Saturday, March 29, 2014

*WANANCHI WA MJI WA KOROGWE WAUPOKEA KWA KISHINDO MPANGO WA TIKA, WACHANGIA MIL. 1.3



Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akifungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Kikao hicho kimefanyika leo Machi 28, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mheshimiwa Mrisho Gambo akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa (kushoto). Pembeni ni Diwani wa Kata ya Mgombezi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya, Maji na Uchumi, Mheshimiwa Omari Chafesi na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akieleza umuhimu wa matumizi ya Tiba kwa Kadi (TIKA) mbele ya mkuu wa mkoa wa Tanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kushoto) akiendesha mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi. Pembeni ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya mji Korogwe, Dokta Jerry Mwakanyamale.
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Singida, Bw. Issaya Shekifu akitoa uzoefu wake katika moja ya Wilaya ya Ilamba, Singida jinsi wananchi wanavyofaidika na TIKA.
Viongozi wa Dini wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Wananchi wa Mji wa Korogwe wakifuatilia mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Msikiti Mkuu Manundu, Korogwe Mzee Daffa Daffa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Ngalawa akisalimia na viongozi wa dini wa Halmashauri ya Mji Korogwe mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
Waheshimiwa Madiwani wa Kata mbalimbali za Halmshauri ya Mji Korogwe wakiwa katika mkutano wa siku ya wadau wa Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) ambapo Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kuchukua maoni yao na kuwaeleza jinsi TIKA inavyofanya kazi.
NHIF 11: Afisa Matekelezo na Uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- Dar es Salaam, Genoveva Vicent akitoa majumuisho jinsi Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA) unavyoweza kuwasaidia wananchi.

Mchungaji Joseph Mhina wa Kanisa la Anglikana Manundu, Korogwe akitoa shukrani kwa wananchi waliofika katika mkutano huo wa wadau. 
Timu ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dar es Salaam na Tanga waliokuwa wakiratibu mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa na Wilaya. Picha zote na Cathbert Kajuna
**************************************
MAAZIMIO YA KIKAO CHA WADAU WA TIKA KATIKA HALMASHAURI YA MJI KOROGWE:-
1. Washiriki wote wa kikao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wamekubaliana kwa kauli moja kukatwa Tshs.10,000 za posho zao kama mchango wa TIKA ili kusaidia wazee na wenye mahitaji maalumu.

2. Kila mshiriki awe mwalimu na mhamasishaji kwa wale wote ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kikao hiki cha wadau wa TIKA
3. Mfuko wa TIKA ni mali ya wana Korogwe hivyo kila mwananchi mwenye uwezo na mfanyakazi achangie kiwango cha Tshs.10,000 kama mchango wa TIKA kwa mwaka kwa mtu mmoja.

4. Watendaji wa Mitaa,Kata na halmashauri wawe karibu na wenyeviti wa mitaa katika kuhamasisha jamii kujiunga na TIKA.
5. Kuhamasisha wanakorogwe walio nje ya Korogwe kuchangia Mfuko wa TIKA kwa kiwango kilichowekwa ili kuuboresha mfuko na kusaidiwa wenye mahitaji muhimu na wazee.

6. Wana Korogwe wenye uwezo zaidi kiuchumi waliopo Korogwe waombwe kuchangia mfuko huu ili kuuboresha.
7. Kuhamasisha makundi maalumu kujiunga na TIKA mfano walemavu,na wawakilishi wao waliohudhuria semina hii wakawe mfano kwa kujiunga na TIKA na kuhamasisha wenzao.

8. Watendaji wa Kata na Mitaa/Vijiji waitishe mikutano ya hadhara kwa ajili ya uhamasishaji na washarikiane na washiriki waliopata mafunzo/semina hii.
9. Viongozi wa dini watatumia vikao vya kidini kwa ngazi zote kitaka kuhamasisha jamii na waumini (misikitini na makanisani)

*WASHINDI WA TUZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA WATUNUKIWA NA MH RAIS.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi walionyakua tuzo mbalimbali wakati wa hafla ya kutunuku Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora wa mwaka 2013 iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku. Picha na Freddy Maro

*BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPITISHA AZIMIO LA KURA YA MSETO



Hatimaye baada ya mvutano wa baadhi wa wajumbe wa Bunge la  Maalum la Katiba kuhusu upigaji wa kura ya siri na ya wazi kuendelea  leo  Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Pandu Ameir Kificho amewasilisha  azimio la mapendekezo ya  ya upigaji kura wa wazi na siri  kutumika kwa pamoja katika kaununi ya 37 na 38, ambalo limetipitishwa na Bunge hilo kwa  matokeo ya  jumla kwa kura  ya ndiyo 376 na hapana 133 .

