Meneja wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) kanda ya kaskazini Bw. Cuthbert Mafupa
akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) waliotembelea hifadhi ya Chome
kujionea hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kutunza misitu pamoja na
mafanikio yaliyofikiwa katika utunzaji wa hifadhi ya msitu wa Mazingira asilia
wa chome (Shengena) ikiwemo kupanda miti katika maeneo yaliyoathika na uvunaji
haramu wa rasilimali za msitu huo.
Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja katika hifadhi ya
Msitu Asilia wa Amani, uliopo Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara ya waandishi
hao iliyolenga kuwajengea uwezo katika uandishi wa habari za Misitu yenye
Mazingira Asilia pamoja na Utalii ikolojia,waliokaa mbele kutoka kushoto ni
Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo
Bw. Frank Mvungi, katikati ni Afisa Misitu Mkuu toka wakala wa huduma za Misitu
Tanzania Bw. Charles Ngatigwa na kulia ni Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel ten Bw. Kibwana Dachi.
Jengo la kihistoria lililojengwa na wakoloni wa kijerumani mnamo mwaka 1902 katika hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa amani uliopo Muheza Mkoani Tanga, Jengo hilo ni moja ya vivutio vikubwa katika hifadhi hiyo .
Prof. Vicky Mckinley ambaye ni Mtafiti kutoka chuo Kikuu cha Roosevelt kilichopo Chicago,Illinois nchini Marekani akipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutunza hifadhi ya Msitu wa mazingira asilia wa Amani uliopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga,wakati wa ziara ya Waandishi wa habari katika Msitu huo hivi karibuni.
Sehemu ya maporomoko ya maji katika hifadhi ya Msitu wa asili ya amani iliyopo Wilayani Muheza Mkoani Tanga ambayo imekuwa kivutio kwa watalii wanaotembelea eneo hilo.
Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome uliopo Same Mkoani Kilimanjaro.
Msaidizi wa Misitu Mkuu ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Zigi katika hifadhi ya Msitu wa asili Amani bw. Mlega Sossele akiwaeleza waandishi wa habari hawapo pichani jinsi wananchi wanavyonufaika na Msitu huo kwa kuwatengea asilimia 20 ya mapato yanayopatikana kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
Serikali
yafanikiwa kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu katika Hifadhi ya Msitu
wa Mazingira asilia wa Chome (Shengena) Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kwa
kutumia ulinzi shirikishi unaohusisha vijiji 27 vinavyoizunguka hifadhi hiyo.
Hayo yamesemwa
na Meneja wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania kanda ya Kaskazini (TFS) bw.
Cuthbert Mafupa wakati wa ziara ya waandishi wa Habari waliotembelea hifadhi ya
Chome na ile ya Amani iliyipo mkoani Tanga ili kujifunza na kuona hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika kutunza misitu asilia.
Akifafanua
Mafupa alisema kwa kufanya doria shirikishi wamefanikiwa kuondoa wachimbaji wa
madini takribani 2000 na kukamata zana mbalimbali kama vile mashine za kusukuma
maji (water pump) 20, buleshi 30, sururu 10.
“Upasuaji
mbao umepungua kutokana na doria shirikishi,na
tumefanikiwa kumata misemeno 10 ,
milango 160 p na vipande 100 vya mbao vilikamatwa” alisema mafupa.
Pia Mafupa
aliongeza kuwa Katika Utaratibu wa ulinzi shirikishi idadi ya Mifugo inayoingia
katika Msitu huo imepungua toka wastani wa ngombe 50 hadi ngombe 5 wanaoingia
ndani ya hifadhi na wahalifu 54 walikamatwa na 16 kati yao wamehukumiwa vifungo
na ishirini 29 wamelipa faini, na 9 kesi zao bado zinaendelea.
Katika
hatua nyingine Mafupa alisema Wakala wa Huduma za Misitu umewawezesha wananchi
kuanzisha bustani za Miti,vikundi vya ufugaji nyuki lengo likiwa ni kuwapa njia
mbadala wananchi ili kujipatia kipato na kuondokana na dhana ya kutegemea msitu
kujipatia mahitaji yao ya kila siku.
Aliongeza kwa
kuwashauri watanzania kutumia fursa ya Utalii ekolijia katika hifadhi za Misitu
asilia zilizopo hapa nchini ili kusaidia kuinua pato la Taifa na kuondokana na
dhana kuwa Utalii ni swala linalowahusu raia wa kigeni pekee.
Naye Rahel
Kisaka mkazi wa kijiji cha Mhero kata ya Chome alipongeza utaratibu
ulioanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu kwa kuwajengea uwezo wa kuanzisha
bustani za miti ambayo wanauza kati ya shilingi 300 hadi 500 na pia mradi wa
kufuga nyuki hali inayochangia kuongeza kipato na kuachana na dhana ya
kutegemea msitu huo kwa mahitaji yao ya kila siku.
Hifadhi ya
Msitu wa Mazingira Asilia wa Chome (Shengena) ni msitu wa Serikali kuu
unaosimamiwa na wakala wa huduma za Misitu Tanzania kupitia Wizara ya Mali
Asili na Utalii na ulitangazwa kwa mara ya kwanza kuwa msitu wa hifadhi mwaka
1951 kwa tangazo la Serikali Na.125 la tarehe 25/5/1951 ambapo katika msitu huo
kuna vivutio vya aina mbalimbali wakiwemo ndege,miti na ina ukubwa wa hekta 14,283.
No comments:
Post a Comment