Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw Leonard Thadeo akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Shirika la Taifa la Bima (NIC) Uganda wakati wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki kwa mchezo wa Netiboli ambayo walicheza na JKT Mbweni ya Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw Leonard Thadeo akimkabidhi Kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya netiboli Klabu Bingwa Afrika Mashariki nahodha wa Timu ya NIC Uganda Obua Desire, baada ya kuifunga timu ya JKT Mbweni ya Tanzania magoli 47–30 jana jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya NIC Uganda wakifurahia ushindi uliopelekea kutetea ubingwa wao jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Netiboli Tanzania ( Chaneta ) Bi. Anna Kibira 9kusoto) -akikabidhiwa majukumu ya Shirikisho la vyama vya mpira wa netiboli Afrika Mashariki (EANA) na Rais wa Shirikisho hilo Bi.Mildred Ajiemba Wanyama jana jijini Dar es Salaam. Tanzania imekabidhi kuongoza sekretariati ya shirikisho hilo kutoka nchi ya Kenya.
Picha zote na FrankShija Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM.
No comments:
Post a Comment