MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wakiwemo wanamichezo, leo wamejitokeza katika mazishi ya bondia wa zamani wa masumbwi ya kulipwa, Iraq Hudu (49).
Marehemu Hudu, maarufu kama ‘Kimbunga’, aliyefariki dunia Ijumaa mjiniDar es Salaam , amezikwa leo majira ya saa 10:00 alasiri katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam .
Bondia huyo aliyewahi kutamba vilivyo katika ulingo wa masumbwi, alifariki alfajiri ya Ijumaa katika hospitali ya Hindu Mandal, akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi.
Hudu alizaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari. Baada ya hapo, alijiingiza katika masumbwi katika miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000, alipoacha. Marehemu ameacha watoto watatu.
Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi |
Mwili wa Iraq Hudu ukishushwa katika gari maalumu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Baadhi wa waombolezaji wakiwa wamebeba jenza lililokuwa na mwili wa bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Iraq Hudu ‘Kimbunga’ wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya bondia Iraq Hudu yakifanika leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment