Tuesday, May 21, 2013

*FLAVIANA MATATA ASHIRIKI MISA YA KUMBUKUMBU YA AJALI YA MV BUKOBA



 Flaviana Matata akiwasha mshumaa katika kaburi la Mama yake mzazi aliyefariki dunia katika ajali ya Meli ya Mv Bukoba, ikiwa ni miaka 17 tangu ilipotokea ajali hiyo ilipotokea. Flaviana aliwasha mshumaa huo ikiwa ni ishara ya kuomboleza akiungana na ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo, ambapo shughuli hiyo imefanyika leo katika Makaburi ya Igoma, jijini Mwanza, walikozikwa baadhi ya marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
 Flaviana Matata akishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki na baadhi ya waombolezaji waliopoteza ndugu zao katika ajali ya Meli ya MV Bukoba, wakiwasha mishumaa kwa pamoja ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka, wakati wa Ibada maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo.
 Flaviana Matata akiwa na Baba yake mzazi na ndugu, jamaa na marafiki katika Misa ya  maombelezo  Ajali ya MV Bukoba. Misa hiyo imefanyika leo, Igoma Jijini Mwanza.
Flaviana Matata akiwasili ofisini kwa Projest  Samson Kaija, ambaye ni General Manager wa Marine Services Company Ltd, ambao hushirikiana naye katika maombolezo ya Ajali hiyo ambapo mwaka jana aliwapa msaada wa maboya ya kuokolea maisha

* CCM YATOA ANGALIZO KWA WANAOJIPITISHA KUOMBA KUCHAGULIWA KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewaonya na kuwapiga marufuku, makada na wanachama wake wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao, kutothubutu kuanza kujipitipitisha kwa wapiga kura na kusema atakayefanya hivyo asimlaumu mtu kwa kitakachoamuliwa dhidi yake.

Kimesema sheria kanuni na taratibu zinazokiongoza Chama katika kupata wagombea wake ziko palepale na kwamba hakitamvumilia yeyote atakayebainika kuzikiuka.

Onyo hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya 
Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akiongea na waandishi wa habari kuhususu mkutano kati ya CCM na wabunge wake uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

"Viko vyombo vya habari ambavyo kwa makusudi vimepotosha ukweli kuhusu tulichoafikiana katika kikao kati ya CCM na wabunge wake. Si Mwenyekiti wa taifa wala Chama kilichoruhusu wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali kujipitishapitisha kwa wananchi.

"Nasisitiza nukuu hiyo ya baadhi ya vyombo vya habari si sahihi na ni ya kupotosha ukweli. Inaelekea kuna kikundi cha watu wenye mgombea wao wa kuchonga ambaye bila shaka anapungukiwa sifa, hivyo wanajaribu kumuongezea sifa kwa kumlisha Mwenyekiti maneno na kuwapa baadhi ya waandishi wa habari. Uhuni huo haukubaliki," alisema Nape.

Kwa mujibu wa Nape, licha ya ajenda kuhusu wana-CCM wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo udiwani, ubunge na urais kujadiliwa kwa kina katika kikao hicho, hitimisho na majumuisho ya Mwenyekiti wa CCM 
Taifa ilikuwa ni kukemea kwa nguvu zote pirikapirika hizo ambazo ni uvunjifu wa makusudi wa kanuni za Chama.Alisema kimsingi pirikapirika zinazofanywa na baadhi ya makada zinaweza kukigawa Chama na kuvuruga mshikamano na umoja uliopo ndani ya CCM.

Nape alisema CCM ina kanuni na taratibu zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa. Kanuni hizo ni pamoja na za uteuzi wa wagombea wa Chama kuingia kwenye vyombo vya dola toleo la Februari, mwaka 2010 na kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la mwaka 2012.

“Ni mwiko kwa kiongozi au mwanachama yeyote wa CCM kuunda vikundi visivyo rasmi ndani ya chama, au kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chini chini kinyume na ratiba ya uchaguzi na taratibu rasmi zilizowekwa” alisema.Katibu huyo alisema iwapo mwanachama yeyote atakiuka kwa makusudi na kuvunja taratibu hizo, Chama kitamwajibisha bila ya kumuonea haya na kwamba itakapofikia hapo asilaumiwe yeyote kwa kuwa ndivyo taratibu zinavyoagiza.

