Friday, May 16, 2014

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. AMOS MAKALLA MKOANI GEITA



Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akipokea maelezo ya kisima Wilayani Mbogwe. Tayari Wizara ya Maji imeshatoa shilingi milioni 200 kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu ya maji wilayani hapo kutimiza ahadi ya Waziri wa Maji Prof. Maghembe.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akimuandikia jambo Mbunge wa Mbogwe Mh. Augustino Masele. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akiwaonesha jambo, Mbunge wa Mbogwe, Mkuu wa Mkoa wa Geita, RAS wa Geita kabla ya hutuba yake.
Mbunge wa Mbogwe, Mh. Augostino Masele akiwahutubia wananchi wa Mbogwe namna ambavyo yeye kwakushirikiana na Mbunge wa Msalala Mh. Maige walivyoweza kumleta Naibu Waziri wa Maji ili kutatatua na kuzitafutia suluhisho la kudumu kero za maji katika majimbo yao.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Mbogwe baada ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita.
Mbunge wa Msalala Mh. Ezekiel Maige akimuonesha jambo Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Isaka.
Mbunge wa Msalala Mh. Ezekiel Maige akiwahutubia wananchi wa Isaka Wilayani Kahama juu ya utatuzi wa kero ya maji katika eneo hilo. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akichukua dondoo za hotuba hiyo ili aipatie majibu.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akiwahutubia wananchi wa Isaka, aliyekaa chini ni mbunge wa Msalala, Mh. Ezekiel Maige.

Na Athumani Shariff
Naibu Waziri wa Maji, Mh. Amosi Makalla aliongozana na Wabunge wa Msalala na Mbogwe walilazimika kuacha vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea Bungeni mjini Dodoma ilikwenda kukabiliana na matatizo ya maji katika majimbo ya Msalala na Mbogwe.

Makala alichukua uamuzi huo baada ya kupewa mualiko na Ezekiel Maige Mbunge wa Msalala pamoja na Augostino Masele Mbunge wa Mbogwe pindi walipokuwa katika bunge maalumu la katiba.

Akiwa Wilayani Mbogwe, Mh. Naibu Waziri alipokea taarifa za hali ya wilaya pamoja na kero za maji katika wilaya hiyo na kisha kutembelea miradi ya maji kujionea hali halisi ya maji ilivyo pamoja na kero za maji katika maeneo hayo.

Akitaka kujua kuhusu ahadi ya Mh. Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe aliyoitoa juu ya kuchangia shilingi milioni 200 ikiwa ni ahadi aliyoitoa mbele ya Rais. Masele alimtaka Makala awaeleze wananchi wa Mbogwe hatma ya ahadi ya Waziri wa Maji mbele ya Rais Kikwete kwa wananchi wa Mbogwe.

“Mh. Naibu Waziri wa maji, katika ziara ya Rais aliyoambatana na Waziri wa Maji Prof. Maghembe, Waziri wa Maji aliahidi kutuchangia shilingi milioni 200 ili kutanua mtandao wa maji katika wilaya ya Mbogwe, je wananchi wa Mbogwe wanauliza juu ya utekelezaji wa ahadi hii ya Mh. Waziri.” Aliuliza Masele alipokuwa anahutubia wananchi.

Akijibu swali hilo katika mkutano wa hadhara, Mh. Makala alisema, tayari pesa hizo Waziri ameshazitoa tangu tarehe 6 Mei, na ni mategemeo yangu kuwa zitatumika kwa ufasaha na kwa malengo yaliyokusudiwa. “Mh. Waziri ameshazitoa pesa hizo na zipo kwenye akaunti ya mhandisi wa maji, ni nimatarajio yangu kuwa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa” alijibu Makala.

Katika hatua nyingine Masele alimuomba Naibu Waziri, Wilaya ya Mbogwe ipatiwe maji kupitia mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Viktoria kwani chanzo chake ni chakudumu.

Akiwa Wilayani Kahama katika jimbo la Msalala kata ya Isaka, Naibu Waziri alikumbana na kero kubwa ya maji baada ya kujionea upungufu wa maji kwa zaidi ya asilimia 79. 

Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige alimueleza Naibu Waziri kuwa shida ya maji Isaka ni kubwa na vyanzo vya maji vilivyopo havitoshelezi hata robo ya mahitaji ya wananchi.

Akijibu hoja hizo katika mkutano wa hadhara, Mh. Makalla alisema Isaka ipo katika kipaumbele cha hali ya juu kwani ahadi ya kuleta maji katika eneo hili ni ya Rais. Pia aliongeza kuwa Mradi wa kuleta maji Isaka kupitia maji ya Ziwa Viktoria utaanza mwakani. 

