Tuesday, March 25, 2014

*HABARI KUTOKA TFF LEO, KORTI YAAGIZA TFF IKAMATE MIL 106/- KULIPA WACHEZAJI YANGA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tumepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.

Tayari tumeanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.

Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.

Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.

Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo.

*AZAM, YANGA VIWANJANI DAR, TANGA VPL
Timu za Azam na Yanga ambazo zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania pointi tatu.

Azam yenye pointi 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 19.

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina pointi 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).

*KAMATI YA SHERIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa agizo la wanachama kurekebisha katiba zao.

TFF tulitoa agizo kwa wanachama wetu kufanyia marekebisho katiba ikiwemo kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa Machi 20 mwaka huu.

Hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa hatua inayofuata.

*TIMU YA WATOTO WA MITAANI YAENDA BRAZIL
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo (Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani.

John Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania.

Michuano hiyo ya siku 10 inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana) inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.

Mwaka 2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.

*MABINGWA WA MIKOA WATAKIWA MACHI 30
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwa vinatakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu.

Majina ya mabingwa yanatakiwa kuwasilishwa pamoja na usajili wa wachezaji waliotumika kwenye ligi ya mkoa. Kila klabu inaruhusiwa kuongeza wachezaji watano kutoka ndani ya mkoa husika, ambapo unatakiwa uthibitisho wa usajili huo.


Mpaka sasa ni vyama viwili tu ndivyo vimeshawasilisha mabingwa wao. Vyama hivyo ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) ambapo bingwa wake ni Kiluvya United, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi (LIREFA) ambapo bingwa ni Kariakoo SC

*KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA LEO


 Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum wote 12  pamoja na mambo mengine inajukumu la kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mhe. Sitta akiendelea kuongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi
 Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Uongozi Mhe. Anna Abdalah akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe...Picha na Owen Mwandumbya

*RAIS KIKWETE AZINDUA UKARABATI WA BARABARA YA KOROGWE HADI MKUMBARA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wapili kushoto),Wziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli(kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Burundi na Uganda Bwana Philippe Dongier(watatu kushoto),Mwakilkishi wa Kampuni ya ujenzi ya Strabag Bwana Philip Raiver(wanne kushoto) na mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale(kulia) wakiata utepe kuzindua rasmi uakarabati wa Barabara ya Korogwe-Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76 jana mjini Korogwe.Ukarabati huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati), Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(kushoto), pamoja na Mwakiklishi wa Benki ya Dunia Bwana Philippe Dongier wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ukarabati wa barabara ya Korogwe hadi Mkumbara kwa ufadhili ya Benki ya dunia.Uzinduzi huo ulifanyika mjini Korogwe jana .Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Lutemi Mstaafu Chiku Galawa.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiandaa kuapanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa Barabara ya Korogwe hadi Mkumbara jana mjini Korogwe huku mwakilkishi wa Benki ya Dunia inayofadhili mradi huo Bwana Phillippe Dongier akiangalia. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kata ya nchi za Tanzania, Burundi na Uganda Bwana Philippe Dongier (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa Barabara ya Korogwe Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76 uliofanyika jana mjini Korogwe.Kulia ni Waziri wa ujenzi Mh. John Pombe Magufuli. Picha na Freddy Maro.

*RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MKATA HANDENI KOROGWE

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wengine wa wilaya ya Handeni na Mkoa wa Tanga wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua rasmi barabara ya kilometa 119 ya Mkata Handeni Korogwe jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kufungua rasmi barabara ya Mkata Handeni Korogwe jana jioni.Pembeni ya Rais kulia ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli. 

*KASEBA NA MASHALI NANI ZAIDI WA MANZESE V/S MWANANYAMALA

MARASTA WAKUTANISHWA, Japhet Kaseba (kushoto) akipozi na Thomas Mashali, wakati wa utambulisho wa pambano lao la jumamosi.
****************************************************
Hivi karibuni watakutanishwa miamba miwili ulingoni wote wakiwa na nywele zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasta, Miamba hiyo  ambayo mara nyingi huwa gumzo la watu mitaani hususani wapenda mchezo wa ngumi kwa tabia zao na vibweka vyao , hao si wengine bali ni Japhet kaseba na bondia mtukutu Thomas Mashali, ambao  jumamosi ya terehe 29/3/2014 watapanda ulingoni katika ukumbi  PTA viwanja wa maonesho sabasaba, kuonyeshana kazi.
 Thomas  mashali “simba asiyefugika – kama anavojiita” alizaliwa sept 1989 na kukulia mitaa ya manzese jijini Dare s salaam, akiwa mtoto mtundu, mkorofi, mgomvimgovi  na mpenda michezo kama ilivyo kwa mdogo wake Charles Mashali, ambaye pia  alikuwa  bondia mzuri aliyetokea kuwashinda na  kuwasumbua mabondia wengi kama kina Francis Miyeyusho, alishawahi kuchukua ubingwa wa taifa kabla ya kuachana na mchezo wa ngumi.
Mashali amewahi kuwa kivutio cha wengi  ulingoni na kero kwa wengine uraiani kwa tabia yake ya kuwapigapiga  watu na kuwaonea wasio na hatia na kuendekeza ubabe usio na maana akiwa kama tembo wa mitaa ya manzese kwa tabia yake iliyomfanya kwenda jela  mara kwa mara na kumpotezea dira imara katika masumbwi  na kukaa muda mrefu bila kupigana.
Mwaka 2009 alipotokea jamaa mmoja anayeitwa juma shumbili ambae ni promota wa mapambano madogomadogo ya mchangani lakini kwa wakati huu alikuwa anaandaa zaidi katika ukumbi wa texas hall manzese na kumuandalia pambano Thomas mashali akiwa kama mbabe wa manzese na amadu mwalimu akiwa kama  mbabe wa tandika.
Matokeo Mashali aliibuka mshindi  wa pambano hilo kwa kumpiga amadu mwalimu kwa no kaunti ya raundi ya tatu na hili ndilo pambano lake la kwanza rasmi la kulipwa  lililomuingiza katika rekodi ya mabondia  wa kulipwa nchini.
Sasa, Jumamosi Mashali niuso kwa uso na Japhet Kaseba, nani kuibuka kidedea?????

