Friday, June 6, 2014

BALOZI IDDI AONGEA NA WANANCHI WA KIVUNGE NA TUMBATU KUHUSU MATATIZO YA UVUVI.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kivunge kuhusu hitilafu za uvuvi kati ya Kijiji hicho na Tumbatu katika uwanja wa michezo wa Good Hope Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unaguja. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma haji na Katibu wa mkoa Huo Bibi Caterina.
 Umati wa wananchi wa Kivunge wakisikiliza nasaha za Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani kwenye mkutano wa kutathmini hitilafu iliyojitokeza ya uvuvi kati ya wananachi wa Kivunge na Tumbatu.
 Mwakilishi wa Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Bwana Sharifu Kombo Sharifuakitoa Taarifa ya tukio la kuchomwa moto kwa chombo cha Uvuvi cha wavuvi wa Kijiji hicho Kisiwani Tumbatu Mapema Mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji akiwaasa wananchi wa Kivunge kujiepusha na cheche zinazopenyezwa na baadhi ya watu kwenye migogoro yao ya kijamii hapo uwanja wa michezo wa Good Hope Mkwajuni. Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.
****************************************************************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzia sasa haitachukuwa dhamana tena ya kulipa gharama zozote zitakazotokana na baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao kwa kuvunjiana vyombo vyao wavyovitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.  
Alisema kitakachosimamiwa zaidi kwa sasa katika kukabiliana na wimbi hilo linaloonekana kuendelezwa katika baadhi ya maeneo hapa nchini ni kufuatwa kwa mkondo wa sheria dhidi ya watu watakaohusika na uharibifu wowote ule wa mali za raia au za Umma. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

No comments:

Post a Comment