Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili kushoto) akipokea hundi yyenye thamani y ash. Bilioni moja ktoka TIPER gawio la hisa katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma. Wa kwanza kshoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair, Wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma na Wizara ya fedha Kaimu Msajili wa Hazina Elius Mwakabinga (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira nchini wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake kwa serikali leo mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya kampuni ya TIPER invyoshikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza soko la ajira nchini wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake kwa serikali leo mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma.
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (hayupo pichani) wakati wa hafla ya
kupokea gawio la hisa za Serikali katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma.
Wanafuata ni baadhi wa Maafisa waandamizi wa Wizara Fedha.
(Picha na habari na Ingiahed Mduma
na Eleuteri Mangi-Wizara ya Fedha)
TIPER YAIKABIDHI SERIKALI GAWIO LA SHILINGI 1,275,000.00.
Serikali imepokea shilingi bilioni moja kutoka
TIPER ikiwa ni gawio ambalo kampuni
hiyo imekuwa ikilipa kwa Wanahisa wake kila mwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servarcius Likwelile alipokuwa akipokea gawio hilo katika hafla
iliyofanyika leo mjini Dodoma.
Dkt. Likwelile alisema kuwa gawio hilo
litaelekezwa kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha 2013/2014 unaomalizika kwa
kuangalia maeneo ambayo yanawagusa wananchi ikiwemo sekta ya elimu, afya na
maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
hiyo, Daniel Belair alisema kuwa si mara ya kwanza kwa kampuni yake kutoa gawio
kama hilo kwa Serikali ambapo mwaka jana muda kama huu kampuni ilitoa kiasi
kama hicho kama gawio
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kampuni yake
imeendelea kufanya vizuri katika kukuza maisha ya kijamii na kiuchumi ambapo
kwa sasa inafanyakazi kwa saa 24 na siku saba za wiki.
Kwa kuzingatia utendaji huo, kampuni ya TIPER
imekuwa kichocheo kukuu cha kuzalisha ajira nchini ambapo hadi sasa asilimia 99
ya wafanyakazi wake ni nguvu kazi ya Watanzania.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TIPER Prof. Abdulkarim Mruma alisema kuwa imekuwa ni muhimu kwa kampuni yao
kuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kwa nchi na kuleta mafanikio makubwa ya
upatikanaji wa mafuta nchini.
Aidha,
TIPER Prof. Mruma alisema kuwa kwa sasa kampuni yao imejikita katika kuleta
mafuta yaliyosafishwa nchini ili kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.
“Kwa sasa tunaleta mafuta yaliyosafishwa badala ya
mafuta ghafi ambayo yanazalisha tope jingi ambalo limekuwa ni hatari katika
kutunza mazingira yetu” alisema Prof. Mruma
Pamoja na ufanisi huo, kumekuwepo na changamoto za
kuboresha mkataba wa utendaji na usimamizi wa hesabu masuala ambayo wanahisa
wote wawili wanaendelea kuyafanyia kazi kwa madhumuni ya kuwa na matokeo mazuri
zaidi kwa pande zote.
Kiutendaji kampuni ya TIPER inaendeshwa kwa ubia
kati ya Serikali ya Tanzania ambayo inahisa zenye asilimia 50 na Kampuni ya Oryx
Energies SA asilimia 50.
Pamoja na Tanzania Kampuni ya Oryx Energies SA
inafanyakazi katika mnchi mbalimbali duniani ambazo ni Benin, Burkina Faso,
Côte d'Ivoire, Guinea Conakry, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra
Leone, Afrika Kusini, Uhispania (Visiwa vya Canary), Togo, Uganda na Zambia.
Imetolewa na :
Msemaji wa Wizara ya
Fedha
Dodoma
13/6/2014
No comments:
Post a Comment