Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Pera wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze, Ridhiwani aliwaambia wananchi hao kura yao ya tarehe 6 mwezi wa Nne itakuwa ndio jibu la changamoto zote kwa wananchi wa jimbo la Chalinze kwani anatambua Changamoto zote za jimbo hilo.
Wananchi wa Kata Pera waahidi kumpigia kura Ridhiwani Kikwete tarehe 6 mwezi wa nne baada ya kuridhishwa na Hotuba zake zinazogusa changamoto zao kama elimu, maji, zahanati, barabara na namna atakavyoboresha miundo mbinu ya jimbo la Chalinze na kuwasaidia wafugaji katika suala zima la kuongeza majosho ya mifugo.
Imani Madega akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Pera na kuwataka wana CCM kuwa kitu kimoja na kuhakikisha Ridhiwani Kikwete anashinda kwa kura nyingi ilikufanikisha azma ya kusaidia jimbo la Chalinze kukua kimaendeleo inakua.
Msanii Sam wa Ukweli akiruka juu na Morani wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge kupitia CCM uliofanyika Mbala Kijiweni, kitongoji cha Mbala kwenye kijiji cha Chamakweza kata ya Pera.
Meneja wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze Ndugu Steven Kazidi akizungumza na viongozi wa wafugaji wa kijiji cha Chamakweza kata ya Pera wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mbala Kijiweni.
Mgombea Ubunge wa CCM Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wafugaji wa kijiji cha Chamakweza ,Ridhiwani alihutubia wafugaji hao ambao walimueleza kuwa wanatatizo kubwa la majosho ya mifugo yao na wanaamini yeye akiwa Mbunge atawasaidia katika kuboresha miundo mbinu itakayowasaidia kufuga kwa kisasa zaidi.
Wananchi wa Bwawani Pingo wakielekea kwenye uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la CCM lililokuwa likizinduliwa na mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
No comments:
Post a Comment