Mafuriko kwa Dar es salaam nzima |
Dalaja la mto mpiji lililokatika leo asubuhi limesababisha wakazi wa Bagamoyo kushindwa kufanya shughuli zao,Kukatika kwa Dalaja hilo kumesababishawakazi wa Bagamoyo kushindwa kufika Dar na wale wa Dar kutokufika Bagamoyo kutokana na kuwa ndio njia kuu. Wakazi wa Bagamoyo wakihaha baada ya kuona kwamba wameshindwa kupita katika Dalaja hilo kuendelea na majukumu yao. |
Sinza nako hali ni tete soko la afrika sana nalo likiwa limezingirwa na mafuliko,kutokana na hali hii kwa wakazi wa mabondeni mnashauliwa kuondoka kwani mvua bado zinaendelea kunyesha ikiwa leo ni siku ya pili ambapoimetangazwa kunyesha kwa siku tano Mfululizo. |
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa ameokoa baadhi ya mali zake huku asijue kwa kwenda
Tanesco mmeiona hii?Mbali ya nyumba hizi kufunikwa na maji ila bado nyumba hii kushoto umeme unawaka eneo la jangwani jambo ambalo ni hatari zaidi (picha na Mroki Mroki)
Hivi ndivyo mvua inavyowatesa wananchi wanaoishi mabondeni jiji Dar es Salaam ila bado hawataki kuhama
No comments:
Post a Comment