Kura hizo zimetangazwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge ,hilo, Mhe.Samia  Sululu kabla ya kuahirisha  kikao hicho leo usiku, ambapo  alisema   azimio hilo limepitishwa na Bunge hilo , kufuatia  upigaji wa kura ,ambapo  idadi ya kura zilizopigwa ni  509, wakati mauhudhurio  ya wajumbe yalikuwa 511.
Mhe . Samia alisema kwa  upande wa kura za wazi zilizopigwa ni 438, ambazo za ndiyo zilikuwa 351 na hapana ni 87, wakati kura za siri  zilizopigwa zilikuwa ni 71, ambazo  za ndiyo zilikuwa 25 na hapana ni 46.

Uamuzi huo umefuatiwa  baada  ya hali hiyo ambayo ilitokea tena  kwa mara nyingine jana jioni  mara baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Kificho kuwasilisha mapendekezo  ya upigaji kura wa wazi na siri  kutumika kwa pamoja katika kaununi  hizo.

Tangu jana jioni na leo  baadhi ya wajumbe wamekuwa wakitoa michango kutaka upigaji kura huo uwe wa wazi  na siri , huku wengine kutaka kura ya siri.
Awali  Kanuni za 37 na  38 zilibaki kiporo tangu wakati wa utungaji wa kanuni   mbalimbali za Bunge hilo,  na uchangiaji wa kuziboresha, kutokana na mvutano huo, ambao baadhi ya wajumbe  kutaka kura ya uwazi na wengine siri.
Wakizungumzia juu ya makubaliano yaliyofanywa na Kamati ndogo ya Muda ya Maridhiano  na Kamati ya  Kanuni na Haki za Bunge  kuhusu mapendekezo ya upigaji kura huo.  
Mmoja ya wajumbe wa Kamati hiyo ndogo ya Maridhiano, John Nyika alisema  walifanya mazungumzo hayo waliona ni vema  wakubaliana   mtu anayeweza kupiga kura ya uwazi  na anayetaka ya siri wapige kulingana na matakwa yao  ili kuwezesha mchakato huo kupiga hatua mbele.

“ Tunaomba utaratibu huu wa maridhiano  uendelee  … ili tuweze kupiga  hatua  mbele,” huku akisisitiza hawana dhamira yoyote ya  kukwamisha mchakato wa Katiba mpya. Hivyo watakuwa wa kwanza kuunga mkono kwa kura azimio litakalopitishwa kwa kura zitakazokubaliwa.
Naye mjumbe mwingine wa kamati hiyo , Vuai Ali Vuai alisema jambo hilo ni kubwa  kwa Watanzania ndio maana wanatakiwa kupiga kura kwa uwazi umma uweze kuona .

 Kwa upande wake ,mjumbe mwingine wa kamati hiyo ya ndogo  ya Maridhiano Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela amesema   ni vizuri wajumbe hao wakakubali azimio hilo kwa kuwa mpaka sasa wameshatumia siku 40 kujadili kanuni za kuongoza Bunge hilo na zimetumia gharama hivyo wasiendelee kuongeza gharama, zipo siku tatu za kuomba ili kufanikisha maridhiano hayo.

“ Ninawaomba wajumbe wenzangu kukubali azimio hili ili tuweze kusonga mbele na na mchakato wa kupata Katiba ,” alisema Askofu Mtetemela

*RIDHIWANI AITEKA PERA,AHIDIWA KURA ZA KUTOSHA APRILI 6




Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete  akihutubia wakazi wa kijiji cha Pera wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani aliwaambia wananchi hao kura yao ya tarehe 6 mwezi wa Nne itakuwa ndio jibu la changamoto zote kwa wananchi wa jimbo la Chalinze kwani anatambua Changamoto zote za jimbo hilo.

