Monday, May 27, 2013

KINANA: CCM IMEDHAMIRIA KUZOA KATA ZOTE 25

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh Deo Sanga a.k.a Jah People mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye
*************************************
*Ni Katika Uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zinaendelea baadhi ya Kata nchini

 NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
CHAMA Cha Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika kata mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo. Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na  Zuberi Nyamoleo.

"Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;

"Pale Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".

Kinana aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na  Nyamoleo kwa kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani katika kata ya Mbalamaziwa.

"Ninyi ni watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema Kinana.

Kinana alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.

"Mwanachama lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.

Kinana alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.

"Tafadhalini sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe  ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.


Kinana alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

No comments:

Post a Comment