Tuesday, May 20, 2014

UZINDUZI WA KITABU CHA WEKEZA AFRIKA 2014, WASHINGTON, DC




Scott Eisner (kulia)vice President of African Affairs, US Chambers of Commerce akifungua sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 iliyofanyika US Chambers of Commerce Washington, DC siku ya Jumatatu May 19, 2014 wengine katika meza ni Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali na Paul Duffen ambaye ni News Desk Media. 
Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza afrika 2014 ".invest in africa 2014" kitabu kinachotolewa na ubalozi wa umoja wa afrika ilifanyika Jumatatu May 19, 2014 kama kuanzia wiki ya kusherehekea siku ya afrika tarehe 27 mwezi mei .
Katika sherehe hizi zilizoandaliwa kwa pamoja baina ya ubalozi wa afrika washington na jumuia ya wafanya biashara wa marekani US chamber of commerce
Kulikuwa na majadiliano yaliyofanywa na viongozi wanao wakilisha Mabalozi wa kanda 5 za afrika zikiwemo East.West .South Central na North.viongozi hao walizungumzia rasilmali zilizopo Afrika na kuwaalika wawekezaji wawekeze afrika kwani kuna faida kubwa zinapatikana. Kwa upande wa serikali ya marekani ilihudhuriwa na mwakilishi wa msaidizi katibu wa ofisi ya mambo ya nje ya marekani na mgeni mwengine wa heshima ni muwakilishi wa umoja wa matIfa united nation global compact.kitabu kilichotoka mwaka huu pia kimeelezea mafanikio yaliyopatikana afrika na muelekeo katika miaka ijayo.


 Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 ikiendelea.
 Meza upande wa wawekezaji
 Meza waliokaa wawekezaji na wawakilishi wa Mabalozi na baadhi wa wahemimiwa Mbalozi/
Meza waliokaa wawakilishi wa serikali ya Marekani
Mwakilishi wakiendelea na sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014.
 Meza ubande wa waheshimiwa Mabalozi.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula(kushoto) katika picha ya pamoja na Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali na Danille Walker ambaye ni Director of African Affairs, US Chambers of Commerce

Afisa Ubalozi Suleiman Salehe katika picha ya pamoja na Balozi wa Ivory Cost nchini Marekani Mhe. Daouda Diabate

picha ya pamoja waheshimiwa Mabalozi, Maafisa na wawakilishi wa Mabalozi

No comments:

Post a Comment