Tuesday, June 10, 2014

MAHAKAMA YAMTIMUA WAZIRI MKUU WA LIBYA

Ahmed Maiteg anaungwa mkono na makundi ya Waislamu
Mahakama ya juu nchini Libya imesema kuwa kuchaguliwa kwa Ahmed Maiteg kama waziri mkuu mwezi uliopita ulikiuka katiba ya taifa hilo.
Maiteeg aliyeapishwa kuwa Waziri mkuu mwezi uliopita na bunge la taifa ,baada ya kura iliyokumbwa na utata.
Kuchaguliwa kwake na hatimaye kuapishwa kuliipelekea taifa hilo linalosakamwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi ,kuwa na mawaziri wakuu wawili kwani waziri mkuu aliyekuwepo Abdullah al-Thani alikataa kata kata kung'atuka mamlakani .

 Makundi ya Waislamu yanatawala sehemu kubwa ya Libya
Maiteeg mwenye umri wa miaka 42 na anayetokea Misurata alichaguliwa baada ya kuungwa mkono na mirengo ya waislamu .
Hata hivyo taifa hilo limegawanyika kati ya waislamu wa kadri na wale wenye misingi kali ya dini.
Mirengo hiyo ya waislamu ndiyo yanayodhibiti maeneo tofauti ya Taifa hilo.


Uchaguzi unatarajiwa kufanyika terehe 25 June,kuchagua bunge la taifa litakalorithi nafasi inashikiliwa kwa sasa na kongamano la kitaifa al maarufu '' General National Congress'' .

No comments:

Post a Comment