Saturday, March 29, 2014

*MARY KAUNGA ALIVYOMEREMETA KATIKA SHEREHE YAKE YA SEND OFF JIJINI DAR ES SALAAM.



Bi Mary Kaunga (kushoto) na msimazi Jenifer Lweje, wakiingia katika ukumbini, wa Mwenge Social wakati wa sherehe ya kuagwa. 
  Bi Mary Kaunga akiingia katika ukumbini, wakati wa sherehe ya kumuaga 'Send off party'  kulia ni mpambe wake  Jenifer Lweje.
 Wadogo ambao pia walikuwa ni wasimamizi wa Bi Harusi mtarajiwa, Mary Kaunga, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya 'Send off' iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jijini Dar es Salaam.
 Ni wakati wa mkono wa pongezi.
 Wakati wa zawadi kumpongeza Bi harusi mtarajiwa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu

*WANANCHI WA HANDENI WALALAMIKIA KUPORWA ARDHI



 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu pichani.
Alisema hali hiyo imewafanya waishi kwa mashaka wakiamini kuwa ataendelea na tabia yake hiyo, licha ya kumiliki eneo zaidi ya heka 120 hali ya kuwa anashindwa kulilima.

*******************************************************
Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
WANANCHI wa Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wamemlalamikia mwekezaji anayejulikana kwa jina la Amina Singa, kuwa anapora ardhi zao, huku serikali ya Kata Kwamatuku, ikishindwa kuwatetea wakulima wadogo na kuelemea upande wa mwekezaji.
Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Nassib Bakari, pichani.
Mwandishi wa habari hizi alitembelea katika kijiji hicho na kufanya mazungumzo na wananchi sambamba na Baraza la Kata juu ya mgogoro huo unaosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wakulima hao.
Mjumbe wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Mwanahamisi Nyata, pichani.
Akizungumza kwa huzuni kubwa, mkulima aliyejitambulisha kwa jina la Hausi Zuberi, alisema kuwa mwekezaji huyo amechota eneo lake, kama alivyofanya hivyo kwa wananchi wengine waliopakana na shamba lake.
Hausi Zuberi, mmoja wa walalamikaji wa migogoro ya ardhi katika Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
“Mwekezaji huyu ni kero kubwa kwetu kwasababu amechota maeneo yetu wakulima tusiopungua 6 baada ya kuvuka mbele ya mpaka wake, hali inayotufanya tuishi kwa hofu tukiamini kuwa ataendelea kutupora,” alisema.

Naye Paulina Athon Simbaulanga, alisema kuwa uporaji huo umebarikiwa na Baraza la Kata, baada ya kutembelea eneo hilo, jambo linalowafanya waamini kuwa kuna njia ya mkato iliyopitwa katika kufanikisha uporaji huo.

“Amina alikuja kijijini kwetu na kuomba heka 60, lakini sasa ana heka 120 na bado anapora sisi tusiokuwa na hata heka 5, licha ya yeye kumiliki eneo kubwa.

“Hatujui hizo heka nyingine amezipata vipi na sheria za ardhi zinasemaje katika hilo, ingawa serikali ya kijiji inajua na mgogoro huu umebarikiwa na viongozi wetu,” alisema.

Alipotafutwa Amina, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwakuwa wananchi hao ndio waliovamia shamba lake, licha ya kushindwa kusema ni kiasi gani cha shamba analomiliki kijijini hapo kutoka heka 50 zinazotakiwa kisheria.

“Kwanza mtakuwa umefanya makosa kama mmeamua kufanya mazungumzo na wananchi hao kabla yangu, hivyo siwezi kusema lolote,” alisema Amina.

Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Nassibu Bakari Bigo, alikiri kuupokea mgogoro huo wa Amina na wakulima wa kijiji cha Komsala, huku akisema kesi za aina hiyo zimeendelea kushamiri katika maeneo mengi katika Kata hiyo.

“Tuliupokea mgogoro huo, lakini kwa kiasi kikubwa umechangiwa na serikali ya kijiji husika kwa kushindwa kutatua kesi hizo na watu kusaka haki yao Baraza la Kata,” alisema Bakari.

