* Magufuli, Mwakyembe ndani ya nyumba
KINANA |
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa kuuteka mji wa Singida kitakapofanya mkutano wa hadhara wa aina yake kwenye Uwanja wa Peoples mjini hapa.
Taarifa zilizotolewa na kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi na uenezi, Makao Makuu ya CCM, imesema, mkutano huo unaofanyika kuhitimisha ziara ya siku nane ya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi, katika mkoa huo.
Katika mkutano huo pamoja na Kinana, atakuwepo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na mawaziri kadhaa wakiwemo waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ambaye ataeleza utekelezwaji a ilani hiyo ya CCM katika kuboresha miundombinu hasa upande wa ujenbzi wa barabara na madajara na Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ambaye anatarajiwa kueleza kwa kina ubioreshaji wa reli ya kati.
Waziri mwingine ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ambaye anatarajiwa kueleza kwa marefu na mapana kuhusu migogoro ya mipaka iliyopo kati ya hifadhi za taifa na wananchi.
Baada ya mkutano huo, Kinana anatarajiwa kuendelea kesho na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Manyara.
Kabla ya kuanza ziara katika mkoa wa Singida, Kinana alifanya zaiara ya siku 11 katika mkoa wa Tabora ambako alitembelea wilaya zote kama alivyofanya pia katika mkoa huu wa Singida.
Mbali na kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kutembelea miradi mbalimbali, Kinana amekuwa akishiriki moja kwa moja katika ujenzi wa miradi hiyo kama ujenzi wa zahanati, vyumba vya maabara katika shule za sekondari, ujenzi nyumba za walimu, zahanati na vituo cha afya.
Kutokana na ziara hizo, wakati akisikiliza kero za wananchi katika mikutano ya hadhara au ya ndani ya CCM, Kinana amefanikiwa kuibua kero au changamoto ambazo katika baadhi ya maeneo zimekwamisha kutekelewa kwa miradi ikiwemo fedha kutafunwa na watendaji wa serikali au kukosekana uhamasishaji wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi.
Miongoni mwa matunda yaliyojitokeza katika ziara hizo za Kinana ni baadhi ya changamoto zilizokutwa zikiwa sugu kushughulikiwa haraka na watendaji serikali.
Na Bashir Nkoromo, Singida
No comments:
Post a Comment