MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo katika ukumbi wa White House mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imemteua mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chambani, Pemba Mattr Said .(Picha na Bashir Nkoromo)
Tuesday, May 14, 2013
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)
Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara
Kuhusu: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.
USIRI
Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators).
Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii. Wachuuzi (Content Providers) nao hawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.
Suluhisho:
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)
UNYONYAJI
Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato. Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).
Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.
Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances) na hivyo “copyright Association” ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.
SULUHISHO
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kazi za Wasanii.
HITIMISHO
Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013.
Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013.
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MANZESE WAVAMIWA NA MASHETANI NA KUANGUKA HOVYO
Mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja aliyeanguka na kuweweseka leo mchana wakati akiwa shuleni hapo jambo ambalo lilizua hofu kubwa kwa wazazi na wanafunzi wa shule hiyo, huku baadhi ya wanafunzi wakitimua mbio huku na
huko bila kujitambua, jambo lililomfanya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kuwarusu wanafunzi wote kurejea majumbani na kukatis masomo. Haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha tatizo hilo, huku Maustaadh na wachungaji wakifika shuleni hapo na kuwaombea waliopatwa na tatizo
hilo na kukemea.
Imeelezwa kuwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Manzese Uzuri, jijini
Dar es Salaam, wamekumbwa na mashetani jambo lililowafanya kuwa wakianguka hovyo na kutimua mbio huku na huko madarasani huku
wakipiga makelele na kuongea maneno yasiyoeleweka.
Mmoja wa Wachungaji waliowahi kufika shuleni hapo akimfanyia
maombezi mmoja wa wanafunzi hao waliopatwa na tatizo hilo.
Monday, May 13, 2013
MASHUJAA BAND WAZINDUA VIDEO YAO YA RISASI KIDOLE NA FM ACADEMIA BAADA YA KUBUMA NA JB MPIANA
Rais wa Bendi ya Fm Academia, Nyoshi El-Saadat (kushoto) akipozi na Rais wa Bendi ya Mashujaa, Charz Baba (katikati) na Makamu wa Rais wa Fm, King Braize, wakati wa shoo ya uzinduzi wa Video mpya ya Risasi Kidole ya Mashujaa, uzinduzi huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Green Acres, Victoria jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nyoshi alimtunuku tuzi Charz na kumvisha ikiwa ni heshima ya kumtambua kuwa Rais wa bendi hiyo akimtakia mafanikio katika kusimamia na kuiendesha bendi hiyo kwa mafanikio.
Mwishoni mwa maka jana bendi hiyo ilizindua albam hiyo bila mafanikio wakati ilipomualika nguli wa muziki wa dansi, JB Mpiana kutoka Congo, na kupata mashabiki kiduchu huku umeme ukizingua katika viwanja vya Leaders na Jenereta kugoma kuwaka, jambo lililopelekea Mkurugnezi wa Bendi hiyo, Mama Sakina, kuanguka na kupoteza fahamu na kukimbizwa Hospitalini.
Wanenguaji wa Bendi ya Mashujaa, wakishambulia mbele ya mashabiki wao wakati wa uzinduzi huo.
Rais wa Fm Academia, Nyoshi (kushoto) akiwangoza wanenguaji wake kushambulia jukwaa wakati wa uzunduzi huo kwa staili zao 350 walizozitambulisha kati 700.
BREAKING NEEEEWZ!!! BASI LA MAJINJA LAPINDUKA NA KUJERUHI 24 MORO
HABARI ZILIZOUFIKIA MTANDAO HUU HIVI PUNDE ZINASEMA KUWA BASI LA ABIRIA LA MAJINJA LINALOFANYA SAFARI ZAKE DAR- MBEYA, LIMEPINDUKA ENEO LA NANE NANE MJINI MOROGO NA KUJERUHI JUMLA YA WATU 24.
CHANZO CHA HABARI HIZI KIMEELEZA KUWA BASI HILO LIMEPINDUKA BAADA YA DEREVA WAKE KUKWEPA KUGONGANA NA ROLI LILILOKUWA LIKITOKA DAR KUELEKEA MORO USO KWA USO WAKATI AKIJARIBU KULIPITA GARI JINGINE.
MAJERUHI WAMEKIMBIZWA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MKOA MOROGORO, HUKU DEREVA WA BASI HILO IKISEMEKANA KUTOWEKA AMA KUWA NI KATI YA MAJERUHI HAO.
