Thursday, June 27, 2013

*FAMILIA YA MANDERA YAZUA UTATA KUHUSU NI WAPI ATAZIKIWA


Na. Halima Kambi, Dar
Bado Bara la Afrika likiwa katika wingu nzito juu ya Afya ya baba wa Afrika Kusini Nelson Mandela familia yake nayo imeingia katika utata mkubwa juu ya mahali atakapozikwa Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini pindi atakapokufa.

Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni baada ya mjukuu wake, Chifu Mandla Mandela kususia kikao cha familia na kutoka nje ya kikao hicho baada ya kukasirishwa na mjadala wa kufufua miili ya  watoto  watatu  wa mandele .

Kutokana na familia inataka miili ya watoto  hao Thembekile, Makgatho na Makaziwe yaamishiwe Qunu ambako Mandela atazikwa.

Vyanzo vya habari tofauti nchini humo vilisema familia hiyo ilitofautiana na Mandla ambaye anataka babu yake azikwe mahali akozaliwa Mvezo huko wengine wakitaka wosia wwake wakuzikwa karibu na wanawe uheshimiwe
Pia familia ya mzee Nelson Mandela imeanza kusafisha makaburi pamoja na kupanda maua maeneo yanayozunguka viunga hivyo ikiwa ni ishara ya kujiandaa kwa lolote litakalotokea hivi karibuni..

Familia hiyo imefanya maamuzi hayo baada ya hali ya kiongozi huyo kuendelea kutokutia matumaini tangu kupelekwa kwake hospitali kwa ajili ya matibabu

Nelson Mandela ndiye kiongozi pekee wa Afrika aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupinga na kupambana na ubaguzi wa rangi dhidi ya makaburu nchini Afrika ya Kusini..

Hata hivyo maradhi yanayomsumbua kiongozi huyo hivi sasa  ni pamoja na kuathirika kwa mapafu maradhia ambayo yalianza kummaliza toka alipokuwa gerezani

Mbali na utata katika familia pia katika nyumba ya Mzee Mandela Houghton 12th Ave, waandishi wa habari kutoka nchini Marekani wameweka kambi nje ya nyumba hiyo, pia  Rais Zuma ameahirisha safari ya kwenda Mozambique.

Bado maswali mengi yapo kwa wananchi ndani ya Afrika ya Kusini na nje ya juu ya hali yam zee huyo kwani tayari wananchi wanahisi mzee Mandela ameshafariki Dunia lakini madaktari na familia inawaficha katika jambo hilo.

TUZIDI KUMUOMBEA MZEE MANDELA ILI AWEZE KUPONA MARADHI YANAYOMSUMBUA KWANI BADO AFRIKA INAMUHITAJI SANA

No comments:

Post a Comment