 |
Msanii recho haule "pichani" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam Habari zimethibitishwa na Mwenyekiti wa bongo movie Steve nyerere,amesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua,baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye khali yake ikabadilika na kuwa mbaya ikabidi ahamishiwe ICU,Huko pia hali ikazidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia. |
Rachel Haule ambaye kacheza movie mbalimbali ikiwemo Vanesa in Dilema.
Chanzo cha kifo chake chake bado hakijafahamika ingawa taarifa za mwanzo zinasema alikua mjamzito na alikwenda Muhimbili kwa ajili ya kujifungua baadae alifanikiwa kujifungua lakini kwa bahati mbaya mtoto alifariki nae hali ilibadilika akapelekwa ICU lakini baadae akafariki.
Hii ni status yake ya mwisho Facebook.
Moja ya waigizaji walioandika kuhusu kifo cha Rachel ni Shilole ‘sitaki kumkufuru Mugu wangu ila kazi yake haina makosa, tulimpenda ila mwenyenzi Mungu kampenda zaidi, duh.. inauma sana pole Saguda kwa mtihani uliokupata ila tupo pamoja kwa kipindi hiki kigumu’
.
No comments:
Post a Comment