Monday, June 16, 2014

TANZANIA NI NCHI YA PILI AFRIKA MASHARIKI KWA UTAWALA BORA NA VITA DHIDI YA RUSHWA

 Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
 Watumishi kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakipita mbele ya meza Kuu wakati wa Maandamano Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Hab Mkwizu akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi  Mmoja jijini Dar es Salam.
 Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi  Mmoja jijini Dar es Salam.
 Baadhi ya watumishi wa Umma wakifuatilia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
 Afisa Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Robi Bwiru akimueleza jambo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi  Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki , wakati walipotembelea banda la Wizara hiyo.

Hussein Makame-MAELEZO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika amesema kuwa Tanzania inashika nafasi ya pili kati ya nchi tano za Shirikisho la Afrika Mashariki katika suala la Utawala Bora na vita dhidi ya Rushwa.
Waziri Mkuchika amayasema hayo wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza, Serikali ya Tanzania ilitangaza vita dhidi ya Rushwa na imekuwa ikiimarisha mapambano dhidi ya adui huyo hadi katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
“Katika nchi za Afrika Mashariki suala la Utawala Bora na Vita dhidi ya Rushwa, Tanzania tunashika nafasi ya pili, Rwanda ni ya kwanza, ya tatu ni Uganda na ya nne ni Kenya” alisema Waziri Mkuchika.
Waziri Mkuchika alikuwa akizungumzia madai yanayotolewa na baadhi ya watu hapa nchini kuwa Serikali ya Tanzania haina dhamira ya kupambana na Rushwa.
Alikanusha madai hayo na kusema kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya kupambana na Rushwa ndio maana imepitisha Sheria dhidi ya Rushwa,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) ina matawi kila mkoa na kila wilaya.
Alisema  kiashiria kingine cha kuthibitisha kuwa Serikali ya Tanzania inapamabana na Rushwa ni kufikishwa mahakamani kwa watu wanaotuhumiwa na Rushwa.
Hata hivyo, alibainisha kuwa mtumishi wa Takukuru hawezi kuwafikisha watu mahakamani bila ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
Hivyo aliwataka Watanzania wote kutambua kuwa wana wajibu wa kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kufanikisha vita hiyo dhidi ya Rushwa.
Waziri Mkuchika aliwakumbusha Watanzania kuwa mtumishi yeyote wa umma kumhudumia mwananchi ni haki yake, hivyo mtumishi anayeomba Rushwa ili atoe huduma anashiriki katika tendo la Rushwa.
Kutokana na hali hiyo, aliwaomba watumishi wajiepushe na Rushwa kwani Rushwa inawanyima watu haki, kukiwa na malalamiko anayepata haki ni yule anayetoa Rushwa.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka huu inasema “Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya Kuimarisha Utawala Bora na Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi”.
Mwisho

No comments:

Post a Comment