 “Mradi mkubwa wa maji Isaka kutoka ziwa Viktoria utaanza mwaka ujao wa fedha, ahadi ya kuleta maji hapa ni Rais, hivyo hatuwezi kuacha kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais” alisema Makalla.

KINANA AHUTUBIA URAMBO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Urambo kwenye uwanja wa Wananchi na kuwaambia Serikali inatambua kero kubwa ya maji mkoani Tabora na mipango madhubuti ya kuwezesha kupunguza tatizo hilo inaendelea huku huduma ya mradi wa umeme vijijini itapatikana karibuni ikiambatana na Minara ya mawasiliano ya simu,lakini pia Katibu Mkuu aliwataka viongozi wa CCM kurekebisha kasoro zao na kutambua wajibu wao wa kuwatumikia wananchi ikiwa pamoja na kuisimamia serikali katika kutekeleza mipango ya maendeleo iliyoahidiwa kayika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Urambo na kuwaambia kuwa wawe makini na wasanii wa kisiasa ambao wamekosa sera na hoja zinazosaidia mwananchi wa kawaida katika kupambana na changamoto zinazomkabili.
 Mbunge wa Urambo Mashariki Ndugu Samuel Sitta akiwahutubia wakazi wa Urambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Wananchi,Urambo mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi pikipiki Katibu wa kata ya Ukondamoyo Baraka M.Baraka ,Piki piki 16 zimetolewa kwa kata zote 16 za wilaya ya Urambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Samuel Sitta akishirikiana na Mbunge wa Viti maalum Magreth Sitta.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakikabidhi baiskeli 95 kwa Makatibu wa Matawi CCM  ambazo zimetolewa na Mbunge Urambo Mashariki Samuel Sitta akishirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Magreth Sitta.
 Vijana 90 wa CCM wilaya ya Urambo wakionyesha mshikamano wakati wakimpa salaam Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Adulrahman Kinana ikiwa pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika kuimarisha chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishiriki kiapo wakati wa kuwaapisha wanachama wapya wa CCM wilaya ya Urambo ambapo watu 900 walijiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kimila wa urambobaada ya kusimikwa rasmi kuwa Mzee wa kimila.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha Ugobogobo,wengine pichani ni Mbunge wa Urambo Mashariki Ndugu Samuel Sitta,Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Urambo Martha Faustine Susu,Mbunge wa Viti Maalum Magreth Sitta na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na kikundi cha Furaha ,wengine pichani ni Mbunge wa Urambo Masahariki Samuel Sitta,Mbunge wa Viti Maalum Magreth Sitta na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa.

TFF YAOMBOLEZA VIFO VYA WASHABIKI DR CONGO



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- FECOFA, Omar Constant kutokana na vifo vya washabiki.

Washabiki 12 walipoteza maisha uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo kati ya TP Mazembe na AS Vita iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael, jijini Kinshasa.

“Tumeguswa na msiba huo mzito, tunatoa salamu za rambirambi kwako (Rais wa FECOFA), familia za marehemu pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,” imesema sehemu ya barua hiyo ya Rais Malinzi

TUPO TAYARI KUIKABILI ZIMBABWE- NOOIJ,MDAU AAHIDI WACHEZAJI MIL 5/-


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 16, 2014

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya mechi ya Kombe la Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Mei 16 mwaka huu), Nooij amesema kabla ya kuja Tanzania alikuwa akifuatilia Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), hivyo anawafahamu wachezaji wengi.

Amesema wachezaji wanaounda kikosi chake ni wenye uzoefu na mechi za kimataifa, hivyo wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani wamepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyokuwa Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.

Nooij amesema ujio wa washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) kutaongeza morali ya kikosi chake.

Samata na Ulimwengu watawasili nchini Jumamosi mchana, saa 7.30 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo leo (Mei 16 mwaka huu) wanacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Hilal ya huko.

Wachezaji waliopo kambini kwa sasa ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Said Moradi, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Himid Mao, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Khamis Mcha, Ramadhan Singano, John Bocco, Elias maguli na Kelvin Friday.

Wakati huo huo, timu ya Zimbabwe (Mighty Warriors) inawasili kesho alfajiri (Mei 17 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 27. Kesho saa 4 asubuhi (Mei 17 mwaka huu) Kocha wa timu hiyo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zinaanza kuuzwa kesho (Mei 17 mwaka huu) kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, OilCom Ubungo, Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala. Viingilio ni sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 tu.