Kwa mujibu wa Bakari, kesi za migogoro ya ardhi zimeshamiri katika eneo lao, hivyo viongozi wa vijiji wanapaswa kusimamia vyema sheria za ardhi, huku wakitoa elimu kwa wakulima na wananchi wao, wakiwamo walalamikaji wa kesi inayomhusisha Amina, kutokana na mashahidi wao kushindwa kufika walipoitwa na Baraza la Kata

*SERIKALI KUJENGA BANDARI YA MWAMBANI



 Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo, kutoka Tume ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Maduka Kessy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya mwambani ambapo upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga akionesha eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
 imu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi (wa pili kulia) ufukweni mwa bahari, eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha na Joyce Mkinga

Tuesday, March 25, 2014

*BALOZI IDDI AKUTANA NA TAASISI ZA UWEKEZAJI VITEGA UCHUMI KUTOKA WA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA UJENZI


Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Taasisi na washirika wa Maendeleo bado wana fursa nzuri na pana ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo na Kiuchumi. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

*RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA MAABARA YA SHULE YA SEKONDARI MADAGO KOROGWE

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa Maabara ya shule ya Sekondari Madago, wilaya ya Korogwe jana mchana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Tanga. Picha na Freddy Maro

*MAJINA WA VIONGOZI WA KAMATI 12 ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA NA KAMATI YA UONGOZI YATAJWA


Na Magreth Kinabo,  MaelezoDodoma   
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo, ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.

Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo  baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika (jana) Machi 24 , mwaka  2014 mjini  Dodoma .

Mwenyekiti huyo aliyataja majina hayo  katika  Kamati  ya Uandishi Mwenyekiti Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni  Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni Prof. Makame  Mbalawa.

Wengine waliochaguliwa  katika Kamati Na. 2 Mwenyekiti ni Shamsi Vuai Nahodha, Makamu wake ni Shamsa Mwangunga.Kamati Na. 3 Mwenyekiti  ni  Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma MussaJuma.

Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni  Christopher  Ole-Sendeka, Makamu wake ni  Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni  Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni  Assumpter  Mshama.

          Viongozi waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti Stephen Wassira na Makamu wake ni Dkt. Maua  Daftari.Kamati Na. 7  Mwenyekiti  Brig. Hassan Ngwilizi  ,Makamu wake  Waride   BakariJabu.Kamati Na. 8 Mwenyekiti  ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya   Othman.

Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh,Makamu wake Wiliam  Ngeleja,Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna  Abdallah, Makamu wake ni   Salmin Awadh Salmin.Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni Anne  Malecela, Makamu wake  Hamad  Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti  Paul Kimiti na Makamu wake ni  Thuwaybah E. Kisasi.

Wakati huohuo , Sitta  alitangaza wajumbe wa Kamati ya  Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba, ambao  ni wenyekiti na makamu wenyeviti wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua.

 Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamad Abuu Juma.

 Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na katika nafasi hiyo 

*HABARI KUTOKA TFF LEO, KORTI YAAGIZA TFF IKAMATE MIL 106/- KULIPA WACHEZAJI YANGA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tumepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.

Tayari tumeanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.

Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.

Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.

Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo.

*AZAM, YANGA VIWANJANI DAR, TANGA VPL
Timu za Azam na Yanga ambazo zinachuana kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara zinashuka tena viwanjani kesho (Machi 26 mwaka huu) kuwania pointi tatu.

Azam yenye pointi 47 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Mgambo Shooting ipo katika nafasi ya kumi na moja kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 19.

Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na Tanzania Prisons kuanzia saa 10.30 jioni. Yanga ipo nyuma ya Azam kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 47. Hata hivyo, timu hiyo ina mchezo mmoja mkononi.
Tanzania Prisons ambayo ipo chini ya Kocha David Mwamaja hivi sasa ina pointi 22 ikiwa katika nafasi ya kumi. Timu tatu za mwisho katika ligi hiyo itakayomalizika Aprili 19 mwaka huu zitashuka kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Ligi itaendelea tena Jumamosi (Machi 29 mwaka huu) kwa mechi kati ya Ashanti United na Oljoro JKT itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Jumapili (Machi 30 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Kagera Sugar na Ruvu Shooting (Uwanja wa Kaitaba), Mtibwa Sugar na Coastal Union (Uwanja wa Manungu), JKT Ruvu na Rhino Rangers (Uwanja wa Azam Complex), Azam na Simba (Uwanja wa Taifa) na Mgambo Shooting na Yanga (Uwanja wa Mkwakwani).

*KAMATI YA SHERIA KUPITIA MAREKEBISHO YA KATIBA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana mwishoni mwa wiki kupitia taarifa ya utekelezaji wa agizo la wanachama kurekebisha katiba zao.

TFF tulitoa agizo kwa wanachama wetu kufanyia marekebisho katiba ikiwemo kuingiza Kamati ya Maadili. Mwisho wa utekelezaji wa agizo hilo ulikuwa Machi 20 mwaka huu.

Hivyo, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapokea taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa Sekretarieti, na baadaye kutoa mwongozo wa hatua inayofuata.

*TIMU YA WATOTO WA MITAANI YAENDA BRAZIL
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo (Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani.

John Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania.

Michuano hiyo ya siku 10 inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana) inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.

Mwaka 2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.

*MABINGWA WA MIKOA WATAKIWA MACHI 30
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwa vinatakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu.

Majina ya mabingwa yanatakiwa kuwasilishwa pamoja na usajili wa wachezaji waliotumika kwenye ligi ya mkoa. Kila klabu inaruhusiwa kuongeza wachezaji watano kutoka ndani ya mkoa husika, ambapo unatakiwa uthibitisho wa usajili huo.


Mpaka sasa ni vyama viwili tu ndivyo vimeshawasilisha mabingwa wao. Vyama hivyo ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) ambapo bingwa wake ni Kiluvya United, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi (LIREFA) ambapo bingwa ni Kariakoo SC

*KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA LEO


 Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum wote 12  pamoja na mambo mengine inajukumu la kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mhe. Sitta akiendelea kuongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi
 Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Uongozi Mhe. Anna Abdalah akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe...Picha na Owen Mwandumbya

*RAIS KIKWETE AZINDUA UKARABATI WA BARABARA YA KOROGWE HADI MKUMBARA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wapili kushoto),Wziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli(kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Burundi na Uganda Bwana Philippe Dongier(watatu kushoto),Mwakilkishi wa Kampuni ya ujenzi ya Strabag Bwana Philip Raiver(wanne kushoto) na mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS mhandisi Patrick Mfugale(kulia) wakiata utepe kuzindua rasmi uakarabati wa Barabara ya Korogwe-Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76 jana mjini Korogwe.Ukarabati huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati), Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(kushoto), pamoja na Mwakiklishi wa Benki ya Dunia Bwana Philippe Dongier wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ukarabati wa barabara ya Korogwe hadi Mkumbara kwa ufadhili ya Benki ya dunia.Uzinduzi huo ulifanyika mjini Korogwe jana .Wanne kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Lutemi Mstaafu Chiku Galawa.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiandaa kuapanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa Barabara ya Korogwe hadi Mkumbara jana mjini Korogwe huku mwakilkishi wa Benki ya Dunia inayofadhili mradi huo Bwana Phillippe Dongier akiangalia. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kata ya nchi za Tanzania, Burundi na Uganda Bwana Philippe Dongier (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa Barabara ya Korogwe Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76 uliofanyika jana mjini Korogwe.Kulia ni Waziri wa ujenzi Mh. John Pombe Magufuli. Picha na Freddy Maro.

*RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MKATA HANDENI KOROGWE

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wengine wa wilaya ya Handeni na Mkoa wa Tanga wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua rasmi barabara ya kilometa 119 ya Mkata Handeni Korogwe jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kufungua rasmi barabara ya Mkata Handeni Korogwe jana jioni.Pembeni ya Rais kulia ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli.