Afisa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Themistocles Rumboyo akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa hadi kufikia Februari mwaka huu jumla ya maombi 56 ya makampuni ya huduma za ajira nchini yamewasilishwa kwa Kamishna wa Kazi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
Afisa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Omari Sama akijibu swali la waandishi wa habari waliotaka kujua taratibu za kusajili wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Ridhiwani Wema.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa
Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani
Wema
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo piuchani) kuhusu taarifa
za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu au makampuni binafsi kuhusiana na
maudhui ya Tamko la Serikali lililoziagiza wakala binafsi wa Huduma za Ajira kuwasilisha upya maombi ya usajili wa uwakala
kwa Kamishna wa Kazi.
PICHA ZOTE NA
FRANK MVUNGI- MAELEZO
No comments:
Post a Comment