*BREAKING NEEEEEWZZZ!!!!!! MKUU WA MKOA MARA JOHN TUPA AFARIKI GHAFLA


Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa, John Tupa, Mkuu wa Mkoa wa Mara, (pichani) amefariki ghafla muda mchache uliopita. Kwa mujibu wa mtoa habari ni kuwa marehemu Tupa, alikuwa akitoka katika moja ya kikao cha utendaji mkoani kwake ambapo baada ya kupewa 'Breafing', sasa alikuwa akielekea eneo husika kwa ajili ya kutembelea na kukagua kile alichoeleza katika taarifa hiyo, na wakati akipanda gari ndipo alipoanguka na kupoteza maisha. Mungu ametoa na Mungu ametwa, Mungu ilaze roho ya Marehemu Tupa mahala pema pepon, Amina.

Habari zitawajia kwa kadri zitakavyotufikia

Saturday, March 22, 2014

HOTEL YAWAKA MOTO-DAR


Hotel ya Picolo-Iliyopo kawe imewaka moto leo majira ya mchana,chanzo cha moto huo inasemekana ni shoti ya umeme!

KIM KARDASHIAN,KANYE WEST COVER VOGUE;‘This is such a dream come true’














SHARE THIS URL

 Kim Kardashian and Kanye West are on the cover of the April 2014 issue of Vogue.
ANNIE LEIBOVITZ/VOGUE
Kim Kardashian and Kanye West appear on the April cover of Vogue, which hits newsstands March 31.
Kim Kardashian's Vogue dream has finally come true.
After months and months of speculation, the reality starlet covers the April issue of the high-end fashion magazine in the arms of her husband-to-be, Kanye West.
Kardashian, 33, stuns in a white Lavin gown resembling a wedding dress just ahead of the couple’s upcoming nuptials slated for this May in Paris, France. West dons a Saint Laurent blazer.

 Behind the scenes look at Kim Kardashian and Kanye West's cover shoot for Vogue.
VOGUE.COM
The adorable North West joined her parents for their Vogue cover shoot.
The gorgeous shots were taken by famous photographer Annie Leibovitz.
"This is such a dream come true!!! Thank you @VogueMagazine for this cover! OMGGGGGG!!! I can't even," Kardashian tweeted Friday along with a pic of the magazine.

RAIS JK KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA JUMAPILI YA TAREHE 30 MACHI 2014

Ubalozi wa Tanzania London - Uingereza, unafuraha ya kuwatangazia Watanzania wote waishio Uingereza kuwaMhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakutana na Watanzania siku ya Jumapili tarehe 30 Machi 2014.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Forty Avenue, Wembley Park, London, Middx, HA9 9BE, kuanzia saa 10 jioni (16:00).

Katika Mkutano huo, Mhe.Rais Kikwete atazungumzia maendeleo ya nchi yetu na pia kutumia fursa hiyo kusikia masuala yanayogusa maslahi ya wanadiaspora. 

Mhe. Rais atakuwa nchini Uingereza kuanzia tarehe 30 Machi hadi 2 April 2014 kwenye ziara ya kikazi kwa mwaliko rasmi wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. David Cameron.

Ubalozi unapenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wa maeneo ya Uingereza na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kumkaribisha Rais kwenye Mkutano huu adimu.


Kwa Taarifa zaidi:
Simu: 0207 569 1470
Email: balozi@tanzania-online.gov.uk

Ahsanteni sana- Ubalozi wa Tanzania – London

BOFYA HAPA KUCHEKI "MSAMBINUNGWA" YA TUNDAMAN & ALIKIBA

Wednesday, February 26, 2014

*HABARI KUTOKA TFF LEO

*SYMBION KUSAIDIA PROGRAMU ZA VIJANA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Symbion Power Tanzania Limited zimesaini makubaliano ambapo kampuni hiyo itasaidia kwenye maeneo matatu ya mpira wa miguu wa vijana.

