Sunday, May 18, 2014

KIONGOZI WA UPINZANI WA SUDAN AKAMATWA



                Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Sadiq Al Mahdi.

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Sadiq al Mahdi amekamatwa kutokana na madai ya kuchochea chuki dhidi ya serikali.

Bwana Al Mahdi, kiongozi wa chama cha Umma na ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu katika serikali ya kidemokrasia ya Sudan alikamatwa baada ya kuzikosoa sera za serikali katika jimbo la Darfur na kuvishtumu vikosi vya Sudan kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu mbali na kutekeleza ubakaji katika eneo hilo.
Chama chake tayari kimevunja mazungumzo na serikali ya kutaka kubuni serikali ya muungano ili kumaliza mgogoro unaokumba uchumi wa taifa hilo huku kikiwataka wafuasi wake kuandamana.
Jimbo la Darfur limeshuhudia miaka kumi ya umwagaji damu na rais wa Sudan Omar el Bashir anasakwa na mahakama ya kimataifa ya ICC kwa shtaka la uhalifu wa kivita.Habari na bbc

No comments:

Post a Comment