…MDAU AAHIDI WACHEZAJI MIL 5/-
Mdau mmoja wa mpira wa miguu ambaye hataki jina lake litajwe ameahidi kutoa sh. milioni tano kwa wachezaji wa Taifa Stars iwapo wataifunga Zimbabwe katika mechi ya Jumapili.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamshukuru mdau huyo, na linatoa mwito kwa wadau wengine wajitokeze kutoa motisha kwa Taifa Stars.

Bonasi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa wachezaji wa Taifa Stars itatolewa kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

FILAMU YA JOTI SANDUKU LA BABU KUINGIA SOKONI HIVI KARIBUNI



Msanii Lucas Mhavile ‘Joti’baada ya kukaa kimya kwa mda sasa ameibuka na filamu yake ya Joti Sanduku la Babu ambayo amecheza katika husika tofauti tofauti filamu hiyo itakuwa ikisambazwa na   Kampuni ya proin promotions ya jinini Dar es salaam

akizungumzia filamu hiyo Joti alisema kuwa amekuja kivingini kwani kitu alichofanya katika filamu hiyo aijawai kutokea wala kufanywa na mtu yoyote yule katika tasinia hii ya filamu nchini

 hivyo wapenzi wangu wakae mkao wa kula tu kwani wakati wowote kuanzia sasa itakuwa inaingia sokoni kwani filamu hii si yakukosa mana unambiwa uzee mwisho chalinze mjini kila mtu honey

hivyo wapenzi wa filamu nawaomba wanunue nakala halisi ya filamu hiyo pindi itakapotoka ambapo nimelezea mambo mbalimbali ya ujana usichana pamoja na uzee

 mbali na hivyo filamu hiyo imebeba mambo matatu muhimu kwanza ina burudisha pia ina elimisha na kupata ujumbe muhimu kabisa katika jamii inayotuzunguka'

filamu hiyo ya kwanza tangu joti aweke kando mambo ya filamu na kujingiza katika mambo ya uchekeshaji kupitia luninga sasa ameludi tena katika filamu yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la joti sanduku la babu

CHINA NA TANZANIA ZATILIANA SAINI MKATABA WA WENYE THAMANI YA DOLA LAKI MOJA ZA KIMAREKANI.



 Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah akitoa maelezo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo wakati wa sherehe fupi ya utiaji saini mkataba wathamani ya dola laki moja za kimarekani kati ya Chama cha Kupunguza matumizi ya silaha na Maridhiano cha China na Ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania.
 Baadhi ya viongozi toka pande zote mbili wakiwa katika sherehe ya utiaji saini mkataba wa thamani ya dola laki moja za kimarekani kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi za Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania uliofanyika leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

 Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan wakitia saini mkataba huo wa thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) mara baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) akiwakabidhi zawadi baadhi ya wajumbe alokuja nao mgeni wake.


 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (kushoto) akimkabidhi zawadi Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (kulia) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah (aliyekaa kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan (aliyekaa mstari wa mbele kushoto) mara baada ya utiaji saini mkataba wa makubaliano wenye thamani za fedha za kimarekani dola laki moja leo ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam.

China na Tanzania zatiliana saini mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Na. Benedict Liwenga-MAELEZO.
16/05/2014
OFISI ndogo ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania leo imetialiana saini na Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani.
Utaiji saini huo umefanyika leo katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukihusisha viongozi wa pande zote mbili akiwemo Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha kupunguza Matumizi ya Silaha na Maridhiano cha Jamhuri ya Watu wa China (Chinese Peoples’ Association for Peace and Disarmament) Bi. Chen Huaifan.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Thomas Kashililah amesema kuwa mkataba huo wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani utasaidia ofisi ya Bunge kuweza kupata vifaa mbalimbali vya ofisi vikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu, vipaza sauti, kamera pamoja na vifaa vya kurekodia.
“Ndugu zetu kutoka China pamoja na hiki Chama chao wamesaini pamoja nasi mkataba wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ambao wametutaka sisi tuamue wenyewe ni vifaa gani tunahitaji kwaajili ya ofisi yetu ya Bunge mjini Dodoma ili wao waweze kutununulia na kutukabidhi”. Alisema Kashililah.
China na Tanzania zimekuwa zikitiliana saini mikataba mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa namna moja mikataba hiyo imekuwa ikizinufaisha pande zote mbili kiuchumi na mpaka hivi sasa uhusiano huu umedumu kwa muda miaka hamsini.