Thursday, April 17, 2014

KINANA AHITIMISHA ZIARA YA SIKU 21 YA MIKOA YA RUKWA,KIGOMA NA KATAVI



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ambapo nyumba 70 zimekamilika kati ya 90 zitakazojengwa wilayani hapo.
 Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa zinazojengwa katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ngazi baada ya kukagua mradi wa maji wa Ikorongo,Katibu mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Balozi Ali Abeid Karume,mradi huu utakamilika mwezi juni 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza mabomba kwenye mradi wa maji wa Ikorongo wilayani Mpanda mkoani Katavi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpanda mjini kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili na kuwapongeza kuwa wachapakazi hodari katika kusimamia maendeleo yao na kuwataka kuwa makini na wanasiasa kwani mwisho wa siku hoja zao haziwasaidii wao kwenye maisha yao ya kila siku.
 Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili wilayani Mpanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba 32 Makanyagio Mpanda na kuwasihi wakazi hao kuchagua viongozi sahihi na wenye sifa za kuwaongoza.

No comments:

Post a Comment