Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa wazi wa siku moja wa Wadau wa Bodi ya TCAA , uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kuhusu maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni mbalimbali yanayohudumia viwanja vya ndege nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA , Juma Mbwana.
Mwenyekiti wa Baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa anga Tanzania Juma Fimbo(kulia) na Katibu Mtendaji wake Hamza Johari wakitoka baada ya kumalizika kwa kikao kilichowakutanisha wadau wa anga jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alia Aviation Consultants Mahmud .M. Shamte (aliesimama) akifafanua jambo katika mkutano huo wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa wazi wa maboresho wa utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja uliofanyika, jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha huduma za usafiri wa anga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.
Sehemu ya muonekano wa ukumbi wa mkutano wa Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ulikofanyika mkutano wa wazi wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa wadau wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa anga Mei 29.2013 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Equity Aviation Services (T) Ltd Rosemary Kacungira akichangia mkutano wa wazi wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya usafiri salama wa anga. Picha zote na Johary Kachwamba wa MAELEZO
No comments:
Post a Comment