Wachezaji wa Mchezo wa Pool,Winfrida Mponzi kutoka Chuo cha MUCCOBS na Aluiya Herode kutoka Chuo cha SMMUCO wakishindana kulagi wakati wa mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Comitition 2013 Mkoa wa Kilimanjaro.
Mchezaji wa Pool wa Chuo cha KCMC, Kim Kunthea akicheza dhidi ya mpinzani wake Idrisa Juma wa Chuo cha KCMC wakati wa fainali za mashindano ya Safavri Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 mchezaji mmoja mmoja (Singles) Mkoa wa Kilimanjaro.
Wachezaji wa timu ya Chuo cha Institute of Accountant of Arusha (IAA) wakishangilia na kitita cha sh.500,000/= ikiwa ni zawadi mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Lager Higher Learning Pool Compitition 2013 Mkoa wa Arusha.
*************************************
*************************************
MABINGWA watetezi wa Mkoa wa Kilimanjaro wa mashindano ya Pool,Chuo kikuu cha MUCCOBS, juzi walifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa elimu ya juu mkoani Kilimanjaro yajulikanayo kama 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013' baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Chuo kikuu cha MWENGE yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mambuo mwishoni mwa wiki.
Mashindano hayo yaliyoshirikisha vyuo vikuu vinne vya mkoani hapo ambavyo ni MUCCOBS,MWENGE,KCMC na SMMUCO kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Chuo cha MUCCOBS kwa kutetea ubingwa huo kilijinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pamoja tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro katika fainali za taifa zinazotarajiwa kufanyika Juni mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na chuo cha MWENGE ambacho kilijinyakulia kitita cha Sh.300,000.Nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha KCMC ambacho kilizawadiwa Sh.200,000 na nafasi ya nne ni Chuo cha SMMUCO ambacho kilipata Sh.100,000.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Idrisa Juma wa KCMC aliibuka kuwa bingwa hivyo kujinyakulia pesa taslimu Sh.150,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwa upande wa wachezaji mmoja mmoja.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Kim Kunthea wa KCMC ambaye alizawadiwa Sh.100,000.
Na kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Winfrida Mponzi wa MUCCOBS alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa pesa taslim sh.100,000 pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika mashindano ya kitaifa.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Aluiya Herode wa chuo cha SMMUCO ambaye alizawadiwa pesa taslim Sh 50,000.
Wakati jijini Arusha Mabingwa watetezi, IAA walifanikiwa kutetea ubingwa wao wa Mkoa dhidi ya Chuo cha SILA, na kwa nafasi hiyo IAA ilijinyakulia kitita cha Shilingi 500,000 pamoja na tiketi ya kushiliki mashindano ya kitaifa . huku nafasi ya pili ikishikiliwa na SILA ambao walijinyakulia kitita cha Shilingi 300,000.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na CDTI ambao walizawadiwa pesa taslimu sh.200,000.
Upande wa wachezaji mmoja mmoja wanaume Bingwa mtetezi wa Mkoa,Baraka Shayo alitetea ubingwa wake dhidi ya Baraka Robert wa chuo cha SILA, na kwa ubingwa huo, Baraka alijinyakulia pesa taslimu sh.150,000/= na nafasi ya pili ilichukuliwa na Baraka Robert wa SSILA ambaye alizawadiwa sh.100,000.
No comments:
Post a Comment