadhi ya misikiti kupendelea kukashifu viongozi waliopo madarakani  wakati kinachowapeleka  kwenye nyumba hiyo tukufu ni kufanya ibada pekee “. Alifafanua Balozi Seif.
Aliwataka na kuwahimiza waumini hao pamoja na wananchi wa maeneo hayo kuwakataa na kuwatenga watu wote waliojikubalisha kubeba cheche ya shari na utenganifu ndani ya jamii.
Akisoma risala ya waumini na wananchi hao wa Kiboje Mamboleo Ustadhi Juma Abdulla alisema wana jamii hao wameelezea faraja yao kutokana na kumalizika kwa ujenzi wa msikiti huo.
Ustadhi Juma Abdulla hata  hivyo alisema bado zipo baadhi ya changa moto zinazoendelea kuwakabili wana jamii hao wa Kiboje Mambo leo ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu kwao na kizazi chao.
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo Ustadhi Juma alisema kuwa ni pamoja na madrasa, eneo la michezo ya watoto wa kiislamu hasa wakati wa siku kuu pamoja na matengenezo ya chuo cha Qurani kilichopo jirani na msikiti huo.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa Misikiti, madrasa na majengo ya skuli hapa Zanzibar ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza Hassanali alisema kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi itaendelea kuongeza nguvu zake kwenye ujenzi wa majengo ya taasisi hizo yenye upungufu hapa Nchini.
Mh. Raza aliwahakikishia wana jamii hao wa Kiboje Mamboleo  kwamba uongozi wa Jimbo hilo uko katika jitihada za makusudi katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wana jamii hao ikiwemo ya ubovu wa bara bara.
Msikiti wa Kijiji cha Kiboje Mamboleo uliofanyiwa matengenezo makubwa hivi sasa una uwezo wa kusaliwa sala ya kawaida au ile ya Ijumaa na waumini wasiopunguwa mia tatu.

RAIS KIKWETE AONGOZA MKUTANO WA KAMATI YA VIONGOZI WA AFRIKA KUHUSU TABIA NCHI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Kuhusu Tabia Nchi  ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014
PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MPYA WA MISRI MHE ABDEL FATTAH Al-SISI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014
PICHA NA IKULU

MARCIO MAXIMO ASAINI MKATABA WAMIAKA MIWILI KUKINOA KIKOSI CHA YANGA

Kocha Mkuu mpya wa Yanga SC Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kulia ni msaidizi wake Leonado Neiva.
KOCHA Mbrazil Marcio Maximo leo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Young Africans pamoja na msaidizi wake Leonadro Neiva ambao wamesema wamekuja kuisaidia Yanga iweze kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Maximo amesema anajiskia furaha sana kurudi kufanya kazi Tanzania, kwani watu wake ni wakarimu, wapenda mpira hivyo anaona kama yupo nyumbani japo awamu hii ni kwa majukumu ya ngazi ya klabu tofauti na awali alipokua ngazi ya Taifa.
Nimekuja kufanya kazi na Yanga, nawashukuru viongozi wake kwa kuamua kuniamini na kunipa nafasi hii, wamenifuatilia kwa awamu tatu mfululizo na hatimaye safari hii wamefanikiwa kunipata kwa kushirikiana na wakala wangu Ally Mlei sasa kazi ni moja tu kuijenga Yanga.
"Jumatatu naanza kazi moja kwa moja pamoja na msaidizi wangu Neiva kwa kushirikiana na kocha wa kikosi cha U-20, wachezaji waliopo na wachezaji wa kikosi cha U20 watakua wakifanya mazoezi pamoja alisema" Maximo".
Natambua tuna wachezaji wengi katika timu za Taifa mbalimbali ikiwemo ya Tanzania (Taifa Stars), Uganda  (The Cranes) na Rwanda (Amavubi) ambao wapo wanayatumikia mataifa yao, na punde watakapomaliza majukumu hayo wataungana nasi kwa maandalizi.
Kuhusu Kaseja yale yalishapita, najua ni kipa mzuri mwenye uwezo na uzoefu wa kutosha na kipindi hiki najivunia kuwa na makipa watatu wenye uwezo mzuri, Yaliyopita Yameshapita yalikuwa ni timu ya Taifa na sasa tumekutana Yanga kazi yetu ni moja tu kuifanya klabu iwe kwenye hadhi ya Kimataifa zaidi.
Naye kocha msaidizi Leonado Neiva amesema tumekuja kufanya kazi, kwa kushirikiana na wachezaji waliopo kutoka sehem mbambali barani Afrika na Amerika tutapata mchanganyiko mzuri wa uchezaji.
Wakala wa Maximo Barani Afrika Bw Ally Mlehi kwa upande wake amewaomba wapenzi, wanachama na washabiki wa Yanga kuwa wavumilivu kwani soka ni tofauti ni chai ambayo ukikoroga sukari tu unasikia utamu, badala yake wanapaswa kuwapa muda makocha na baadae wataaona matunda yake. HABARI NA PICHA KWA HISANI YA http://www.youngafricans.co.tz/

