Thursday, May 29, 2014

SIX TELECOMS, TATA COMMUNICATIONS WAZINDUA MTANDAO WA VPN

 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte akizungumza katika uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network (VPN)    kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya mawasiliano duniani, Tata Communications. Mtandao wa VPN utawawezesha wafanyabishara nchini kukamilisha shughuli zao za kibiashara hapa nchini bila ya kuvuka mpaka.
 Mwakilishi Mkuu wa kampuni ya Tata Communications kanda ya Afrika, Steven Van der Linde akizungumza katika uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network (VPN)  kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya mawasiliano duniani, Tata Communications. Mtandao wa VPN utawawezesha wafanyabishara nchini kukamilisha shughuli zao za kibiashara hapa nchini bila ya kuvuka mpaka.
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network (VPN) kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya mawasiliano duniani,kulia ni mwakilishi wa kampuni ya Tata Communications kanda ya Afrika, Steven Van der Linde.
Mwakilishi wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Daniel Seyoun akielezea mafanikio ya kampuni yao katika sekta ya mawasiliano ya Tehama nchini na nini watanzania watafaidika baada ya kuzindua mtandao mpya wa Virtual Private Network (VPN) ambao imeingia nchini kwa mara ya kwanza. Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa kampuni ya Tata Communications Kanda ya Afrika, Steven Van der Linde.
******************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
KAMPUNI ya Six Telecoms Limited kwa kushirikiana na kampuni inayongoza duniani ya Mawasiliano, Tata Communications imezindua mtandao maalum wa mawasiliano ujulikanao kwa jina la Virtual Private Network (VPN) ambayo itawawezesha kampuni za sekta ya biashara kuanzisha na kumalilisha shughuli zao bila kusafiri nje ya nchi.
Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Six Telecoms Limited, Rashid Shamte alisema hiyo ni fursa pekee kwa wafanyabiashara nchini kuepuka gharama mbali mbali katika shughuli zao kupata faida.
Shamte alisema kuwa kwa kupitia mtandao wa VPN, mfanyabishara anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mshirika wake wa nje kwa njia ya picha, sauti wameamua kuanzisha mtandao huo ili kuwawezesha wafanyabiashara nchini kuongeza wigo wa biashara zao kwani mpaka sasa zaidi ya nchi 400 duniani zinatumia mtandao wa VPN.
Alisema kuwa mtandao huo umeingia nchini kwa mara ya kwanza na unapatikana kwa bei nafuu na ni salama zaidi kulinganisha na mitandao mingine.
“Mtandao wa VPN ni wa kisasa na ni salama, hakuna mtu anayeweza kuingilia mawasiliano kutokana na ni wa haraka zaidi, tunafurahi kuwa kampuni ya kwanza ya Kitanzania kuanzisha huduma hii nchini baada ya mtandao wetu wa internet wa Metro kuongeza ufanisi wa sekta ya mawaliano ya tehama nchini na nchi nyingine duniani,” alisema Shamte.
Mkurugenzi wa Tata Communications Kanda ya Afrika, Steven Van der Linde alisema kuwa wamefurahi kuingia makubaliano hayo na Six Telecoms Limited na kuwaomba wafanyabiashara kujiunga na mtandao huo.
 Linde alisema kuwa kampuni yao ambayo makao yake makuu yapo nchini India, imejipatia sifa kubwa katika sekta ya mawasiliano ya Tehama na ujio wao Tanzania ni kuboresha sekta hiyo ambayo ni kubwa duniani.
Alisema kuwa kwa kupitia VPN ambayo ni imeleta mafanikio makubwa katika bara la Afrika, Asia-Pasifiki, Amerika, Ulaya na  India, wafanyabiashara watapunguza gharama mbali mbali za uendeshaji wa biashara zao kwani shughuli zote zitafanyika nchini na kukuza uchumi.
“Nimefurahi kupata fursa hii ya kuwekeza hapa nchini kwa kushirikiana na Six Telecoms Limited, hii ni fursa pekee kwa wafanyabiashara kuanza sura mpya na kisasa katika shughuli zao,” alisema Linde.

No comments:

Post a Comment