Saturday, April 12, 2014

KINANA, NAPE WAFANYA MAMBO MAZITO JIMBONI KWA ZITTO KABWE MKOANI KIGOMA


 Kinana akilakiwa baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM, Kata ya Mwandiga, Kigoma Vijijini ambapo alifamya mkutano wa ndani na Kamati ya Siasa ya Kata hiyo.

Kinana akishukuru kwa mapokezi

Kiongozi wa Madereva wa Daladala Stendi ya Mwandiga, Kigoma, Bagaya Mustafa ambaye ni mwanachama wa Chadema, akiwashawishi  wakazi wa eneo hilo kujiunga na CCM, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno, kusitisha operesheni ya Sumatra kuwakamata madereva wasio na sare na kuwatoza faini kubwa, kitendo ambacho kilisababisha kuitisha mgomo wa daladala kati ya Kigoma Mjini na Mwandiga leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye aliyemwelekeza Maneno kutoa sitisho hilo.


 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Ramadhan Maneno akitangaza kusitisha operesheni ,operesheni hiyo iliyokuwa inafanywa na maofisa wa Sumatra kwa ushirikiano na polisi.

Kinana akiongozana na viongozi wengine wa CCM na Serikali alipokagua mradi wa wajasiliamali wa kilimo Kigoma Vijijini.

 Ayub Kabwe ambaye ni Katibu wa Uenezi wa Wilaya ya Kigoma Vijijini, ambaye pia ni babake mdogo wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akihamasisha wananchi wakati wa ziara ya Kinana katika mji wa Mwandiga ambao ni nyumbani kwao Zito.

Kinana akizungumza na mkandarasi wa mradi wa maji katika Kijiji cha  baada ya kutembelea mradi huo ambao umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha. Kinana amewaahidi wananachi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili mradi huo ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

 Watoto wakigombea kuteka maji ya kisima cha mradi huo wa maji


 Vijana wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana katika Kijiji cha Mahembe, Kata ya Mahembe leo.

Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma Kaskazini.

 Nape akisisitiza jambo katika mkutano huo, ambapo alimchanachana Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa kutowajali wapigakura wake bali kuyapigania masuala ya kimastaifa, kama vile masuala ya Buzwagi, viongozi wanaoficha fedha njie ya nchi, badala ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kama vile maji, sekta ya afya, barabara na elimu.


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaburu akihutubia kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Kinana.


 Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopatiwa umeme na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini. Kikiwemo Kijiji cha Mahembe ambacho tayari kimepata umeme.

Kinana akimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini, awaeleze ni lini ujenzi wa shule ya msingi u na kituo cha afya utaanza katika Kata ya Mahembe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo.

 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo


 Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utii wakati wa mkutano huo wa hadhara katika Kata ya Mahembe.Zaidi ya watu 160 walijiunga na chama hicho.


 Wananchi wakinyoosha juu mikono kula kiapo cha utii cha CCM


Kinana akiongea na mtu mwenye ulemavu aliyehudhuria mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe

No comments:

Post a Comment