Wednesday, July 23, 2014

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM NA WANANCHI WA PEMBA WAMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA KUWAANDALIA FUTARI IKURU YA WETE.

 Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba wakifutari pamoja hapo ikulu ya Wete futari iliyoandaliwa na
Rais wa Jamuhuri ya Mauungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akawakilishwa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,h. Mohd Aboud Mohd kati kati akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi kulia kwake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa wakijumuika na wananachi wa mikoa miwili ya Pemba kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.








Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.
Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete
Pemba.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na
 mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Dr. Mrisho Kikwete hapo wete Pemba.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Press  Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao kama inavyoagiza wakati wote.Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya Wananchi wa Miko miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo  Mjini Wete Pemba.
Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na
mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema
 kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi
 ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari
ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao.
Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa
Zanzibar .
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi
alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada
hiyo. Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa
nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi
hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni
katika kujipatia futari.

 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Press  Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao kama inavyoagiza wakati wote.
Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili ya Wananchi wa Miko miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya Ikulu ya Serikali ya Muungano yaliyopo  Mjini Wete Pemba.
Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada
akiyataja kuwa ni pamoja na madrasa, sala pamoja na mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema
Kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futarivya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao.
Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa Zanzibar .
Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada hiyo.Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia hufanywa na baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni katika kujipatia futari.

Othman Khamis Ame. Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Thursday, July 3, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BURUNDI MJINI BUJUMBURA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. P. Nkurunziza alipomtembelea Ofisini kwake Ikulu jijini Bujumbura jana Julai 02-2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Burundi Ikulu jijini Bujumbura jana ambapo alizungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi mbili hizi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya  Viongozi wa Serikali ya Burundi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura jana baada ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa nchi hiyo. Picha na OMR
*************************************
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BURUNDI, MHESHIMIWA PIERRE NKURUNZINZA
Julai 02, 2014: Bujumbura
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumatano Julai Pili, 2014 amekutana na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na kufanya naye mazungumzo. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Rais Nkurunzinza iliyopo katikati ya jiji la Bujumbura.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano baina ya Tanzania na Burundi ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Nkurunzinza na watu wa Burundi kwa sherehe zilizofana za kutimiza miaka 52 ya uhuru. Pia alitumia nafasi hiyo kumtakia kila la heri Mheshimiwa Rais Nkurunzinza pamoja na  watu wa Burundi kufuatia kupiga hatua kubwa za kimaendeleo sambamba na kuweza kuwafanya wananchi wa Burundi kuwa wamoja.
Pia alimueleza Rais Nkurunzinza kuhusu umuhimu wa kuzidi kuifanya Burundi kuwa nchi moja kwa kuwaunganisha watu wake na akaeleza kuwa, Tanzania inafurahi kuona hatua kubwa za kimaendeleo zikipigwa nchini Burundi na kwamba ili hatua hizo ziwe madhubuti, upo umuhimu wa kuwafanya wananchi wa Burundi kubakia wamoja na wanaoshirikiana katika kuiendeleza nchi yao.
“Burundi ikifanya vizuri maana yake ni kuwa Afrika Mashariki imefanya vizuri. Tanzania tutafurahi na nchi zote za ukanda wetu zitafurahi,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza kuwa lengo la Tanzania siku zote ni kuona jirani zake wakiishi kwa utulivu na wakifanya mambo yao ya maendeleo katika hali ya amani.
Katika mazungumzo hayo Rais Nkurunzinza aliendelea kuishukuru Tanzania kwa uhusiano wake wa karibu na Burundi na akaongeza kuwa wananchi wa nchi yake wamefurahishwa sana kwa Tanzania kushiriki katika sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Burundi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore jana. Pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania, sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Somalia na Waziri Mkuu wa Chad.
Msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais umeondoka leo jijini Bujumbura na kurejea jijini Dar es Salaam tayari kabisa kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa. Katika msafara huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim.
Imetolewa na:              Ofisi ya Makamu wa Rais
Julai 2, 2014 Bujumbura: Burundi