Wananchi wa Kata Pera waahidi kumpigia kura Ridhiwani Kikwete tarehe 6 mwezi wa nne baada ya kuridhishwa na Hotuba zake zinazogusa changamoto zao kama elimu, maji, zahanati, barabara na namna atakavyoboresha miundo mbinu ya jimbo la Chalinze na kuwasaidia wafugaji katika suala zima la kuongeza majosho ya mifugo.
 Imani Madega akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Pera na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuhakikisha Ridhiwani Kikwete anashinda kwa kura nyingi ilikufanikisha azma ya kusaidia jimbo la Chalinze kukua kimaendeleo inakua.
 Msanii Sam wa Ukweli akiruka juu na Morani wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM uliofanyika Mbala Kijiweni, kitongoji cha Mbala kwenye kijiji cha Chamakweza kata ya Pera.
 Meneja wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Steven Kazidi akizungumza na viongozi wa wafugaji wa kijiji cha  Chamakweza kata ya Pera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbala Kijiweni.
 Mgombea Ubunge wa CCM Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafugaji wa kijiji cha Chamakweza ,Ridhiwani alihutubia wafugaji hao ambao walimueleza kuwa wanatatizo kubwa la majosho ya mifugo yao na wanaamini yeye akiwa Mbunge atawasaidia katika kuboresha miundo mbinu itakayowasaidia kufuga kwa kisasa zaidi.
Wananchi wa Bwawani Pingo wakielekea kwenye uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la CCM lililokuwa likizinduliwa na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

*TUZO YA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2014 - 2014 LEO,MGENI RASMI WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda kesho atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013-14, itakayowakutanisha wanawake wanne itakayofanyika kesho katika Ukumbi wa The African Dream mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ndiye atakuwa mgeni rasmi katika utoaji tuzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, ambayo ndiyo iliyoratibu zoezi hilo, Eric Shigongo, alisema jana kwamba shughuli hiyo itakuwa ni hitimisho la kazi kubwa ya kupokea na kuchuja kura zilizotumwa na wasomaji kumtafuta mwanamke bora ambaye ni nembo kwa taifa.
Prof. Anna Tibaijuka.
“Zoezi hili lilifanyika kwa muda wa miezi tisa, kuanzia Juni mwaka jana hadi Machi mwaka huu. Awali kabisa watu walitakiwa kutuma majina ya wanawake wanaowaona ni bora ili wapigiwe kura, watu waliitikia vizuri sana, kwani jumla ya majina 150 yalitumwa katika kipindi cha miezi miwili.
Dk. Asha Rose Migiro.
“Baada ya hapo majina hayo yakaandikwa katika magazeti na watu wakatakiwa kupiga kura ili kuwatoa wanawake ambao wanadhani hawakustahili tuzo hizo,” alisema Shigongo, ambaye kampuni yake inatoa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi.
Alisema katika awamu ya kwanza ya miezi hiyo miwili, majina ya wanawake 20 yaling’ara na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya kupigiwa kura, ambapo baada ya muda kama huo pia, wanawake kumi walipata alama nyingi na hivyo kuingia katika awamu ya tatu na ya mwisho.
Mh. Anne Kilango Malechela.
Alisema kwenye hatua hiyo ya mwisho, wanawake watano walipita ambao ni Ananilea Nkya, Anna Tibaijuka, Anna Kilango Malecela, Asha Rose Migiro na mama Maria Kham. Katika zoezi hilo, wanawake hao wenye mvuto katika jamii walichuana na mmoja wao, Nkya, kuondolewa baada ya kura zake kutotosha kwa ajili ya fainali,” alisema Shigongo.
Dk. Maria Kamm.
Kwa upande wake, mratibu wa Tuzo hizo, Luqman Maloto, alisema tukio hilo la kihistoria ambalo pia litashuhudiwa na wabunge wa Bunge la Katiba walio mjini Dodoma, litaambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali, akiwemo Linah,” alisema Maloto

*STOOOP! KIGODORO, KHANGA MOKO NDEMBENDEMBE, TISHETI NDEMBENDEMBE ZAPIGWA STOP MISS TANZANIA



Na Michael Maurus, Dar es Salaam
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA), limeitaka Kamati ya Miss Tanzania kutohusisha burudani zinazokiuka maadili ya Mtanzania wakati wa mashindano yao ya urembo mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mashindano ya Miss Tanzania 2013 kilichofanyika kwenye ukumbi wa baraza hilo, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa BASATA, Vivian Shalua, alisema kuwa maadili ni muhimu kuzingatiwa katika mashindano hayo ili kuepukana na dhana potofu kuwa yanahusiana na uhuni.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kulia akiwa na Miss Tanzania wa mwaka 1998, Basila Mwanukuzi

