Monday, May 26, 2014

MO ATAKA MADHEBEBU DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU

DSC_0575

Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.
Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.
DSC_0467
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila vikwazo",amesema.
Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya dini",amesema.
Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.

No comments:

Post a Comment