Hili ndilo lori lililopata ajali katika kijiji cha Hanga, iliyotokea jana.
********************************
Watu nane wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .
Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga pamoja na abiria
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki, amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa nne na nusu ( 4:30 ) usiku katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili Mkoa wa Ruvuma, huku ikielezwa kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi, ambapo pia imeelezwa kuwa dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha huku akiwa amelewa.
Ajali hiyo imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA.
Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo ametokomea kusikojulikana na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.
Kamanda wa Polisi amesema gari hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8) na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.
Kutokana na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mara moja.
No comments:
Post a Comment