CHUO KIKUU CHA ST JOHN'S CHANYAKUWA UBINGWA WA MASHINDANO YA POOL YA VYUO VIKUU
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (katikati) akimkabidhi nahodha wa chuo kikuu cha St.John’s, Mkole Mpangala fedha taslim Sh.500,000 baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’ katika mkoa wa Dodoma, (wa pili kushoto), mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani wa Dodoma (DOPA),Fred Mushi.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (mwenye suti) akifurahi pamoja na wachezaji wa chuo cha St. John’s baada ya kutwaa ubingwa wa ‘Safari Lager Higher Learing Pool Competition 2013’ Mkoa wa Dododma.
***************************
Na Mwandishi Wetu.Dodoma
CHUO kikuu cha St.John's, juzi kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashidano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa ya 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013' baada ya kukifunga chuo kikuu cha UDOM magoli 13-3 katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Mashindano hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla, yalifanyikia kwenye wa Royal Village.
Jumla ya vyuo vikuu vinne vya mkoani hapa vilishiriki mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Chuo cha St. John's kwa kutwaa ubingwa huo kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya kujinyakuia fedha taslim Sh.500,000 pia kitauwakilisha mkoa wa Dodoma katika fainali za taifa ambazo zitafanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es salaam.
Fainali hizo zitashirikisha vyuo vinane ambavyo vitaibuka mabingwa kwenye mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo.
Chuo cha UDOM kwa kushika nafasi ya pili kilizawadiwa Sh.300,000 huku chuo cha CBE kilichoshika nafasi ya tatu kiliondoka na Sh.200,000 na chuo cha Mipango kilipewa Sh.100,000 baada ya kushika nafasi ya nne.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Juma Daniel wa chuo cha Mipango alitwaa ubingwa huo na kujinyakulia fedha taslim Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa na Abdallah Abdallah wa chuo cha UDOM aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kujifunga kwa bahati mbaya alishika nafasi ya pilli na kupewa Sh.100,000.
Remi Jackson wa chuo cha UDOM naye alifanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mchezaji mmoja (wanawake) na hivyo kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa za mashindano hayo na Mwanaisha Abdallah wa chuo cha CBE alipewa Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya pili.
Kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Naibu Waziri wa Habari,VIjana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla aliwapongeza wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza kuuinua mchezo huo na kuufikisha hapa ulipofika.
Makalla pia aliwapongeza viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa kwa ushirikiano wao ambao umeendelea kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni vema mkaendeleza amani na ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool uendelee kumvutia kila Mtanzania, kwa kweli ni mchezo mzuri ambao na mimi nitaanza kujifunza.
Nakwa upande wa serikali inautambua kama ilivyo michezo mingine na wizara itaendelea kuwaunga mkono katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze kuiletea heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa,"alisema Makalla.
* RAIS KIKWETE AZINDUA JENGO LA SAYANSI KATIKA KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA TROPIKI LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na akiangalia katika darubini vimelea vya magonjwa ya mihogo vilivyo katika sehemu ya utafiti baada ya kuzindua rasmi rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo bnaada ya kuzindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Picha ya pamoja...
Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akiwa na Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso E. Lenhardt pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhe. Tonia Kandiero wakati wa uzinduzi rasmi rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU
Wednesday, November 28, 2012
*SHARO MILIONEA AZIKWA LEO MUHEZA NA MAMIA

Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele

Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkonona Msanii wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.
Tuesday, October 30, 2012
*AZAM WAMWANGUKIA KOCHA WALIOMTIMUA, NI BAADA YA KUMTIMUA KOCHA MPYA ALIYECHAPWA 3-1 NA SIMBA
![]() |
| Kocha aliefukuzwa Boris Bunjak |
![]() |
| Aliyekuwa Kocha wa Azam Stewart Hall |
KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
*GODFREY NA UPENDO WAMEREMETA
Bwana harusi Godfrey Mng'anyi akipozi kwa picha na mkewe, Upendo, wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanandoa hao walifunga ndoa yao katika Kanisa la Manzese. Bwana harusi ni mfanyabiasha na Bi Harusi ni mjasiliamali katika Ofisi yake ya Stationary.
Sunday, October 14, 2012
*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA MAHUJAJI JIJINI DAR JANA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud
Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika
kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na
kuwakabidhi Misahafu kila mmoja kabla ya
kuondoka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud
Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika
kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na
kuwakabidhi Misahafu kila mmoja kabla ya
kuondoka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Misahafu, mmoja kati ya
Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud
Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya
kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
Sehemu
ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka
kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege
kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Sehemu
ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka
kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege
kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Tuesday, October 9, 2012
*MWANAFUNZI ALIYEFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE AKIWA WODINI
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato hicho akiwa wadi namba 7B katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo jana, baada ya kulazwa kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe ambapo hivi sasa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.
Saturday, October 6, 2012
*RICK ROSS ALIVYOPAGAWISHA USIKU WA SERENGETI FIESTA LEADERS CLUB
Msanii wa muziki kutoka nchini marekani, Rick Ross, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha kubwa la Serengeti Fiesta, lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Mbali na msanii huyo pia walikuwapo wasanii kibao wa muziki wa Bongo Flava kutoka Bongo na nje ya Bongo.
Msanii AT, akishambilia jikwaa na mnenguaji wake wakati wa tamasha hilo.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Tamasha hilo, waliobahatika kujitokeza kushuhudia mashambulizi.
Sehemu ya mashabiki wakiburudika.
Tuesday, October 2, 2012
*THOMAS MASHALI KUKIPIGA NA BONDIA WA UGANDA SIKU YA NYERERE DAR
Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Bondia Medi Sebyala wa Uganda, litakalofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Mratibu wa Pambano hilo linalosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO, Regina Gwae, amesema mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Mashali anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vema nchini.
“Huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda Ulaya, ukaikimbia Afrika Mashariki, hivyo tumeona tumpe pambano Afrika Mashariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa,” alisema Regina.
Aliongeza kuwa, mazungumzo na bondia Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo ili ausaini baada ya kuupitia.
“Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, huwezi kuacha kuwataja Mashali na Sebyala,” alisema Regina.
Regina alisema wanataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala naye ni mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia mahiri nchini Fransis Cheka na Rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti.
Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye kuvutia wakiwemo mabondia chipkizi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Jonas Segu, mabondia wengine watakacheza utangulizi watatangazwa baadaye watakaosindikiza mpambano huo.
Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
Friday, September 14, 2012
*UNICEF YALIPIGA JEKI JESHI LA MAGEREZA
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima (kulia) akipokea msaada wa kijamii kutoka kwa Mwakilishi Msaidizi wa kitengo cha kuunganisha watoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa ( UNICEF) nchini Paul Edwards (kushoto) leo jijini Dare es Salaam. Msaada huo una vitu mbalimbali kama vyandarua, magodoro, mito, taulo na vifaa vya michezo.venye thamani ya shilingi ya dola za kimarekani 8,972. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Fidelis Mboya, Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima, akizungumza machache baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Magereza waliohudhuria Hafla ya makabidhiano ya msaada wa kijamii wa Vifaa mbalimbali kutoka UNICEF kwa watoto waliopo Magereza mawili ya watoto nchini Segerea na Ruanda (Mbeya), Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Slaam.
Sunday, September 2, 2012
ROSE LUCAS ATWAA TAJI LA REDD'S KANDA YA MASHARIKI 2012
Redd’s
Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas, akipunga mkono baada ya
kutangazwa mshindi na kujinyakulia taji hilo kwa kuwashinda warembo
wenzake 10 katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo
katika Hoteli ya Nashera 'mji kasoro Bahari'.
Redd’s
Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas (katikati) akipunga mkono kwa
furaha akiwa na washindi wenzake, mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na
Mshindi wa tatu Joyce Baluhi, baada kutangazwa washindi wa shindano
hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo, Warembo hawa
wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
Washiriki
wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kutangazwa kuingia katika hatua hiyo. Kutoka kushoto ni 6.
Zuhura Gora, 7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce
Baluhi.
Warembo
wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show yao ya pamoja ya
ufunguzi wa shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro
usiku wa kuamkia leo.
Wandaaji
wa mashindano ya Mikoa iliyoleta washiriki wa Miss Kanda ya Mashariki
wakitambiana huku Mwandaaji wa Mkoa wa Lindi, Ramadhan Shaha (katikati)
akionesha ishara ya ushindi aitumiayo mkiambiaji wa Kimataifa wa Jamaika
Bolt. Shaha alifanikiwa kutoa mshindi wa pili wa mashindano hayo.
Wengine kushoto ni Mwandaaji wa Mtwara, Rajab Mchata, Mwandaaji wa
Morogoro, Frank Ezekiel na kulia kabisa ni Mama Mchata.
Subscribe to:
Posts (Atom)































kj.jpg)
vf.jpg)




