Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, wakati Kinana alipowasili katika Wilaya ya Hanang, akitokea mkoani Singida, kwenda kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na njia ya kuzitatua katika mkoa wa Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Hanang Christina Mndeme wakati wa mapokezi hayo.
Sumaye akimlaki Katibu wa NEC, Itikadi na Uenzi Nape Nnauye, katika mapokezi ya Kinana yaliyofanyika katika kijiji cha Gehandu, Wilaya ya Hanang, Manyara. Kushoto Mkuu wa wilata hiyo Mndeme
Kinana akisalimiana na Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu wakati wa mapokezi hayo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisalimiana na Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara, Omar Chambo wakati wa mapokezi hayo.
Nape akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Hanang
Nape akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini, Jeetuson Patel wakati wa mapokezi kuingia wilaya hiyo Hanang
Mapokezi ya Kinana Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Vijana wa UVCCM, wakati wa mapokezi yake, Kijiji cha Gehandu, Hanang Manyara
Kinana akiingia Hanang, Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme (kulia) akiwa na mabinti wa Kibarbaig wakati wa mapokezi ya Kinana.
Vijana wa Kibarbaig wakionyesha ushupavu wao wa kuruka wakati wakimburudisha Kinana wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Gehandu, wilayani Hanang
Binti wa Kibarbaig akiruka wakati yeye na wenzake wakitoa burudani kwenye mapokezi ya Kinana
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga misumari kwenye kenchi kwenye jengo la maabara ya shule ya Sekondari ya Mwahu Kata ya Kihandu, wilayani Hanang.
.Kinana na Nape wakimhoji vizuri Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba aeleze alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha za mnara huo haijulikani nani analipwa.
Hatua hiyo ya kumhoji ilitokea baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto kuwa viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba iliserikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo. Picha zote na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment