Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, wakati alipofika kwenye Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo, ambapo jumla ya miti 8,000, imeandaliwa kupandwa katika eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiumwagia maji mti alioupanda katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza, akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la msingi baada ya kupanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi wa kambi ya JKT Ruvu baada ya kupanda miti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana wa JKT walio katika mpango maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo na kusimamia suala zima la mazingira, baada ya kupanda miti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo, baada ya kupanda miti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF)baada ya kupanda miti.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya maafisa wa Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Ruvu, wakati akiondoka eneo hilo baada ya kupanda miti kama ishara ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, leo.
Vijana wa JKT wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment