Monday, March 31, 2014

'BIG RESULTS NOW' YAKUSANYA MABILIONI KWA KIPINDI CHA NUSU MWAKA

 Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, leo Machi 28, 2014. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now). 
 Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
 Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
Baadhi ya 'Mablogger', wakiwa bize wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha.
**************************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Kibaha 
Serikali imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 

Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu.

Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.  

Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia. 
Alisema huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha  viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki. 

Aidha, viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana. Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka. 

Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16.

*BALAA LA MVUA ILIYONYESHA JIJINI DAR JANA




Vijana wakisaidia kulikwamua gari la Polisi, lililokwama katika shimo lililokuwa halionekani kutokana na maji kujaa katika njia nyingi za barabara eneo la Kiwalani jijini Dar es Salaam, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini.
Viaja wakijipatia ajila ya ghafla kusaidia kulitoa gari lililozama kutokana na mvua zinazoendelea jijini.
Mmiliki wa gari lenye namba za usajili T 684 BEG, akiangalia gari lake lililoangukiwa na mti nje ya Hospitali ya Kairuki, kutokana na mvua iliyonyesha jijini Dar jana.
 
Mkazi wa Msasani, akitoka nje ya nyumba ake baada ya kujaa maji.
Hapa ni Nyumba za Dar Villa zilizopo Chama TJM. Picha na Francis Dande

*WANAHARAKATI WAMUUNGA MKONO JK KUPAMBANA NA UJANGILI


DSC_0079
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale,akizindu rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.

Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.(Picha na Zainul Mzige).
****************************************
Na. Zainul Mzige.
Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.

Mratibu wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni.
Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.

“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema.
Aliongeza kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi ya wanyamapori.
DSC_0037
Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.
 Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

*WACHEKI WALIONG'ARA KWENYE RED CARPET YA UZINDUZI WA ZANZIBALICIOUS WOMEN GROUP @ ZANZIBAR OCEAN VIEW


DSC_0243
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi. Mwanaidi Salehe (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Uwezeshaji, Bi. Fatma Gharib Bilal wakati wa sherehe za uzinduzi wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious uliofanyika mwishoni mwa juma ndani ya Zanzibar Ocean View.Picha na Zainul Mzige.
DSC_0058
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious, Bi. Umul-kulthum Ansel (kulia) akipozi na MC wa shughuli Bi. Fauziat Abood (katikati) pamoja na mjumbe mmoja wa wajumbe Mariam Yusuph Otembo.
DSC_0063
Pichani juu na chini ni wageni waalikwa wakipata Ukodak kabla ya shughuli kuanza kwenye Red carpet.
DSC_0064DSC_0181
Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.
DSC_0027
DSC_0190DSC_0193DSC_0194DSC_0199DSC_0031DSC_0085DSC_0094DSC_0100DSC_0107DSC_0110DSC_0113DSC_0150DSC_0163DSC_0155DSC_0233DSC_0238DSC_0170DSC_0178DSC_0205DSC_0209DSC_0264DSC_0121DSC_0165DSC_0071DSC_0075DSC_0226DSC_0255  DSC_0253    DSC_0069  DSC_0079

WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO


Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia bi Prisca Ulomi akitoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika  Uandaaji wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mtandao,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum. 
*****************************************
Fatma Salum-Maelezo
Serikali yawatahadharisha wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuondoa vitendo vya uhalifu hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa kutambua umuhimu wa TEHAMA wameamua kuandaa muswada wa Sheria  za Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao (Cyber Laws).

Akieleza zaidi Bi Prisca amesema kuwa Muswada wa sheria hizo ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi (The Personal Data Protection Bill), Muswada wa Sheria ya Biashara ya Miamala ya Kielektroniki (Electronic  Transaction Bill), na Muswada wa Sheria ya Kuzuia Uhalifu kwa njia ya Kompyuta na Mtandao (Computer and Cyber Crimes Bills).

“Sheria hizo zitasaidia kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini kwa kudhibiti uhalifu kwa kutumia mitandao na kuwalinda watoto dhidi ya matumizi yasiyofaa ya mitandao”. alisema Bi Prisca.
Bi Prisca aliongeza kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuweka miundombinu ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha na kuharakisha utoaji wa huduma mbalimbali na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watu wanatumia vibaya teknolojia hiyo, hivyo kuna umuhimu wa kuwepo sheria zitakazodhibiti uhalifu kupitia mitandao.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  imetoa rai kwa wananchi kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake watumie vizuri mitandao hiyo kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla hali inayoweza kuathiri ukuaji wa sekta hiyo nchini

*WIZARA YA AFYA YAELEZEA MPANGO WA UPIMAJI AFYA WANANCHI KWA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 Meneja Masoko  na Elimu kwa Umma  toka  Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Bi Anjela Mziray akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu programu ya upimaji wa Afya kwa wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza inayoendeshwa na mfuko huo hapa nchini. Kulia ni Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja na kushoto ni Afisa habari ,Idara ya Habari Maelezo  Bi Fatma Salum.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika leo jijini Dar es salaam uliolenga kuelimisha wananchi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari,shinikizo la damu na Saratani.
************************************
Na frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaweka mikakati madhubuti kupambana na magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini.

Hayo yamesema na  Meneja Masoko  na Elimu kwa Umma  toka  Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray  wakati wa mkuatano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akieleza Bi Anjela amesema kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya imekuwa ikichukua juhudi za maksudi katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na Saratani za aina mbalimbali.

Akifafanua zaidi Bi Anjela amesema programu hiyo imekuja kutokana na ukweli kwamba magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka na yamekuwa tishio na kusababisha vifo vya watu wengi nchini na duniani ambapo takwimu za shirika la afya Duniani za mwaka 2012/2013 watu zaidi ya milioni 35 hufa kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Bi Anjela aliongeza kuwa kati ya waathirika wa magonjwa yasiyoambukiza milioni 28.1 wanatoka katika nchi zinazoendelea ambapo kwa Tanzania magonjwa hayo husababisha vifo mara 4 zaidi mijini ambavyo ni sawa na  asilimia 12.8 wakati asilimia 3.1 wapo vijijini.

 Akitolea Mfano Bi Anjela alisema katika zoezi la upimaji lililofanyika Dodoma Septemba, 2013 jumla ya watu 591 walipimwa kati yao 14  sawa na asilimia 2.3 waligundulika kuwa na kisukari, na 28 sawa na asilimia 5 walikuwa na shinikizo la damu, wakati  watu 128 sawa na asilimia 22 walikuwa na uzito uliokithiri.
Bi Anjela aliongeza kuwa katika zoezi lililofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam ocktoba, 2013 watu 450 walipimwa, nusu yao waligundulika kuwa na uzito uliokithiri na katika zoezi lililofanyika Zanzibar watu 273 walipimwa ambapo kati yao watu 10 sawa na asilimia 3.6  waligundulika kuwa na kisukari, watu 83 sawa na  asilimia 30.4 walikuwa na uzito uliokithiri.

Naye  Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja  alitoa wito kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi  na kuzingatia lishe bora ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo  na shinikizo la damu.


Katika jitihada za Kutoa huduma bora kwa wananchi  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebuni mkakati maalum ambao unajulikana kama Afya Bonanza ambayo ni Kampeni ya kupima afya na kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza  na inakusudiwa kufanyika mikoa yote hapa nchini ambapo  Zoezi hilo lilizunduliwa rasmi Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam  mwezi machi 2014