Saturday, April 12, 2014

KINANA AMPONGEZA JK KWA KAZI NZURI



Ampongeza kwa ujenzi wa madaraja matatu makubwa, Daraja la Malagarasi,Kilombero na Daraja la Kigamboni.Ujenzi wa Sekondari za Kata Nape awaambia wakazi wa kijiji cha Mahembe wachague viongozi watakaotatua matatizo yao ya msingi kwanza na si vinginevyo kwani takwimu zinaonyesha viongozi wengi wa upinzani wameshindwa kutatua matatizo ya wananchi wa majimbo wanayoyaongoza.Wanachama  wapya 160 na 7 kutoka upinzani wajiunga na CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini na kuwataka kufanya kazi kwa umoja na mshikamano .
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Kigoma Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa wilaya ya Kigoma Vijijini waliokuwa nje ya ofisi za CCM Wilaya kabala ya kuelekea kwenye kijiji cha Mahembe ambapo mkutano mkubwa wa hadhara ulifanyika.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kigoma Vijijini akiwa pamoja na kiongozi wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Wilaya hiyo Ndugu Mgaya Mustafa ambaye alitoa taarifa ya kuwepo kwa kero ya kukamatwa Daladala kwa sababu ya kukosa sare za dereva na kondakta ambazo kwa maelezo ya madereva hao tatizo lipo kwa aliyepewa tenda kuchelewesha kushona.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkungwe kata ya Mahembe wilaya ya Kigoma Vijijini na kuwaambia Chama Cha Mapinduzi kiahidi kinachoweza kutekelezeka hivyo ahadi ya kuwapatia maji wanakijiji hao ipo na mkandarasi alishajenga mradi kwa asilimia 70 hivyo watapata maji mapema iwezekanavyo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mradi wa maji  katika kijiji cha Mkungwe kata ya Mahembe wilaya ya Kigoma Vijijini
 Kijiji cha Mkungwe wilaya ya Kigoma Vijijini kupata maji safi na salama hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mahembe ambapo alitoa sifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kujenga madaraja makubwa matatu,Maragarasi ,Kilombero na Kivukoni na kujenga Shule za Kata nchi nzima.

No comments:

Post a Comment