Saturday, July 6, 2013

* MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM LEO


 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipozungumza nao leo.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika ukumbini hapo kuzungumza nao leo.
Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao.

*WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAFURIKA KUSHUHUDIA TAMASHA LA FILAMU LA GRAND MALT


Wananchi waliofurika katika Tamasha la Filamu la Grand Malt linalofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
********************************
 
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWANZO MWISHO! Leo ni leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, wakati kutakapofungwa rasmi Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima.

Huku wasanii wote mashuhuri wa filamu wakitarajiwa pia kufanya vitu vyao jukwaani, kazi kubwa itakuwa kwa burudani kali zitakazotolewa wakati wa kufunga tamasha hilo.


Mbali na hilo, pia kutakuwa na shindano kali hatua ya fainali ya kusaka wakali wa kurap pamoja na kukata nyonga, ambao nao watajiondokea na kitita kikubwa cha fedha.

Akizungumzia hilo, Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema kutakuwa na mambo makubwa zaidi uwanjani hapo na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kile kitakachoendelea.


 “Kila kitu kipo tayari na wasanii wote wakali wa filamu watakuwepo ili kutoa burudani kwa mashabiki waliofika hapa, huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa,” alisema.

Baadhi ya wasanii wa filamu wanaotarajiwa kuwepo ni Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’, Shamsa Ford, Ritchie Ritchie, Steven Jacob ‘JB’, Chuchu Hans, Steve Nyerere, Hashim Kambi na wengineo wengi.

 Akizungumzia hilo, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona tamasha hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akitaka mashabiki kufurika Nyamagana leo kuona kile kinachoendelea.

“Hapa Mwanza tumeshuhudia vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kuona mashabiki walivyolipokea tamasha hili, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Katika mashindano ya kurap na kucheza katika kila eneo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na Sh 200,000 wa pili Sh 100,000 na watatu Sh 50,000.

Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika leo, huku wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.

Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

*MLINZI WA MAKAO MAKUU YA CUF MUHARAMI ABDALLAH SHAABAN TANGANYIKA AMEZIKWA LEO


 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfankazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail
 Sehemu ya waombolezaji
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji wengine.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea.

*WAMASAI KUTOKA MKOANI ARUSHA WATEMBELEA BANDA LA AICC LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM.


.Katibu Mhitasi wa Arusha Intarnational Confrerence Centre. Joyce Mollel (kushoto) akiwaonyesha baadhi ya akinamama wa kikundi cha Masai cha Munduli Arusha shughuli wanazotoa, wakati akimama hao walipotembelea katika banda lao lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

Wednesday, July 3, 2013

*NBC BANK & AFRICAN FIRST LADIES SUMMIT AFRICA, MKURUGENZI WA NBC ATOA SOMO


 Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa  Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD),  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.
 Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.  
Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa  Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo. 

*JUMLA YA SH.MILIONI 3, 250,000 REDD'S MISS TEMEKE 2013 KUJINYAKULIA ZAWADI ZA


Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo sambamba na wasanii watakaotumbuiza siku hiyo Ben Paul na Luiza Mbutu wa bendi ya Twanga pepeta ambapo shindano hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili kushoto ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tz Albert Makoye.

Luiza Mbutu, akizungumza wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.
*****************************************
MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika keshokutwa siku ya Ijumaa Julai 5, mwaka huu, ataondoka na zawadi nono zenye jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo, yaliyofanyika mwaka huu.
Mshindi huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni 3,250,000.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha Sh.800,000 pesa taslim na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.
Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa mafanikio makubwa.
Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super Bokilo na Charles.
Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa,  Hyness Oscar, Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo .                                                                 
Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym & Spa, 100.5 Times FM na Kitwe General Traders. Mbali ya wadhamini hao pia Redds Miss Temeke imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu na mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu hasa kwa upande wa zawadi.
Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
BMP Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka wa 18 sasa, inatanguliza shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kuandaa Miss Temeke kwa ufanisi katika muda wote huo, shukrani sana.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions

*RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MABANDA YA BIASHARA SABASABA


 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa n Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Makazi(UNHABITANT) Phillemon Mutashubirwa  kuhusu wanavyofanya kazi ya kusaidia watoto wa shule na wanawake kwenyeMaonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu  J. K Nyerere jijini  Dares Salaam.
Picha zote na Magreth Kinabo –Maelezo.

MSIKILIZE LULU ALICHOSEMA NDANI YA TAKE ONE


Kwa mara ya kwanza tangu msanii Elizabet Michael (Lulu) kutoka gerezani ameongea mengi katika kipindi cha Take One cha Clauds TV kinachoongozwa na mwanadada Zamaradi Mketema

Tuesday, July 2, 2013

CHEKI MAGOLI YA MOROCCO VS TANZANIA

PATA TRAILER YA MAPISHI

*RAIS OBAMA NA UJUMBE WAKE WAMEONDOKA LEO


 Rais wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle, wakipanda ndege yao aina ya Air Force One, tayari kuondoka nchini kurejea nchini kwao baada ya kumaliza rasmi ziara yao katika Bara la Afrika, ambapo amemalizia ziara hiyo kwa kufanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania. Obama na msafala wake ameondoka leo mchana.
 Rais Obama na mkewe, wakipunga mikono kuwaaga wenyeji wao Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Viongozi wa Kiserikali na wananchi waliofika uwanjani hapo kuwaaga leo, mchana wakati wakiondoka nchini.
 Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakipunga mikono kuwaga wageni wao Rais Obama na mkewe wakati wakiondoka nchini leo mcahana baada ya kumaliza ziara yao.
 Rais Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.

*OBAMA MTAALAM WA SOKA PIA,AFANYA VITU ADIMU DAR KABLA YA KUPAA LEO


 Rais wa Marekani, Barack Obama, akipiga danadana za kichwa wakati alipowasili kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya Ubungo jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya kuizindua rasmi mitambo hiyo ikiwa ni sehemu ya kumalizia ziara yake ya siku mbili kabla ya kuondoka nchini leo.

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA MKUTANO WA SIKU 3 WA VIONGOZI WA KIMATAIFA WA KUTOKOMEZA NJAA BARANI AFRIKA, ADDIS ABABA-ETHIOPIA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammmed Gharib Bilal, akifunga  Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa  Kimataifa  wenye  lengo la  kutokomeza  njaa Barani Afrika .Mkutano huo ulimazika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye  Mkutano wa Kimataifa   kuzungumzi  juu ya   kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika uliomalizika  mjini Addis Ababa Ethiopia.
 Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakifuatilia kwa makini mkutano wa Afrika uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika  jana  jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi wa kimataifa waliohudhuria Mkutano wa  Kimataifa  uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa  Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa  AUC  Dk.  Nkosazana  Dlamina Zuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa umoja huo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika  mjini Addis Ababa Ethiopia jana jioni. Picha na OMR

Monday, July 1, 2013

*MASANJA, SHILOLE WAFIKA UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI


 Juu na chini ni Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakiwa nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC mara walipopita na kupiga picha nje ya mjengo Jumapili June 30, 2013 walipokua wakitokea uwanja wandege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Kesho mchana Jumanne April 2, 2013 watatembelea rasmi mjengo huo na kusaini kitabu cha wageni.
 Masanja na Shilole wakiwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wakiangalia menyu tayari kwa kuagiza dinner ya mchana walipokwenda mgahawa wa kijiji cha Swahili uliopo Beltsville, Maryland
 Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na mmiliki wa mgahawa wa Swahili Village Bwn.Kelvin.
Masanja na Shilole wakiingia kwenye usafiri wao kuelekea Hotelini walikofikia

*OBAMA ATUA BONGO, APOKELEWA KWA MUZIKI NA MATARUMBETA ASEBENEKA KWEUPEEEEEE


Rais Jakaya Kikwete, akiwa na mgeni wake, Rais wa Marekani, Barack Obama, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo mchana huku kwa pamoja wakifurahia na kucheza ala za muziki wa Matarumbeta uwanjani hapo. 
Baada ya kuwasili Uwanjani hapo Obama, alikagua Gwaride maalum na kusalimiana na wananchi waliokusanyika uwanjani hapo kwa kuwapungia mikono, ambapo aliwaacha hoi wananchi hao pale alipofika mbele ya wasanii wa muzuki wa matarumbeta na kuanza kusebenekwa kwa kucheza muziki huo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu. 
Baada ya hapo Obama na msafara wake walielekea Ikulu ambapo pia alikuwa na kikao cha faragha na mwenyeji wake na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari, walioruhusiwa kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Rais Barack Obama na Familia yake wakishuka kutoka ndege ya Airforce One muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.
 Rais Barack Obama na Familia yake wakishuka kutoka ndege ya Airforce One muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.
 Hawa ni baadhi ya wananchi waliojitokeza pande za Barabara mpya ya Obama, geti kubwa la Ikulu kwa ajili ya kumlaki Rais Obama.
 Wakimsubiri Obama.....
 Hawa pia ni baadhi tu ya wananchi walikuwa katika njia za makutano ya Barabara aliyopita Obama, wakisubiri kumlaki.
 Njia zote zilizo katika makutano na barabara aliyopita Obama zilifungwa kwa muda kama hivi. PICHA NA KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Friday, June 28, 2013

*WAWILI WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE


Wachezaji wawili kutoka Tanzania ni miongoni mwa wachezaji 50, waliochaguliwa baada ya kufanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichopo Doha nchini Qatar, kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Wachezaji hao ni pamoja na Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.

Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal

Thursday, June 27, 2013

*FAMILIA YA MANDERA YAZUA UTATA KUHUSU NI WAPI ATAZIKIWA


Na. Halima Kambi, Dar
Bado Bara la Afrika likiwa katika wingu nzito juu ya Afya ya baba wa Afrika Kusini Nelson Mandela familia yake nayo imeingia katika utata mkubwa juu ya mahali atakapozikwa Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini pindi atakapokufa.

Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni baada ya mjukuu wake, Chifu Mandla Mandela kususia kikao cha familia na kutoka nje ya kikao hicho baada ya kukasirishwa na mjadala wa kufufua miili ya  watoto  watatu  wa mandele .

Kutokana na familia inataka miili ya watoto  hao Thembekile, Makgatho na Makaziwe yaamishiwe Qunu ambako Mandela atazikwa.

Vyanzo vya habari tofauti nchini humo vilisema familia hiyo ilitofautiana na Mandla ambaye anataka babu yake azikwe mahali akozaliwa Mvezo huko wengine wakitaka wosia wwake wakuzikwa karibu na wanawe uheshimiwe
Pia familia ya mzee Nelson Mandela imeanza kusafisha makaburi pamoja na kupanda maua maeneo yanayozunguka viunga hivyo ikiwa ni ishara ya kujiandaa kwa lolote litakalotokea hivi karibuni..

Familia hiyo imefanya maamuzi hayo baada ya hali ya kiongozi huyo kuendelea kutokutia matumaini tangu kupelekwa kwake hospitali kwa ajili ya matibabu

Nelson Mandela ndiye kiongozi pekee wa Afrika aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupinga na kupambana na ubaguzi wa rangi dhidi ya makaburu nchini Afrika ya Kusini..

Hata hivyo maradhi yanayomsumbua kiongozi huyo hivi sasa  ni pamoja na kuathirika kwa mapafu maradhia ambayo yalianza kummaliza toka alipokuwa gerezani

Mbali na utata katika familia pia katika nyumba ya Mzee Mandela Houghton 12th Ave, waandishi wa habari kutoka nchini Marekani wameweka kambi nje ya nyumba hiyo, pia  Rais Zuma ameahirisha safari ya kwenda Mozambique.

Bado maswali mengi yapo kwa wananchi ndani ya Afrika ya Kusini na nje ya juu ya hali yam zee huyo kwani tayari wananchi wanahisi mzee Mandela ameshafariki Dunia lakini madaktari na familia inawaficha katika jambo hilo.

TUZIDI KUMUOMBEA MZEE MANDELA ILI AWEZE KUPONA MARADHI YANAYOMSUMBUA KWANI BADO AFRIKA INAMUHITAJI SANA