Saturday, April 19, 2014

MCHEZO WA YANGA v/s SIMBA NA MATOKEZO YOTE YA MICHEZO YA LEO



 Mshamuliaji wa Yanga, Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Simba, Nassor Chollo (kushoto) na Said Ndemla (katikati) wakati wa mchezo wa kufunga dimba la Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1. 

bao la Simba walioanza kushinda lilifungwa na Haruna Chanongo, katika dakika ya 76 baada ya Krosi safi ya beki William Lucian. Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 86 kupitia winga wake machachari, Simon Msuva, kwa shuti kali lililomshinda kipa Ivo Mapunda. hadi mwisho wa mchezo huo, Yanga 1-1 Simba.


MATOKEO KAMILI YA MICHEZO YA LIGI KUU ILIYOCHEZWA KWENYE VIWANJA SABA LEO:- 
Yanga 1 (Simon Msuva Dk 86') v/s Simba 1 (Haruna Chanongo 76'), 
Oljoro 1 v/s Mtibwa Sugar 1, Rhino Rangers 0 v/s Ruvu Shooting 2 (Hamis Kisuke Dk 10)', Elias Maguli Dk 17')
 Mbeya City 1 (Saad Kipanga Dk 75') v/s Mgambo 0, 
Coastal 0 v/s Kagera Sugar 1 (Themi Felix  Dk 50')
Tz Prisons 1  (Peter Michael Dk 54') v/s Ashanti 0
 JKT Ruvu 0 v/s Azam Fc 1 (Brian Umony Dk 79')
 Beki wa Simba, Issa Rashid, akijaribu kumtoka winga wa Yanga, Simon Msuva, wakati wa mchezo huo.


Wachezaki wa Simba, wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na haruna Chanongo.
 Simon Msuva, akishangilia bao lake aliloisawazishia Yanga...
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao lao la kusawazisha lililofungwa na Simon Msuva.
 Kikosi cha kwa nza cha Simba na makocha wake....
 Kikosi cha kwanza cha Yanga...

 Mshambuliaji wa Yanga , Hamis Kiiza akiruka kukwepa kwanja la beki wa simba, Nassor Chollo wakati wa mchezo huo. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka wachezaji wa Simba Ramadhan Singano (kulia) na Nassor Chollo.

AZAM FC WAKABIDHIWA KOMBE LAO LA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


Wachezaji wa Azam Fc, ambao ni Mabingwa wapya wa  Ligi ya Tanzania Bara  wakishangilia baada ya kukabidhiwa Kombe lao la ubingwa na kuweka historia ya kutwaa Ubingwa wa Soka kwa mara ya kwanza tangu walipopanda daraja na kuanza kucheza ligi kuu.
hafla hiyo ya kukabidhiwa kombe ilifanyika kwenye uwanja wa Azam complex Chamazi baada ya mchezo wao na JKT Ruvu ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0

MATOKEO KAMILI YA MICHEZO YA LIGI KUU ILIYOCHEZWA KWENYE VIWANJA SABA LEO:- 
Yanga 1 (Simon Msuva Dk 86') v/s Simba 1 (Haruna Chanongo 76'), 
Oljoro 1 v/s Mtibwa Sugar 1, Rhino Rangers 0 v/s Ruvu Shooting 2 (Hamis Kisuke Dk 10)', Elias Maguli Dk 17')
 Mbeya City 1 (Saad Kipanga Dk 75') v/s Mgambo 0, 
Coastal 0 v/s Kagera Sugar 1 (Themi Felix  Dk 50')
Tz Prisons 1  (Peter Michael Dk 54') v/s Ashanti 0
 JKT Ruvu 0 v/s Azam Fc 1 (Brian Umony Dk 79')

VIONGOZI WA JUMUIYA COLUMBUS, OHIO WAMFANYIA DINNER BALOZI LIBERATA MULAMULA NA MUMEWE


 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na katibu wa Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio Bi. Happiness Salukele wakiwemo wajumbe wa Jumuiya Nasra Murumah, Chiseko Hamisi na kushoto ni mweka hazina wa Jumuiya Bi. Vera Teri
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mumewe Bwn. George Mulamula wakikaribishwa kwenye mgahawa wa Mitchell's Steakhouse wa Columbus, Ohio na wajumbe wa Jumuiya wakiwemo viongozi kwenye chakula cha jioni walichomuandalia Mhe. Balozi na Mumewe. Mhe. Balozi Liberata Mulamula yupo Columbus kwa ajili ya Fundraisng ya Jumuiya ya Watanzania Columbus, Ohio itayaofanyika leo Jumamosi April 19, 2014 katika ukumbi wa Comfort Inn uliopo 1213 E. Dublin Granville Road, Columbus, Ohio na kiingilio ni $15 na muziki utaporomoshwa na Dj Luke kutoka DC.
 Wajumbe wakimpokea Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mumewe Bwn. George Mulamula mara tu walipowasili kwenye mgahawa wa Mitchell's Steakhouse, anayesalimia na Balozi ni mjumbe Michael Mngodo.
Kutoka kshoto ni katibu wa Jumuiya Bi. Happiness Salukele, Mume wa Balozi Bwn. George Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula, mweka hazina Bi. Vera Teri na mjumbe Nasra Murumah.
 Wajumbe wakiangalia menu tayari kwa kuagiza chakula cha jioni walichomuandalia Mhe. Balozi pamoja na Mumewe.
 Wajumbe wakiwemo kwenye chakula cha jioni walichomuandalia Balozi pamoja na mumewe.
 Kutoka kushoto ni Deo Mwalujuwa, mjumbe Joe Ngwilizi, mjumbe Michael Mngodo na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Columbus Ohio, Bwn Jimmy James.

19 WENGINE WATAJWA TAIFA STARS


 Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).

Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).

Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).

Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) naBayaga Athanas Fabian (Mbeya).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

MICHUANO YA BEACH SOCCER YAIVA
Michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.

Uzinduzi huo utaanza saa 5 asubuhi na mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MASHINDANO YA TANZANIA MOVIE TALENTS YAANZA LEO MKOANI MBEYA


 Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea muda huu katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
 
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
 Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano ya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
 
 Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano ya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
 Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.
Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea mkoani Mbeya muda huu.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.
Mpaka sasa Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.
Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

KUELEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO MJINI ZANZIBAR.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Muungano katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Muungano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo.
 Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua Kongamano la Muungano kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, leo.
  Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua Kongamano la Muungano kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano) Samia Suluhu, akizungumza machache wakati akimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua Kongamano la Muungano leo.
Viongozi waliohudhuria Kongamano hilo, wakiwa meza kuu. Wa pili (kulia) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kushoto) Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, (wa pili kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) na (kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais, Mohamed Aboud.