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAWASILISHA MPANGO MKAKATI WA TAKWIMU ZA KILIMO KWA WADAU

 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke  akizungumza na wadau mbalimbali  wakati wa kujadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo leo jijini Dar es salaam. Mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kukusanya takwimu sahihi zinazokidhi viwango vya ndani na vile vya kimataifa.
 Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini Tanzania Bi. Diana Tampelman  akizungumza na waandishi wa habari kupongeza  hatua iliyofikiwa katika kukamilisha Mpango mkakati wa Takwimu za Kilimo nchini Tanzania  na kueleza  kuwa hatua hiyo inaendana na  Mpango wa Dunia  ulioanzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuboresha takwimu za kilimo maeneo ya vijijini.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Kijadili Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
*******************************
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  inakamilisha  Mpango mkakati  wa Takwimu za Kilimo wa mwaka 2014/15  mpaka 2018/19  utakaoiwezesha Ofisi  hiyo kuendesha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za kilimo nchini kila baada ya miaka 5.
Akizungumza wakati wa mkutano uliohusisha wadau mbalimbali wa kupitia  na kujadili rasimu ya mwisho ya mpango huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu kukusanya takwimu sahihi zinazokidhi viwango vya ndani na vile vya kimataifa.
Amesema  mpango mkakati huo unalenga kuboresha shughuli za ukusanyaji wa takwimu za kilimo  hapa nchini  kwa kujenga mfumo mmoja wa utoaji wa takwimu za Kilimo kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuliko ilivyo sasa na kubainisha kuwa taarifa zote za shughuli za kilimo nchini zitaingizwa kwenye mfumo wa serikali.
“Hapa tumekutana wadau mbalimbali kutoka  serikalini kwa maana ya wizara husika  na  wawakilishi kutoka mashirika ya maendeleo, lengo letu ni kupitia na kujadili rasimu hii ya mwisho itakayotuwezesha kujenga uwezo wa ndani wa  ukusanyaji wa takwimu za kilimo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka taifa’’ Amesema
Amefafanua  kuwa mpango huo utaiwezesha Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bara na ile ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar kupata takwimu za shughuli zote za kilimo kuanzia wazalishaji wenyewe, hali ya kilimo, mazao, masoko pia kutoa mwelekeo wa nini kifanyike kuboresha sekta hizo kupitia takwimu zitakazokusanywa.
Aidha, amesema kuwa vipaumbele vya mpango huo vimeshaainishwa na kuwekwa mbele ya wadau ili kuwezesha upatikanaji wa nyenzo na uwezo wa kutekeleza mpango huo.
Kuhusu kufanikisha  mpango huo Bw. Oyuke  amesema kuwa jopo la taifa la wataalam  limeundwa likihusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na ile ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, Wizara husika za Kilimo, Chakula na Ushirika,Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Maliasili na Utalii pamoja na wataam kutoka mashirika ya maendeleo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani(FAO) nchini Tanzania Bi. Diana Tampelman  amepongeza  hatua iliyofikiwa katika kukamilisha Mpango mkakati huo nchini Tanzania  na kueleza  kuwa hatua hiyo inaendana na  Mpango wa Dunia  ulioanzishwa mwaka 2010 kwa lengo la kuboresha takwimu za kilimo maeneo ya vijijini.
“Tunapongeza hatua hizi na tutaongeza nguvu zetu katika mpango huu ili kupata uhalisia wa shughuli za kilimo Tanzania kuhusu nani kazalisha nini na kwa kiwango gani ingawa watu wanaweza kushindwa kuona umuhimu wake lakini tunajua kuwa taarifa hizi ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi” Amesema Diana.
Naye mtaalam kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Mzee Mohammed Mzee akiwasilisha mada kuhusu Hali ya Takwimu za kilimo nchini amesema kuwa kwa kipindi kirefu takwimu za kilimo zimekuwa zikipatikana kupitia Wizara na Taasisi zenye dhamana ya usimamizi wa sekta ya kilimo na kusababisha upatikanaji wa takwimu zinazotofautiana kutokana na njia zilizotumika wakati wa ukusanyaji wa takwimu hizo.
“Kisheria Ofisi ya Taifa ya Takwimu hapa nchini ndio yenye dhamana ya kukusanya  na kusambaza takwimu, suala la ukusanyaji wa takwimu lina njia zake, kumekuwa na shida ya ya njia za ukusanyaji wa takwimu hizi na wakati mwingine takwimu kutofautiana ,kukamilika kwa mpango mkakati huu kutaliondoa tatizo hili” Amesema.

MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA KEKO, ATOA POLE KWA WAATHIRIKA

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam. Mtemvu amewapa pole walipoteza mali zao kutokana na moto huo ambao chanzo cha ke hakijajulikana.  Hadi inakisiwa imepatikana hasara ya zaidi ya sh. milioni 97.
 Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
 Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
 Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo,

HATUA YA MTOANO 16 BORA KOMBE LA DUNIA,

1:- JUNI 28,  MJINI BELO HORIZOTE
BRAZIL v/s CHILE
Mshindi kati ya Brazil na Chile, atacheza na Msindi wa kati ya Colombia na Uruguay

2:- JUNI 28, MJINI RIO DE JENEIRO
COLOMBIA v/s URUGUAY
**************************************************
3:- JUNI 30, MJINI BRASILIA 
UFARANSA v/s NIGERIA

4:- JUNI 30, MJINI  PORTO ALEGRE
UJERUMANI v/s MSHINDI WA KUNDI H
********************************************************
5:- JUNI 29 MJINI FORTALEZA
UHOLANZA v/s MEXICO
Mshindi kati ya Uholanza na Mexico, atacheza na mshindi kati ya Costarica na Ugiriki
JUNI 29 MJINI RECIFE
COSTA RICA v/s UGIRIKI

JULAI 1 MJINI SAO PAULO
ARGENTINA v/S SWITZERLAND

JULAI 1 
MSHINDI WA KUNDI H v/S MAREKANI
Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Mashindano ya soka kombe la dunia yanaendelea kunoga na kupamba moto nchini Brazil yakijumuisha jumla ya wachezaji 892 wanaoshiriki mashindano wa mpira wa miguu duniani maarufu “Fifa World Cup” ya mwaka 2014.
Mashindano hayo yamepambwa na majina ya wachezaji mbalimbali Mastaa kutoka nchi zinazoshiriki kinyang’anyiro hicho kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA, wachezaji wenye majina yenye herufi “M” ndio wanaoongoza kwa idadi kubwa katika michuano hiyo ambao jumla yao ikiwa ni 85.
Miongoni mwa wachezaji hao ni mshambuliaji Lionel Messi kutoka Argentina, Thomas Mülar kutoka Ujerumani,John Obi Mikel kutoka Nigeria, Hossein Mahini kutoka Iran na  wachezaji wengine kutoka mataifa yanayoshiki finali hizo.
Majina mengine 807 ya wachezaji yapo katika herufi “A” hadi “Z” ukiyatoa yale ya herufi “M” ambapo  herufi A wapo wachezaji 68, B 69, C 57, D 56, E 21, 25, G 47, H 40, I wachezaji 17, J 42, K 42, L 30, N 17, O 23, P 40 na Q mchezaji mmoja, R 43, S 70, T 19, U wachezaji watano, V 37, W, 16, X  wachezaji wawili, Y na Z wachezaji 10.
Katika mashindano hayo kuna jumla ya nafasi 736 za wachezaji ambapo kuna magolokipa 96, walinzi 230, walinzi wa kati 250 na washambuliaji 160. 
Wachezaji hao wanatoka katika timu za mataifa ya Algeria, Argentina, Australia, Ubelgiji,  Bosnia na Herzegovina, Brazil, Cameroon, Chile, Colombia, Costa Rica, Ivory Coast, Croatia, Ecuador, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ghana.
Mataifa mengine yanayoshiki fainali hizo ni Ugiriki, Honduras, Iran, Italia, Japan, Jamuhuri ya Korea, Mexico, Uholanzi, Nigeria, Ureno, Urusi, Hispania, Switzerland, Uruguay na Marekani.
Wachezaji hao wanaounda timu za mataifa yao kwa kutokana na uraia wao aidha wa kuzaliwa au kujiandikisha na wanacheza mpira katika vilabu mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA,  wachezaji 14 wanazechezea timu ya Bayern Muenchen,wachezaji 14 wanazechezea timu ya Manchester United, 13 Barcelona, 12 Chelsea, 12 Juventus,  12 Real Madrid,  12 SSC Napoli, 10 Liverpool, 10 Manchester City,  10 Paris Saint-Germai na  wachezaji 10 wanachezea timu ya Arsenal.