Akizungumzia malengo ya kikao hicho, alisema kililenga kutathimini utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM majimboni na kuangalia namna bora ya kuweka msukumo mpya na mkubwa zaidi kwa sehemu iliyobaki ya utekelezaji wake katika kipindi cha mwaka 2010/2015, ili kuhakikisha ahadi za Chama na wagombea wake zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Baadhi ya magazeti (Uhuru halimo) katika matoleo yao ya juzi, yalimnukuu Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwaruhusu wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuendelea na mchakato.

Magazeti hayo yalidai kuwa Rais aliruhusu hilo kutendeka huku 
akiwatahadharisha watakaokuwa tayari kufanya hivyo kuendesha kampeni zao kwa ustaarabu bila kuibua chuki na kujenga makundi kwa kuwa ni hatari kwa uhai wa Chama.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWENYEKITI MSTAAFU WA KAMATI TENDAJI YA BUNGE LA CHINA NA UJUMBE WAKE.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Bunge la China, Lu Youngxiang (wa pili kushoto) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Bunge la China, Lu Youngxiang (wa tatu kushoto) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

*FIFA YAMTEUA LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA



Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.

Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.

*MAMA SALMA AKUTANA NA DR JEROME PAULSON KUTOKA MAREKANI NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MADAKTARI WA WATOTO NCHINI


 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Daktari bingwa wa watoto Jerome Paulson, Mkurugenzi wa Afya ya watoto na Mazingira kutoka Chidren's National Medical Center ya huko Washington nchini Marekani aliyemtembelea Mama Salma kwenye ofisi ya WAMA jijini Dar es Salaam leo. Dr. Jerome amekuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa Madaktari Bingwa wa watoto hapa nchini kuhusu afya ya mtoto na mazingira  kufuatia makubaliano aliyoyafanya na Mama Salma wakati alipotembelea taasisi hiyo huko Washington mwaka 2012.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Daktari Bingwa wa watoto Jerome Paulson aliyeambatana na Mkewe pamoja na viongozi wa Chama cha Madaktari wa watoto hapa Tanzania (Paediatrc Association of Tanzania-PAT). Kutoka kushoto ni Dr. Augustino Masawe akifuatiwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa watoto nchini (PAT) Dr. Rodrick Kisenge, Mrs Jerome na kwa nyuma ni Dr. Francis Furia,Mjumbe na Dr. Hadija Mwamtemi, Mwekahazina wa chama hicho
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa Watoto Jerome Paulson kutoka Marekani na Viongozi wa Chama cha Madaktari wa Watoto hapa Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, leo.  PICHA NA JOHN LUKUWI

*TIMU 14 RCL KUUMANA RAUNDI YA PILI WIKIENDI



Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.

Timu zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Siku hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Stand United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Mjini Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.

Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.

*JK AONGOZA KIKAO CHA CCM MJINI DODOMA LEO



  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe, wakati wa Kikao Cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, kilichofanyika leo May 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa mkutano wa Kamati hiyo, leo Mei 21, 2013,  kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Picha na Bashir Nkoromo

Monday, May 20, 2013

*FULL MABONDIA WAKIWA NA MASHALI, MIYEYUSHO, MCHUMIATUMBO WASHINDWA KUFURUKUTA KWA TASWA FC YA LALA KWA BAO 2-1


 Kikosi cha Taswa Fc, TIMU ya Taswa Fc jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Full Mabondia, inayoundwa na mabondia mahiri wa Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilikutana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar jana mchana, huku timu ya mabondia ikiwakilishwa na mabondia kama, Thomas Mashali, Mchumiatumbo, Francis Miyeyusho, Majia, Kanda Kabongo, na wengine wengi. Picha zote na www.sufianimafoto.com
 Wadhamini wa timu ya Taswa, Kampuni ya TSN, pia walikuwepo viwanjani hapo wakionyesha kinywaji cha Chilly Willy, kinachotengezwa na kampuni hiyo. Pichani ni baadhi ya warembo wanaotangaza bidhaa za kampuni hiyo, wakiwa katika meza yao.
 Beki wa Taswa Fc, Juma Ramadhan, (nyuma) akimdhibiti mshambuliaji wa Full Mabondia, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Muhidin Sufiani 'Sufianimafoto' (kulia) akimfinya mchezaji wa Full Mabondia, wakati wa mchezo huo jana.
 Beki wa Taswa Fc, Elius Kambili, akiambaa na mpira.
 Beki wa Taswa Fc, Salim (kulia) akiondosha moja ya hatari mbele ya Bondia, Mchumiatumbo.
 Kipa wa Full Mabondia, akiwa golini huku akiwa peku peku, wakati wa mtanange huo jana.
 Zahoro Milanzi wa Taswa Fc, (kushoto) akiambaa na mpira wakati wa mtanange huo.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakipasha kabla ya kuanza kwa mtanange huo jana.
Sufianimafoto (katikati) akipozi na Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) na 'Chuji' (kulia) kabla ya kuanza kwa mtanange huo jana.
Benchi la Taswa Fc.

*MWASISI WA TANU, ALLY SYKES KUZIKWA LEO DAR, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na baadhi ya wazee waliohudhuria shughuli za msiba, wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

*REDD'S MISS KIGAMBONI WAJIFUA KUJIANDAA KUWANI TAJI JUNI 7 UKUMBI WA NAVY BEACH.


 Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 wakiwa kwenye mazoezi yao ya pamoja kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho kitakachotarajia kufanyika Ijumaa Juni 7 mwaka huu kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni Kigamboni.
Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 wakiwa kwenye mazoezi yao ya pamoja kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho kitakachotarajia kufanyika Ijumaa Juni 7 mwaka huu kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni Kigamboni.

*NGASA ALEJEA' NYUMBANI' YANGA ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI,ATAMBULISHWA RASMI LEO


 KATIBU Mkuu wa Mabingwa wa Soka  Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Lawrence Mwalusako, leo amemtambulisha rasmi Mshambuliaji mwenye mapenzi ya moyoni na timu hiyo  Mrisho Ngassa, aliyekuwa na mahasimu wao wakuu, Simba.

Mwalusako, amemtambulisha Ngassa kuwa hivi sasa ni mchezaji mpya na halali wa Yanga, baada ya kuanguka saini ya kuitumikia Klabu hiyo kwa miaka miwili, ili kuisaidia katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara na michuano ya kimataifa, inayoikabili timu hiyo baada ya kuwa mabingwa na Ligi Kuu iliyomalizika jana.



Ngassa, ameamua kurudi Yanga baada ya kuihama timu hiyo na kutimkia, Azam FC na baade kabla ya mwaka jana kuuzwa kwa mkopo, Simba, ambako amekuwa akisumbuliwa kila mara na viongozi hadi mashabiki kuwa hana mapenzi na timu hiyo na hasa kwa kitendo chake cha kubusu Jezi ya Yanga aliyorushiwa na mmoja wa mashabiki wa Yanga, katika moja ya mechi za mwaka jana wakati akiwa Azam.


Aidha Mwalusako, alisema kuwa Ngassa,  ni mchezaji wa kwanza kutangazwa na klabu hiyo na kusani mkataba wa miaka miwili ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu, ambapo ni leo ni siku muhimu iliyokuwa ikisubiriwa na Viongozi wa Yanga, Ngassa na hata mashabiki wa Yanga, waliokuwa wakiushauri uongozi kumrejesha Ngassa ''Tunduni''.  na tayari ameshaanguka saini ya kuichezea klabu yake hiyo ambayo anamapenzi nayo makubwa hapa nchini kwa miaka 2.

Ngassa, akibusu Jezi ya Yanga, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Yanga,  Lawrance Mwalusako, wakati wa utambulisho rasmi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

*HOTUBA YA 'MR. SUGU' YAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA LEO YAPIGWA 'STOP'




Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyokuwa ikisomwa na Msemaji (Waziri Kivuli wa Wizara hiyo) ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Bungeni imesimamishwa kwa kile kilechoelezwa kukiuka taratibu za Bunge.

