Sunday, March 30, 2014

KINANA ATINGA NKASI, MAMIA WAHUDHURIA MKUTANO WAKE MJI MDOGO WA NAMANYERE


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Jumapili, Machi 30, 2014.
 Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
 Vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Wazee wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere 
 Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri, mkuatno huo wa Namanyere 
 Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 
















Mzee Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi. Picha zote na Bashir Nkoromo.

No comments:

Post a Comment