Makubaliano hayo yametiwa saini leo (Februari 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam. Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati upande wa Symbion aliyesaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Peter Gathercoles.

Maeneo ambayo Symbion itasaidia ni ujenzi wa vituo viwili vya kuendeleza vipaji vitakavyojengwa Kidongo Chekundu na Kinondoni mkoani Dar es Salaam, mashindano ya Taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 12 (U12) yatakayofanyika mwaka huu na kuisaidia timu ya U17 ya Tanzania (Serengeti Boys).

Serengeti Boys itacheza na Afrika Kusini, Julai mwaka huu katika mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa wachezaji wa umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Niger.

Hivyo Symbion imetoa dola 60,000 (zaidi ya sh. milioni 96) kwa ajili ya mashindano ya U12, na dola 50,000 (zaidi ya sh. milioni 80) kwa ajili ya maandalizi ya Serengeti Boys kwa mechi dhidi ya Afrika Kusini.

Rais Malinzi ameishukuru Symbion kwa kukubali kushirikiana na TFF katika mpira wa miguu wa vijana, lakini vilevile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwani ndiye chachu ya kampuni hiyo kuamua kujishirikisha na mpira wa miguu wa vijana.

*ZAMBIA WATUA KUIKABILI TWIGA STARS
Timu ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo) inatua nchini kesho mchana (Februari 27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka huu).

Shepolopolo yenye msafara wa watu 29 itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na itafikia kwenye hoteli ya Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.

Waamuzi wa mechi hiyo kutoka Burundi wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.

*RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars).


Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.

*CHAMA cha Mapinduzi (CCM), chajiingiza matatani baada ya kuwapangisha wafanyabiashara wawili katika flemu moja

indexCHAMA cha Mapinduzi (ccm), kimejiingiza matatani baada ya kuwapangisha wafanyabiashara wawili katika flemu moja ya kufanyia biashara.  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam mfanyabishara Charles Msigwa alisema aliingia mkataba na Mecy Mziray ambaye kwa sasa ni marehemu na aliendelea kumlipa kodi ndugu wa marehemu Vesta Haule. 

Alisema wakati akiendelea kufanya biashara katika banda hilo alishangazwa na viongozi wa CCM tawi la Vigaeni Kata ya Ndugumbi kumfuata wakitaka aingie mkataba upya na chama hicho. 

“Nimekuwa nikiendesha shughuli zangu za biashara kwa muda wa miaka minne ndipo nilipofuatwa na viongozi wa CCM na kunishauri nichukue mkataba nao ili chama kipate mapato,”alisema Msigwa. 

Aliongeza kuwa viongozi hao walimuita kwenye ofisi ya tawi na kumuhakikishia hakutakuwa na tatizo lolote juu ya mkataba huo. “Viongozi hao waliniambia kuwa mabanda hayo hayarithishwi hata hivyo aliyeachiwa amekuwa msumbufu wa kodi mwenye banda alishafariki kwa hiyo banda huwa linarudi na kuwa mali ya chama,”alisema. 

Msigwa alisema kuwa aliujaza mkataba huo na kuurudisha ofisini kwao alipotaka kuulipia akawa anazungushwa zungushwa. 

“Nilipeleka malalamiko yangu Kwa uongozi wa Wilaya ambapo uliwaandikia barua ya kwamaba wanitafutie banda jingine iwapo nikiwa tayari kutimiza masharti ya kuwa mpangaji wa chama hicho na nilikubali lakini uongozi huo haukufanya kama ulivyo agizwa,”alisema Msigwa. 

Awali Chama cha mapinduzi (CCM) kiliingia mkataba wa kujenga banda hilo na Marehemu Mecy Mziray gharama zake na asingeweza kutoka mpaka gharama zake za ujezi zitakapo malizika.

Monday, January 6, 2014

BOFYA HAPA UCHEKI MY NUMBER ONE REMIX YA DIAMOND FT DAVIDO

Number One Diamond and Davido

*MIONDOKO YA HARUSI YA MOHAMED NA ELIZABETH


KWA MAHITAJI YAKO KATIKA SHUGHULI ZA SHEREHE KAMA VIDEO, PICHA, MUZIKI NA MC'S PIA KAVA DISGN, VIDEO EDITING N.K WAWEZA KUWASILIANA NASI KWA:-

SIMU NO:- 0752 882038/0714656660/0784782038 au 0655 306109/0787 200005/0754306109
BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com

WEBSITE:- www.sufianimafoto.com, www.nasmamafoto.blogspot.com

Sunday, January 5, 2014

*RAIS KIWETE ALIPOPOKEA MATEMBEZI YA UVCCM ZANZIBAR JANA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, jana.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akikagua Brass Band ya  Chipukizi kabla ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na wana UVCCM baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Mwenyekiwa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar  Dkt Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine waki imba wimbo wa mashujaa wakati wa  ya kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akihutubia baada ya  kupokea maandamano ya watembeaji  kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar. PICHA NA IKULU