Tuesday, March 25, 2014

*KASEBA NA MASHALI NANI ZAIDI WA MANZESE V/S MWANANYAMALA

MARASTA WAKUTANISHWA, Japhet Kaseba (kushoto) akipozi na Thomas Mashali, wakati wa utambulisho wa pambano lao la jumamosi.
****************************************************
Hivi karibuni watakutanishwa miamba miwili ulingoni wote wakiwa na nywele zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasta, Miamba hiyo  ambayo mara nyingi huwa gumzo la watu mitaani hususani wapenda mchezo wa ngumi kwa tabia zao na vibweka vyao , hao si wengine bali ni Japhet kaseba na bondia mtukutu Thomas Mashali, ambao  jumamosi ya terehe 29/3/2014 watapanda ulingoni katika ukumbi  PTA viwanja wa maonesho sabasaba, kuonyeshana kazi.
 Thomas  mashali “simba asiyefugika – kama anavojiita” alizaliwa sept 1989 na kukulia mitaa ya manzese jijini Dare s salaam, akiwa mtoto mtundu, mkorofi, mgomvimgovi  na mpenda michezo kama ilivyo kwa mdogo wake Charles Mashali, ambaye pia  alikuwa  bondia mzuri aliyetokea kuwashinda na  kuwasumbua mabondia wengi kama kina Francis Miyeyusho, alishawahi kuchukua ubingwa wa taifa kabla ya kuachana na mchezo wa ngumi.
Mashali amewahi kuwa kivutio cha wengi  ulingoni na kero kwa wengine uraiani kwa tabia yake ya kuwapigapiga  watu na kuwaonea wasio na hatia na kuendekeza ubabe usio na maana akiwa kama tembo wa mitaa ya manzese kwa tabia yake iliyomfanya kwenda jela  mara kwa mara na kumpotezea dira imara katika masumbwi  na kukaa muda mrefu bila kupigana.
Mwaka 2009 alipotokea jamaa mmoja anayeitwa juma shumbili ambae ni promota wa mapambano madogomadogo ya mchangani lakini kwa wakati huu alikuwa anaandaa zaidi katika ukumbi wa texas hall manzese na kumuandalia pambano Thomas mashali akiwa kama mbabe wa manzese na amadu mwalimu akiwa kama  mbabe wa tandika.
Matokeo Mashali aliibuka mshindi  wa pambano hilo kwa kumpiga amadu mwalimu kwa no kaunti ya raundi ya tatu na hili ndilo pambano lake la kwanza rasmi la kulipwa  lililomuingiza katika rekodi ya mabondia  wa kulipwa nchini.
Sasa, Jumamosi Mashali niuso kwa uso na Japhet Kaseba, nani kuibuka kidedea?????

No comments:

Post a Comment