Monday, March 31, 2014

*'MBABE WA MANZESE' MASHALI, ALIVYOMGALAGAZA 'MBABE WA MWANANYAMALA' KASEBA



Na Mwandishi Wetu
MBABE wa Manzese, bondia Thomas Mashali, mwishoni mwa wiki alimgalagaza mpinzani wake mbabe wa Mwananyamala, Japhet Kaseba kwa pointi na kutwaa mkanda wa WBO uzito wa Light Heavy katika pambano lao lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam.

Majaji wote watatu walimpa ushindi bondia wa huyo wa Manzese aliyetangzwa mshindi kwa pointi 97-93 dhidi ya mbabe wa Mwananyama baada ya pambano hilo la raundi la 10, ambalo lilimalizika bila mtu kuanguka chini hata kwa sekunde wala kuhesabiwa kwa kuleweshwa ngumi.

 Mabondia hao wakichapa makonde ya kibabe.
 Bondia Japhet Kaseba akiwa na wapambe wake kabla ya kuanza kwa pambano hilo.
 Bondia Thomas Mashali, akiandaliwa kupanda ulingoni.
 Bondia Japhet Kaseba, akipanda ulingoni.
 Bondia Thomas Mashali, akipanda uliongoni.
 Mwandishi wa Chanel 5, Patrick Nyembela (kushoto) akiwa na mmoja kati ya askari waliokuwa wakilinda amani ukumbini humo.
***********************************

Kaseba aliyepanda ulingoni kwa mbwembwe nyingi, alianza vibaya katika raundi mbili za kwanza kabla ya kusimama imara katika raundi ya tatu na kumsukumia makonde mazito mpinzani wake.

Kaseba alirudi kwa kujiamini raundi ya nne na kumtandika mpinzani wake katika raundi yote hiyo. Hata hivyo, Mashali alizinduka raundi ya tano na kumdhibiti mpinzani wake, akianza kurusha ngumi za mbali na kuhama upande kwa haraka.

Raundi ya sita, Kaseba aliingia na maarifa ya kupiga na kukumbatia hatimaye kufanikiwa kumpunguza kasi Mashali.
Kaseba alifanya vizuri katika raundi ya saba na ya nane, lakini Mashali akazinduka raundi ya tisa na kumalizia ya 10 pia vizuri.




Japokuwa hata matokeo yangetangazwa sare kusingekuwa na malalamiko, lakini Japhet aliridhia uamuzi wa majaji na kumkumbatia Mashali baada ya pambano.

Pamoja na ushindi, lakini Mashali hakucheza katika kiwango chake kiasi cha kumaliza raundi 10 na rasta mwenzake huyo ambaye kwa sasa anacheza ngumi kwa kulazimisha tu, kwani uwezo uliofanya akaitwa ‘Champ’ umekwishamkimbia. 


 Alan Kamote wa Tanga, (kulia) akijikunja kuachia konde kwa mpinzani wake, Karage Suba, katika pambano lao la raundi 10, lililokuwa la Ubingwa wa UBO. Kamote alishinda kwa KO katika raundi ya sita.
*********************


Katika mapambano ya utangulizi, Alan Kamote alimshinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tano Karage Suba na kutwaa ubingwa wa UBO uzito wa Light, pambano kati ya Freddy Sayuni na Rajab Maoja lilivunjika raundi ya nne baada ya Maoja kuchanika na kushindwa kuendelea kugombea ubingwa wa PST.  

Said Mundi alimpiga Jumanne Mohamed kwa pointi pambano la uzito wa bantam, Issa Nampepeche alimpiga kwa pointi Zuberi Kitandula uzito wa bantam pambano lisilo la ubingwa, Saidi Chaku alitoka sare na Jocky Hamisi pambano la Feather lisilo la ubingwa na Majid Said alimpiga kwa pointi Frank Zaga uzito wa bantam pambano lisilo la ubingwa pia.


 MAPAMBANO YA UTANGULIZI
 Bondia Juma Fundi (kushoto) akichapana na Haji Juma, katika pambano lao la raundi sita. Katika pambano hilo, Juma Fundi aliibuka kidedea kwa Pointi.
 Mabondia Rajab Maoja (kushoto) na Fredy Sayuni, wakichapana katika pambano lao la raundi 10, lililokuwa na kuwania ubingwa. Mabondia hao walitoka droo. 
 Wapambe wa Fredy, wakimbeba bondia wao baada ya pambano hilo kukatishwa katika raundi ya 4, kwa mpinzani wake kuumia.
 Karage Suba (kulia) akijaribu kujibu mashambulizi.

Allan Kamote, akiwa na mkewe wakishangilia ushindi

No comments:

Post a Comment