Friday, June 13, 2014

MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TABORA

MWwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF nchini Balozi Ali Mchumo akizungumza na Wadau wa mfuko huo ambapo alisema NHIF imekusudia kuboresha mfuko huo ili kuondoa kero kwa wanachama  hususani upatikanaji wa dawa.

Mgeni rasmi katika Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Tabora Bw.Elibariki Kingu ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tabora,Mkutano uliofanyika katikaukumbi wa Isike Mwanakiyungi ambapo wadau walikuwa wakijadili Changamoto mbalimbali ikiwa na lengo la kuboresha mfuko huo kwa wanachama wake.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Hamisi Mdee akielezea malengo ya mkutano huo wa wadau ambapo pamoja na mambo mengine alihimiza wadau kujitokeza kufungua maduka ya dawa muhimu vijijini ambayo yatasajiliwa  NHIF na yatakuwa yakitoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii.
Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua akizungumza katika mkutano huo
Meneja wa NHIF kanda magharibi Bw.Emmanuel Adina akitoa maelezo mafupi kuhusu mfuko huo kwa kanda ya magharibi.



Baadhi ya viongozi na wadau wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wa mkutano wa Wadau ambao unalengo la kujadili Changamoto mbalimbali zinazoukabili Mfuko huo.Picha na KAPIPIJhabari.COM

No comments:

Post a Comment