Akisimama kuomba Muongozo wa Spika, Mbunge wa CCM jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey Weston Zambi, aliliambia Bunge kuwa Hotuba hiyo katika kurasa zake 12 za awali imejaa maneno ya uchochezi kwa Serikali ya CCM.


Zambi alisema miongoni mwa maneno hayo ya Uchochezi ni yale ya kusema kuwa Serikali ya CCM kuwashambulia wanahabari kwa kuwapiga, kuwang’oa kucha, kuwamwagia tindi kali na kuwaua jambo ambalo sio kweli.

Kufuatia hatua hiyo Spika wa Bunge Anne Makinda alipokea Mwongozo huo na kuliahirisha Bunge hadi Hotuba hiyo itakapo pitiwa upya ndipo iletwe tena Bunge hapo.

Saturday, May 18, 2013

ALIEMEREMETA NA UKURASA HUU.

Ni Bi Harusi wetu Rahma akiwa na mpambe wake siku ya kitchen party yake iliyofanyika tarehe  03/05/2013 katika ukumbi wa chonya inn Ubungo River side-Dar es salaam,Picha na Nasma Mafoto.

YANGA YAMNYONYOA MNYAMA KWEUPEEEEEE, 2-0 TAIFA


 Kipa wa Simba, Juma Kaseja, akitaabika chini baada ya kushindwa kuuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Didier Kavumbagu, katika dakika ya 5 na kuandika bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza. Simba nao walipata penati dakika chache baadaye baada ya Canavaro kumuangusha Ngassa katika eneo la hatari na petati ikapigwa na Mussa Mude aliyempelekea kipa katika engo ya kushoto kwake na kuokolewa na kipa huyo.  Kipindi cha pili Hamis Kiiza aliifungia Yanga bao la pili kwa kuunganisha mpira uliorushwa na Mbuyu Twite. Hadi kipute hicho kinamalizika Yanga 2, Simba 0.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akichuana na beki wa Simba, Shomari Kapombe, na mpira huo ulitoka na kuwa kona iliyozaa bao. Sasa mpira ni kipindi cha pili, kaa na ukurasa huu utakaokuletea full matukio ya mechi hii ya Watani wa jadi.

Tuesday, May 14, 2013

UNESCO yaendesha warsha ya siku moja kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini

Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho (katikati) akizungumza wakati kufungua warsha siku moja ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini ambapo warsha hiyo imeshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo AMREF, UNICEF, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoka Tanzania Bara na Visiwani, TGNP, Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na nyinginezo. Kushoto ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO na kulia ni Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo.
Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo akitoa mwongozo kwa washiriki wa warsha hiyo ambapo katika majumuisho yalioamuliwa kwenye warsha iliyofanyika leo ya kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini yatawasilishwa katika mkutano wa Mawaziri utakaohusisha nchi 21 za Afrika Mashariki na Kusini.
Picha juu na chini ni National Program Officer – HIV & Sexuality Education Mathias Herman kutoka UNESCO akichambua mpango wa majukumu ya nchi za Afrika Mashariki na Kusini na kutoa ufafanuzi wa matokeo ya utafiti wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini ambapo ameongeza kuwa nchi inatakiwa kujipanga kwa kusaidiwa na UNESCO pamoja na washirika kuongoza jitihada za kitaifa ambazo zitawawezesha washirika wakubwa ambao ni vijana kushiriki katika mikakati ya kitaifa itakayowasidia vijana nchini kujua mtazamo wao.
Pichani ni Washirki wakifuatilia uchambuzi wa Ripoti uliokuwa ukiwasilishwa na Mathais Herman kutoka UNESCO.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Ufundi stadi Bw. Raymond Benedict (kushoto) akikata kujua kuhusu mapitio ya Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini, huduma zinazotolewa na serikali na nini hatma na vijana wameelewa kwa kiwango gani.
Pichani juu na chini washiriki wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO nchini wakichangia maoni yao.Pichani juu Katikati ni Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Lwidiko Edward akiwakilisha vijana na kulia ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO
Picha juu na chini ni Washirki wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha ya siku moja ya ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho.