Friday, May 30, 2014

WATUHUMIWA WA MLIPUKO WA MABOMU JIJINI ARUSHA WAPANDISHWA KIZIMBANI.

Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.
WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni 12

Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .

"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu wan chi.  
Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.

No comments:

Post a Comment