Friday, April 11, 2014

WACHEZAJI WA TIMU YA WATOTO WA MITAANI WATAKA KUSAIDIWA KUKUZA VIPAJI


Mfungaji bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka  Mwanza Tanzania, (TSC)ambayo iliibuka mshindi katika mashindano Kombe la Dunia la  Watoto  hao yaliyofanyika Brazil, mwaka huu  Frank William ameishauri , Serikali na jamii kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuweza kukuza vipaji vyao.
Kauli hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na William wakati walipolitembelea Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma , wakiwa na viongozi wao ,ambapo walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake  Juma Nkamia.
Alisema  siri ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda kuwakilisha watoto wengine wa mitaani. Hivyo  aliomba jamii kuwasaidia watoto wengi wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata  elimu lakini wana vipaji mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue  Amos, alishauri Serikal iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018 ya kombe  hilo.
Mchezaji mwingine wa timu hiyo ,Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa kuwasaidia, hivyo aliitaka iwekeze katika  soka la vijana  kwa  sababu baada ya miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.
Aliwaomba wajumbe wa  Bunge  hilo ,kuwasaidia ili waweze  kuvikuza vipaji vyao.
Naye Kocha wa timu hiyo,Suileiman Jabir alisema wadau  mbalimbali  kuwasaidia na  kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni wengi  ambao wanaweza kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya ushindi huo,  ni  kuwa na mpango wa kutafuta vijana wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi ya kiutalaamu na kiufundi.
 Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Aliwataka wajumbe wa Bunge  hilo, kuhakikisha was aula la watoto hao, linapewa kipaumbele na kuweka sheria itakayowadhibiti wakina baba wanatekeleza watoto,huku akiisa jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi wanapofariki dunia. 
Rais wa timu hiyo, Altaf Hirani aliiomba Serikali kuweza kuwasaidia kupata kiwanja  cha michezo  kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au kwenye  maeneo mengine ya nchi

No comments:

Post a Comment