Tuesday, June 17, 2014

"WOMEN WITH ATTITUDE" SINEMA YENYE LADHA YA SHUGHULI KUONYESHWA NGOME KONGWE LEO

DSC_0166

Mtanzania mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya "Woman with Altitude" iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani 
Unaweza kudhani kwamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya dhahabu, kumbe sivyo kabisa.
Hili linajadiliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.
Sinema hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini.
Baada ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal waliamua kupanda milima mingine nmirefu katika mabara mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
DSC_0162  
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na documentary iliyopewa jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo itakayooyeshwa leo jioni ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014.
Machi 2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima Kilimanjaro.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao.
Filamu hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11 waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.
Wanawake hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza katika mahojiano alisema kwamba taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni ujumbe tosha kwa vijana na wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya kuyabadili.
 DSC_0098
Baadhi ya wasanii na waigizaji filamu wanaohudhuria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
(WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar

No comments:

Post a Comment