Vilabu vingine vilivyotoa wachezaji wanaoshiriki faina hizi ni Atletico Madrid wachezaji 9, FC Porto wachezaji 9,  FC Internazionale wachezaji 8,  AC Milan wachezaji 8,  Schalke 04 wachezaji 7, FC Zenit St. Petersburg wachezaji 7,  FC Dynamo Moscow  wachezaji 7,  SS Lazio wachezaji 7, Southampton FC wachezaji 7, VfL Wolfsburg wachezaji 7, Tottenham Hotspur wachezaji 6,  Newcastle United wachezaji 6, FC Basel wachezaji 6, Everton wachezaji 6,  CSKA Moscow wachezaji 6,  Borussia Dortmund wachezaji 6, AS Roma wachezaji 5, Feyenoord Rotterdam wachezaji 5, Fenerbahce SK wachezaji 5,  FSV Mainz 05 na  Galatasaray SK  zote zimetoa wachezaji watano kila mmoja.
Ili kuhakikisha timu za mataifa hayo zinakuwa na mafanikio wapo jumla ya makocha 32 wa timu za mataifa hayo ambao wanaongoza benchi la ufaundi kwa timu zao.
Fainali  mwaka huu zilianza 12 Juni na zinatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 kwa kwa mechi ya fainali ambayo itaamua nani atatawazwa kuwa mwamba wa soka duniani baadya ya bingwa mtetezi Hispania kutolewa mapema katika mzunguko wa kwanza wa mashindano haya.
Mpaka sasa hadi kufikia kipindi hiki cha hatua ya pili ya timu 16 bora, miamba iliyofanikiwa kupenya katika hatua hiyo kutoka kundi A ni Brazil na Mexco, kundi B Uholanzi na Chile, kundi C ni Columbia na Ugiriki, kundi D Costa Rica na Uruguay, kundi E ni Ufaransa na Swirtzerland, kundi F ni Argentina na Nigeria, kundi G ni Ujerumani na Marekani na kutoka kundi H timu zilizopenya ni Ubelgiji na Algeria.
Kigenga cha hatua ya timu 16 bora kitapulizwa Juni 28 mwaka huukwa timu ya wenyeji wa mashindano Brazil kuvaana na Chile.
Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Columbia ambao watacheza na Uruguay, Uholanzi watacheza na Mexco, Costa Rica watacheza na Ugiriki, Ufaransa watacheza na Nigeria, Ujerumani watacheza na Algeria, Argentina watacheza na Swirtzerland na kipenga cha mwisho katika hatua hii kitakuwa kati ya Ubelgiji ambao watavaana na Marekani hapo Julai Mosi mwaka huu katika dimba la Arena Fonte Nova, Salvador nchini Brazil.

Mataifa yaliyofuzu kushriki fainali za mwaka huu ni 32, ambapo imekuwa na fainali ya 19 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1930. Mataifa hayo yanatoka katika bara la Africa, Asia, Amerika ya kaskazini, Amerika ya kusini, Oceania na Ulaya.

TBC YAKABIDHIWA GARI LA KURUSHIA MATANGAZO NA SERIKALI YA CHINA

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana
 Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akijadiliana na jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.

SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TBC LAKABIDHIWA RASMI GARI LA KURUSHIA MATANGAZO NA SERIKALI YA CHINA

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana
 Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akijadiliana na jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China jana jijini Dar es Salaam.
 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China jana jijini Dar es Salaam.