Sunday, March 30, 2014

WINDHOEK AMBAO NI WADHAMINI WAKUU WA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 3 YA BONGO MOVIE WAFANYA KWELI KATIKA UKUMBI WA EAST 24 MWISHONI MWA WIKI


 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Mengele (Nyerere) akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa sherehe ya Kutimiza miaka 3 ya Klabu ya Bongo Movie, sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Katika Jengo la Arcade Mikocheni, Mwishoni mwa Wiki
Warembo wakiwa wamebeba Chupa za Windhoek zinazosambazwa na kuuzwa na Kampuni ya Mabibo Beer ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa Sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya Klabu ya Bongo inayoongozwa na Steve Nyerere.
Mwenyekiti wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies, Bw Johnson Lukaza akipokea cheti cha kuthaminiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu nchini  iitwayo Proin Promotions Limited.
 Burudani pia zilikuwepo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa East 24 uliopo Mikocheni katika jengo la Arcade.
 First lady wa B Band inayoongozwa na Baba Zoro
 Wadau wakifuatilia burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali waliopanda kwenye jukwaa
 Warembo wa Bongo Movie wakiingia ukumbi tayari kwa Kufurahia Miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Nuruel akiendelea kuimba kwa hisia katika sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki
 Mwenyekiti wa Bongo Movie akitoa maneno kwa wageni waalikwa pamoja na wasanii wa bongo movie na muziki nchini waliohudhuria sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa East 24.
 Keki ikikatwa kama ishara ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bongo Movie ikiwa imetimiza miaka 3
 Rich Rich akilishwa keki na Mwenyekiti
 Mwenyekiti wa Makampuni yaliyochini ya Proin Group of Companies, Bw Johnson Lukaza akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Bi Mwenda akifurahi kukabidhiwa cheti cha sifa ya kuwa msanii mkongwe
 Mtitu akipokea Cheti kutoka Kwa Mwenyekiti.
 Hawa ndio mabalozi wa Windhoek waliochaguliwa katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 ya bongo movie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila ambae alikuwa mdhamini mkuu wa sherehe hiyo kupitia kampuni ya Mabibo Beer akitoa maneno mawili matatu mara baada ya mabalozi wa Bia ya Windhoek kuchaguliwa
 Amin Akishusha Burudani 
 Linex akiimba kwa hisia

HEIFER INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUENDELEZA SEKTA YA MAZIWA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.
 Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam
 Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer International Tanzania umedhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda Foundation
Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akifungua Pazia kuashiria Mradi huo wa Kuendeleza sekta ya maziwa umezinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo jijini Dar Es Salaam.
 Mjasiliamali wa Maziwa kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana akitoa Ushuhuda wake kwa wageni waalikwa kuhusu mafanikio aliyoyapata akiwa kama mdau wa sekta ya maziwa.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo ambae pia ni Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akimpongeza Mjasiliamali wa Waziwa kutoka Mkoani Iringa, Bi Diana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kuendeleza Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini.


 Baadhi ya Wageni waalikwa na Wadau kutoka Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki wakifuatilia mada kwa makini wakati wa UZinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki
 Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambae pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Heifer International Tanzania na EADD pamoja na wadau wa Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mh Kaika Telele ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya Kilolo mara baada ya kumalizika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa Wiki.

*TAMASHA LA MUZIKI KUHUSU MUUNGANO LAFANA


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifungua Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi katika Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akitoa hotuba fupi wakati wa tamasha hilo, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel.
 Mshereheshaji kutoka kikundi cha Temeke akionyesha umahiri wake kwa  kula moto wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi lililofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 Kundi la muziki wa dansi lijulikanalo kwa jina la Mashujaa wakitumbuiza wakati wa Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi,Taharabu, Kizazi Kipya na Utenzi siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa makundi ya muziki wa Dansi,Taarabu,Kizazi kipya na Utenzi walioshiriki Tamasha la Muungano la Fainali la Muziki wa Dansi, Taarabu, Kizazi Kipya na Utenzi wakiwa katika picha ya pamoja ambapo katika muziki wa dansi kundi la Msondo ngoma liliibuka kidedea huku upande wa taarabu Jahazi Modern Taarabu walishika nafasi ya kwanza huku muziki wa kizazi kipya msanii Kelvin Nyoni kawabwaga wenzake na katika fani ya Utenzi Bi. Mariam Mponda kashika nafasi ya kwanza.Picha na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

MHESHIMIWA RAIS AMEWASILI LONDON KWA ZIARA YA KISERIKALI


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Ruthanne Chipeta mara baada ya kuwasili jijini London leo Machi 30, 2014 kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Serikali ya Uingereza


Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Tobiko Kallaghe mara baada ya kuwasili jijini London leo Machi 30, 2014 kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Serikali ya Uingereza
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipokewa mara baada ya kuwasili jijini London leo Machi 30, 2014 kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Serikali ya Uingereza
                                                            Picha kutoka kwa Michuzi

MABONDIA JUMA FUNDI NA BAINA MAZOLA WASAINI KUPAMBANA MEI 11

Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana misuli na Baina Mazola baada ya kusaini mkataba wa kupigana Mei 11 katika ukumbi wa DID HALL Mabibo Mwisho 
Promota wa mchezo huo wa masumbwi Mahiyo Mkumbi kulia akiwaonesha mkataba mabondia pamoja na viongozi wa masumbwi kabla ya kutia saini mkataba huo kwa ajili ya mpambano wa mei 11

Bondia Juma Fundi akitia saini mkataba wa kupambana na Baina Mazola mei 11 katika ukumbi wa DID Mabibo mwisho

Promota wa mchezo wa masumbwi Mahiyo Mkumbi katikati akiwainua juu mabondia kutambulisha mpambano wao utakaofanyika mei 11 mabibo mwisho

WANAFUNZI WA UDOM MWAKA WA MWISHO, WAMEAHIDI KUJIUNGA NA PPF


Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo kwenye semina iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo zaidi ya wanafunzi 500 walihudhuria semina hiyo Jumamosi Machi 29, 2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wakifuatilia mada kutoka kwa Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele

Saturday, March 29, 2014

*SHOMARI KAPOMBE BADO NJIA PANDA KUTUA YANGA AU AZAM, SIMBA, MMMH!!!!!! WATASUBIRI SANA



Jangwani au Chamazi? Shomary Kapombe anataka kucheza timu ambayo itashiriki michuano ya Afrika mwakani.
***********************************************************

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SHOMARY Kapombe ameamua kurejea nyumbani Tanzania kutoka Ufaransa, lakini anataka kucheza klabu ambayo itashiriki michuano ya Afrika mwakani- maana yake, uwezekano wa kurejea Simba SC sasa unakuwa mdogo.
Kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, anamaliza Mkataba wake Simba SC mwezi ujao, lakini alikwishaingia Mkataba wa miaka minne na AS Cannes ya Ufaransa mwaka jana.

Na Simba SC imekubaliana na klabu ya Daraja la Nne Ufaransa, kuununua Mkataba wa mchezaji huyo arejee kufanya kazi Msimbazi baada ya kushindwa kuendelea kucheza Ulaya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alizungumza na AS Cannes mwezi uliopita na kufikia makubaliano ya kuuziana Mkataba huo, ili Kapombe arejee Msikmbazi.

Poppe alisema kwamba Simba SC imekubali kuilipa Cannes kiasi cha Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.

Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu.

Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.  

Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua kubaki moja kwa moja nyumbani akidai halipwi mishahara.
Kapombe mwenyewe amekuwa mgumu kuzungumzia suala hilo, lakini tayari kuna habari kwamba Yanga SC na Azam zinamtaka pia mchezaji huyo.

Yanga SC na Azam FC ndizo zipo kwenye nafasi ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, hadi sasa zikiwa zinakimbizana kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Azam FC ipo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 50 ilizovuna katika mechi 22, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 46, lakini wana mchezo mmoja mkononi. 

Wakati Yanga SC imebakiza mechi tano na Azam FC nne, mchuano wa kuwania ubingwa unaonekana kuwa mkali zaidi baina ya timu hizo mbili na mechi za Jumapili zinatarajiwa kutoa picha zaidi ya mbio zao.

Azam FC ikiwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Simba SC, wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Yanga SC watahamia Mkwakwani, Tanga kuwakabili Mgambo JKT

*CHEKI VIDEO MPYA YA WAKONGWE, PROF, JAY, J. NATURE NA JAY MOE, WAMETISHA NA GWANDA ZA KIJEDA



Na Dina Ismail, Dar es Salaam
WASANII watatu wakongwe na maarufu wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Juma Kassim ‘Nature’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’ wamerekodi kwa pamoja wimbo mpya uitwao JWTZ ikiwa ni pamoja na video yake hii.
Sauti ya wimbo huo na Video umerekodiwa katika studio za Williamz Visions chini ya mtayarishaji Mike Mwakatundu ‘Mike T’. 
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, mtayarishaji huyo, Mike T, maarufu kama Mnyalu, amesema kuwa, yeye anakuwa muongozaji wa kwanza wa video au filamu Tanzania kupata fursa ya kutumia vifaru, ndege, helikopta na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika kazi zake.