“Maadili yazingatiwe katika mashindano ya mwaka huu, kuanzia kwa washiriki hadi burudani zitakazohusishwa, kama ‘vigodoro’, ‘kanga moja mbendembende’ na nasikia siku hizi kuna ‘tisheti ndembendembe’,” alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema kuwa BASATA ipo tayari kuyapigania mashindano ya Miss Tanzania kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo.

Mkurugenzi huyo pia aliitaka Lino kuwaelimisha mawakala wanaoandaa mashindano hayo juu ya umuhimu wa kuwa na vibali kutoka BASATA, ikiwa ni pamoja na kutowavumilia watovu wa nidhamu bila kujali ukongwe wao katika tasnia hiyo.

Kwa upande wake, Ofisa Sanaa Kitengo cha Matukio, Kurwijira Maregesi, aliitaka Lino kujipanga kujiweka tayari kufanya mashindano hata pale inapokosa mdhamini, huku mjumbe mwingine katika kikao hicho ambaye ni Ofisa Sanaa BASATA, Philemon Mwasanga, akisisitiza mawakala kuwekeana mikataba na warembo kabla ya mashindano kuanza.
“Lino isiwafumbie macho mawakala wasiojali mikataba na warembo, na warembo waisome na kuielewa ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea,” alisema.

Akijibu hoja kadhaa zilizoibuliwa katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga, alisema kuwa wamejipanga ili kuweza kufanya mashindano yao bila kutegemea wadhamini, huku akiitaka BASATA kuwasaidia katika hilo.

“Tatizo mashindano yetu gharama yake ni kubwa sana, nasi hatupendi kuona ubora wake ukishuka kutokana na kushindwa kumudu gharama, ndio maana tumekuwa tukihangaika kuomba udhamini kutoka katika makampuni mbalimbali makubwa hapa nchini,” alisema.

Juu ya mikataba baina ya warembo na mawakala, Lundenga alisema: “Mwaka huu 
tumesisitiza mawakala waingie mikataba na washiriki kabla ya mashindano na tutakuwa makini katika kufuatilia hilo na changamoto nyinginezo zilizoibuliwa katika kikao hiki.”

Mmoja wa warembo walioshiriki mashindano ya mwaka jana ambaye ni Miss Sinza 2013, Prisca Clement, alisema kuwa kuna umuhimu wa kuongezwa kwa zawadi katika ngazi za chini ili kumwezesha mshiriki kujivunia na kujitosa kwake katika mashinsdano hayo bila kujali kama ameshinda au la.

Mashindano ya Miss Tanzania 2014 yamezinduliwa mapema wiki hii ambapo fainali zake zinatarajiwa kuwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Orginal.

*MARY KAUNGA ALIVYOMEREMETA KATIKA SHEREHE YAKE YA SEND OFF JIJINI DAR ES SALAAM.



Bi Mary Kaunga (kushoto) na msimazi Jenifer Lweje, wakiingia katika ukumbini, wa Mwenge Social wakati wa sherehe ya kuagwa. 
  Bi Mary Kaunga akiingia katika ukumbini, wakati wa sherehe ya kumuaga 'Send off party'  kulia ni mpambe wake  Jenifer Lweje.
 Wadogo ambao pia walikuwa ni wasimamizi wa Bi Harusi mtarajiwa, Mary Kaunga, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya 'Send off' iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jijini Dar es Salaam.
 Ni wakati wa mkono wa pongezi.
 Wakati wa zawadi kumpongeza Bi harusi mtarajiwa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu

*WANANCHI WA HANDENI WALALAMIKIA KUPORWA ARDHI



 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu pichani.
Alisema hali hiyo imewafanya waishi kwa mashaka wakiamini kuwa ataendelea na tabia yake hiyo, licha ya kumiliki eneo zaidi ya heka 120 hali ya kuwa anashindwa kulilima.

*******************************************************
Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni
WANANCHI wa Kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wamemlalamikia mwekezaji anayejulikana kwa jina la Amina Singa, kuwa anapora ardhi zao, huku serikali ya Kata Kwamatuku, ikishindwa kuwatetea wakulima wadogo na kuelemea upande wa mwekezaji.
Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Nassib Bakari, pichani.
Mwandishi wa habari hizi alitembelea katika kijiji hicho na kufanya mazungumzo na wananchi sambamba na Baraza la Kata juu ya mgogoro huo unaosababisha malalamiko mengi kutoka kwa wakulima hao.
Mjumbe wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, Mwanahamisi Nyata, pichani.
Akizungumza kwa huzuni kubwa, mkulima aliyejitambulisha kwa jina la Hausi Zuberi, alisema kuwa mwekezaji huyo amechota eneo lake, kama alivyofanya hivyo kwa wananchi wengine waliopakana na shamba lake.
Hausi Zuberi, mmoja wa walalamikaji wa migogoro ya ardhi katika Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
“Mwekezaji huyu ni kero kubwa kwetu kwasababu amechota maeneo yetu wakulima tusiopungua 6 baada ya kuvuka mbele ya mpaka wake, hali inayotufanya tuishi kwa hofu tukiamini kuwa ataendelea kutupora,” alisema.

Naye Paulina Athon Simbaulanga, alisema kuwa uporaji huo umebarikiwa na Baraza la Kata, baada ya kutembelea eneo hilo, jambo linalowafanya waamini kuwa kuna njia ya mkato iliyopitwa katika kufanikisha uporaji huo.

“Amina alikuja kijijini kwetu na kuomba heka 60, lakini sasa ana heka 120 na bado anapora sisi tusiokuwa na hata heka 5, licha ya yeye kumiliki eneo kubwa.

“Hatujui hizo heka nyingine amezipata vipi na sheria za ardhi zinasemaje katika hilo, ingawa serikali ya kijiji inajua na mgogoro huu umebarikiwa na viongozi wetu,” alisema.

Alipotafutwa Amina, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwakuwa wananchi hao ndio waliovamia shamba lake, licha ya kushindwa kusema ni kiasi gani cha shamba analomiliki kijijini hapo kutoka heka 50 zinazotakiwa kisheria.

“Kwanza mtakuwa umefanya makosa kama mmeamua kufanya mazungumzo na wananchi hao kabla yangu, hivyo siwezi kusema lolote,” alisema Amina.

Katibu wa Baraza la Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Nassibu Bakari Bigo, alikiri kuupokea mgogoro huo wa Amina na wakulima wa kijiji cha Komsala, huku akisema kesi za aina hiyo zimeendelea kushamiri katika maeneo mengi katika Kata hiyo.

“Tuliupokea mgogoro huo, lakini kwa kiasi kikubwa umechangiwa na serikali ya kijiji husika kwa kushindwa kutatua kesi hizo na watu kusaka haki yao Baraza la Kata,” alisema Bakari.

Kwa mujibu wa Bakari, kesi za migogoro ya ardhi zimeshamiri katika eneo lao, hivyo viongozi wa vijiji wanapaswa kusimamia vyema sheria za ardhi, huku wakitoa elimu kwa wakulima na wananchi wao, wakiwamo walalamikaji wa kesi inayomhusisha Amina, kutokana na mashahidi wao kushindwa kufika walipoitwa na Baraza la Kata

*SERIKALI KUJENGA BANDARI YA MWAMBANI



 Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo, kutoka Tume ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Bw. Maduka Kessy (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bandari ya mwambani ambapo upembuzi yakinifu tayari umeshafanyika.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga akionesha eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
 imu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Freddy Liundi (wa pili kulia) ufukweni mwa bahari, eneo ambapo bandari ya Mwambani itajengwa.
Picha na Joyce Mkinga

Tuesday, March 25, 2014

*BALOZI IDDI AKUTANA NA TAASISI ZA UWEKEZAJI VITEGA UCHUMI KUTOKA WA KAMPUNI ZA KIMATAIFA ZA UJENZI


Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Taasisi na washirika wa Maendeleo bado wana fursa nzuri na pana ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi mbali mbali ya Maendeleo na Kiuchumi. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

*RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA MAABARA YA SHULE YA SEKONDARI MADAGO KOROGWE

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa Maabara ya shule ya Sekondari Madago, wilaya ya Korogwe jana mchana. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Tanga. Picha na Freddy Maro