Klabu bingwa ya soka katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, TP Mazembe, imemsajili mchezji wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Ali Sadiki.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amepewa mkataba wa miaka mitano, kwa kupendeza kwa mchezo wake wakati wa wiki moja la majaribio kutoka katika klabu ya Stars ya Zimbabwe.
"Mazembe ni klabu kubwa na tunataka wachezaji wazuri zaidi kutoka kote duniani kuja hapa,’’ alisema Katumbi.Kusainiwa kwa Sadiki ni sehemu ya meneja wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi kuimarisha klabu hiyo katika ligi ya taifa.
Ikiwa kuna wachezaji wazuri zaidi, hata barani Ulaya wanakaribishwa kuja hapa.’’
Mazembe ni washindi mara nne wa ligi ya klabu bingwa Afrika na sasa wako katika robo fainali ya ligi ya mwaka huu sawa na AS Vita, Zamalek ya Misri, na Al-Hilal ya Sudan.
Sadiki alikuwa katika timu ya taifa ya Zimbabwe ambayo mwaka huu ilifika nusu fainali ya mabingwa wa Afrika.
Wakati huohuo, mchezaji wa Zambia Nathan Sinkala anayesakata kabumbu ya kimataifa, atamaliza msimu wake na klabu ya Sochaux ya Ufaransa mwaka huu
Katumbi amesema kuwa kuna vilabu kadhaa viavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ifikapo Januari mwaka ujao. .
No comments:
Post a Comment