“Naamini kwa kumtanguliza Mungu kila kitu kinawezekana, baada ya yote, naamini magwiji hao wamefunika katika video  hii na wamefanya kweli,”amesema Mike T, ambaye pia ni gwiji wa Bongo Fleva.

*WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KUANDAA KONGAMANO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50 tangu kuzaliwa kwake. 

Kongamano hili la Vijana kuhusu Muungano linafanyika Jumapili Machi 30, 2014  kuanzia Saa  5:00 Asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na litarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC Taifa.

Kongamano hili ni sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.

Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.


Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi  ujao unafikisha miaka 50.Washiriki wa Kongamano hili  ni vijana  300 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.

Washiriki wa Kongamano hili watapata fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha mada kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu Mapendekezo ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.

Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini wanakaribishwa kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu kongamano hili.

Imetolewa na Idara ya Habari -  MAELEZO
29 Machi 2014

*WANANCHI WA MJI WA KOROGWE WAUPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA TIKA, WACHANGIA MIL. 1.3



Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa uzoefu wake katika moja ya Wilaya ya Ilamba, Singida jinsi wananchi wanavyofaidika na TIKA.
Viongozi wa Dini wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Mkuu Manundu, Korogwe Mzee Daffa Daffa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimia na viongozi wa dini wa Halmashauri ya Mji Korogwe mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Waheshimiwa Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmshauri ya Mji Korogwe wakiwa katika mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
NHIF 11: Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- Dar es Salaam, Genoveva Vicent akitoa majumuisho jinsi Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) unavyoweza kuwasaidia wananchi.

Mchungaji Joseph Mhina wa Kanisa la Anglikana Manundu, Korogwe akitoa shukrani kwa wananchi waliofika katika mkutano huo wa wadau. 
Timu ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dar es Salaam na Tanga waliokuwa wakiratibu mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa na Wilaya. Picha zote na Cathbert Kajuna
**************************************
MAAZIMIO YA KIKAO CHA WADAU WA TIKA KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE:-
1. Washiriki wote wa kikao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wamekubaliana kwa kauli moja kukatwa Tshs.10,000 za posho zao kama mchango wa TIKA ili kusaidia wazee na wenye mahitaji maalumu.

2. Kila mshiriki awe mwalimu na mhamasishaji kwa wale wote ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kikao hiki cha wadau wa TIKA
3. Mfuko wa TIKA ni mali ya wana Korogwe hivyo kila mwananchi mwenye uwezo na mfanyakazi achangie kiwango cha Tshs.10,000 kama mchango wa TIKA kwa mwaka kwa mtu mmoja.

4. Watendaji wa Mitaa,Kata na halmashauri wawe karibu na wenyeviti wa mitaa katika kuhamasisha jamii kujiunga na TIKA.
5. Kuhamasisha wanakorogwe walio nje ya Korogwe kuchangia Mfuko wa TIKA kwa kiwango kilichowekwa ili kuuboresha mfuko na kusaidiwa wenye mahitaji muhimu na wazee.

6. Wana Korogwe wenye uwezo zaidi kiuchumi waliopo Korogwe waombwe kuchangia mfuko huu ili kuuboresha.
7. Kuhamasisha makundi maalumu kujiunga na TIKA mfano walemavu,na wawakilishi wao waliohudhuria semina hii wakawe mfano kwa kujiunga na TIKA na kuhamasisha wenzao.

8. Watendaji wa Kata na Mitaa/Vijiji waitishe mikutano ya hadhara kwa ajili ya uhamasishaji na washarikiane na washiriki waliopata mafunzo/semina hii.
9. Viongozi wa dini watatumia vikao vya kidini kwa ngazi zote kitaka kuhamasisha jamii na waumini (misikitini na makanisani)

*WASHINDI WA TUZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA WATUNUKIWA NA MH RAIS.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi walionyakua tuzo mbalimbali wakati wa hafla ya kutunuku Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora wa mwaka 2013 iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku. Picha na Freddy Maro