Thursday, May 30, 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR KUWASILI NCHINI TANZANIA JUMAMOSI.


Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa kaka wa Marehemu Keneth Mangwea, zinaeleza kuwa,  
mwili wa marehmu mdogo wake, Albert Mangwea, unatarajia kuwasili 
nchini siku ya Jumamosi ya Juni 1, ukitokea nchini Afrika ya Kusini.

Aidha Keneth, amesema kuwa utaratibu wa shughuli zote za maziko ikiwa ni pamoja na kuaga mwili wa marehemuna kutoa 
heshima za mwisho kwa 
Msanii huyo nguli wa Muziki wa Kizazi kipya 
Tanzania zitatolewa 
baada ya kamati Uhusika 
na familia kupanga.

Kaa nasi na Endelea kupitia mtandao 
huu ili kupata taarifa kuhusu shughuli nzima ya msiba 
wa Ndugu yetu Albert mangwea, aliyefariki
Mei 28 Nchini Afrika ya Kusini

*SHINDANO LA QS QUEENS KUFANYIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII

 *Ni Sehemu ya kuomboleza kifo cha Ngwea na kushirikisha wakali kibao kama vile Mb Dog, Madee, Diamond, Nay wa Mitego na wengineo
Na Mwandishi Wetu, Dar 
ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi wa Shindano la QS Queens 'Utamu Extra' linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya kesho ya Juni Mosi katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya kuenzi mchango wa msanii Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.

Ngwea amepangwa kuletwa kesho Jumamosi kwa ajili ya maziko yake yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro, huku onyesho hilo la maombolezo likihudhuliwa na wakali kibao wa muziki hapa nchini lilioandaliwa kwa muda mrefu na kilele chake kuwa Jumamosi hii.


Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo mchana, Meneja Masoko wa Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment, Freddy Felix, alisema kuwa shindano hilo litafanyika pia katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata warembo 20 watakaoishi katika Jumba moja kwa ajili ya kupata kimwana huyo wa QS Queens.

Alisema kuwa wasanii wengi wamepangwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, akiwamo Ney wa Mitego, Wanaume Halisi, ikiongozwa na Juma Nature, MB Dog, Diamond, Inspector Haroun, Madee, H-Baba, Snura, Khadija Kopa, Solid Ground Family na wengineo, wakiwamo wasanii chipukizi, Amor na Shalviny.

“Wasichana wote wanaotaka kushiriki shindano hili ambao ni kama uzinduzi wake, watajiandikisha katika fomu maalum ukumbini hapo, ambapo baadaye watatafutwa wengine ambao wote wataishi kwa miezi miwili katika nyumba moja itakayotembelewa na watu mbalimbali.

“Huku mshindi akijishindia gari la kifahari, pia wanapokuwa katika jumba hilo kila siku mtu atalipwa kadri tutakavyokubaliana, huku tukiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo mzuri katika shindano hili,” alisema Felix.

Kwa mujibu wa Felix, shindano hili kabla ya kupatikana warembo hao litatembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara, kama vile Mwanza, Tanga, Morogoro, Mbeya, Iringa na kwingineko kwa ajili ya kutafuta msichana mmoja wa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha QS ilitangaza kuwa mabinti wanaotakiwa kushiriki katika shindano hilo ni wale wenye vipaji maalum na uwezo wowote wa kupambanua mambo, huku kigezo cha elimu kikiwekwa pembeni.

Shindano hilo pia litaonyeshwa katika vituo vya Channel Ten, DTV, Clouds, ambapo huko kote wadau na wapenzi wa mambo ya urembo na burudani watapata fursa ya kuwapigia kura washiriki kabla ya siku ya kilele chake kitakachofanyika baadaye mwaka huu.

KUMRADHI KWA PICHA HIIKijana Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove, mkaazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, akiwa katika ward namba 6 hospital ya Sokoine -Lindi baada ya kuchomwa moto na vibaka

Na Abdulaziz Lindi 

Kijana Ismai Mayoba (31) anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri Manispaa ya Lindi ambaye amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.

  Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndg Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo

*MBUNGE WA NYAMAGANA ACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI, NAIBU SPIKA JOB NDUGAI AHAIRISHA KIKAO


 Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, leo amechafua hali ya hewa bungeni baada ya kusoma hotuba yaake iliyowakasirisha wapinzani wenzao wa Chama cha CUF, jambo lililomfanya Naibu Spika Job Ndugai, kuahirisha Kikao cha Bunge mapema asubuhi.

Wabunge wa Chama cha CUF wamezua tafrani hiyo Bungeni mjini Dodoma leo wakati Mbunge huyo wa Nyamagana, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wenje akiendelea kusoma hotuba hiyo  ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai,  akipinga maneno yaliyokuwa yameandikwa katika ukurasa wa nane wa hotuba hiyo yaliyosomeka Hivi:- 

Mheshimiwa Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka Chama cha Libera Democratis.

Baada ya hapo wabunge wa Cuf walisimama na kusema wakitaka maneno hayo yafutwe ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukurasa huo wa hotuba wakati huo msomaji alikuwa amefika kwenye ukurasa wa nne.

Baada ya kuona mabishano na kutoelewana ukumbini humo, Naibu Spika , Job Ndugai, alitumia busara zake na kutangaza kusitisha shughuli za Bunge  kabla mambo hayajawa mabaya maana kulikuwa na kila dalili za kuanza kushikana mashati baada ya baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuanza kufoka kwa sauti kubwa ndani ya Bunge, bila kufuata utaratibu.
Wabunge wa CUF wakisimama na kucharuka huku kila mmoja akifoka kivyake ......

*MATOKEO MAPYA YA WALIOFELI MITIHANI KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) 
leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-
QT.

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI 
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)  ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0          UTANGULIZI
MtihaniwaKidatochaNne, 2012ulifanyikanchinikotekuanziatarehe8/10-25/10/2012. Baraza la Mitihani la Tanzaniakatikakikaochakecha 94 kilichofanyikatarehe 30 Mei, 2013 liliidhinishamatokeo haya
2.0          USAJILI NA MAHUDHURIO
Jumlayavituo5,058vilitumikakatikakufanyamtihanihuoikilinganishwa 
na vituo4,795vilivyotumikamwaka 2011.
2.1          TaarifazaWatahiniwa
Jumlayawatahiniwa480,029  walisajiliwakufanyaMtihaniwaKidatochaNne 2012 wakiwemowasichana217,587sawa na asilimia45.33 na wavulana262,442sawa na asilimia54.67.WatahiniwawaliofanyamtihaniwaKidatochaNne 2012  ni 458,139sawa na asilimia95.44.Watahiniwa21,890 sawa na asilimia4.56yawatahiniwawotewaliosajiliwa, hawakufanyamtihani.

2.2          WatahiniwawaShule
Watahiniwawashulewaliosajiliwa ni  411,225 wakiwemowasichana182,982sawa na asilimia44.50 na wavulana228,243sawa na asilimia55.50.Watahiniwawashulewaliofanyamtihaniwalikuwa397,138sawa na asilimia96.57. Aidha, watahiniwa14,087sawa na asilimia3.43 hawakufanyamtihanikutokana na sababumbalimbalizikiwemoutoro, ugonjwa na vifo.
2.3          WatahiniwawaKujitegemea
Watahiniwawakujitegemeawaliosajiliwawalikuwa ni 68,804wakiwemowasichana34,605 sawa na asilimia50.30 na wavulana34,199sawa na asilimia49.70.Watahiniwa61,001wakiwemowasichana 30,918 nawavulana 30,083  wamefanyamtihaniwakatiwatahiniwa7,803sawa na asilimia 11.34 hawakufanyamtihani.
3.0          MATOKEO YA MTIHANI

*KLABU YA YANGA YAPONGEZWA NA KAMPUNI YA BIA YA KILIMANJARO LEO

Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil. 25 kwa Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa Timu yeyote itakayo chukua ubingwa wa Ligi Kuu.Wengine pichani ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Mussa Katabaro,Mkurugenzi wa Fedha Yanga,Denis Oundo pamoja na Geoffrey Makau.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya kuipongeza Timu ya Yanga baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara,hafla hiyo imefanyika kwenye Ukumbi wa TBL Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Mussa Katabaro.
Katibu Mkuu wa Yanga,Laurance Mwalusako akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuipongeza Timu ya Yanga baada ya kutwaa Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara.Kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe

*WADAU WA TCAA WAKUTANA DAR KUJADILIANA UBORESHWAJI WA NAMNA YA KUTOA LESENI


 Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano wa wazi wa siku moja wa Wadau wa Bodi ya TCAA , uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kuhusu  maboresho ya utoaji wa leseni  kwa makampuni mbalimbali yanayohudumia viwanja vya ndege nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA , Juma Mbwana.
 Mwenyekiti wa  Baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa anga Tanzania  Juma Fimbo(kulia)  na Katibu  Mtendaji wake Hamza Johari wakitoka baada ya kumalizika kwa kikao kilichowakutanisha wadau wa anga jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alia Aviation Consultants Mahmud .M. Shamte (aliesimama) akifafanua jambo katika mkutano huo wa maboresho ya utoaji wa leseni  kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege.
 Baadhi ya wadau wa mkutano wa wazi wa maboresho wa utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja  uliofanyika, jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha huduma za usafiri wa  anga pamoja na changamoto  mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.
 Sehemu ya muonekano wa ukumbi  wa mkutano wa Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ulikofanyika mkutano wa wazi wa maboresho ya utoaji wa leseni   kwa wadau wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa anga Mei 29.2013 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka  Equity Aviation Services (T) Ltd Rosemary Kacungira  akichangia mkutano wa wazi wa  maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni  katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya usafiri salama wa anga. Picha zote na Johary Kachwamba wa MAELEZO

*MASHINDANO YA KUMRITHI REDD'S MISS TANZANIA, BRIGIT KUENDELEA LEO


Na Mwandishi Wetu
KINYANG’ANYIRO cha safari ya kumpata Redd’s Miss Tanzania, kinazidi kushika kasi ambapo leo kutakuwa na mashindano katika vitongoji kadhaa vya kupata warembo wao.
Kazi kubwa itakuwa ya kumsaka Redd’s Miss Tabata, shindano ambalo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Dar West Park uliopo Tabata, pale warembo watakapopanda jukwaani kumsaka yule atakayetwaa taji.
Kwa mujibu wa Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga kila kitu kimekamilika, huku burudani ikitarajiwa kutolewa na bendi ya African Stars  ‘Twanga Pepeta’ na katika ukumbi wa Club Bilcanas kutakuwa na kinyang’anyiro cha wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali toka eneo la Temeke ambao watamsaka mrembo wao hapo na burudani itaongozwa na Ben paul huku kiingilio kikiwa sh 10,000  .
Wakati Tabata wakisaka mrembo wao, shughuli pevu itakuwa katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma kumsaka Redd’s Miss Dodoma, wakati warembo zaidi ya 10 watakapopanda jukwaani.
Katika shindano hilo litakalokuwa na burudani kadhaa kutoka kwa Richie Mavoko na Saki Band, kiingilio kinatarajiwa kuwa Sh 20,000 kwa viti maalumu na Sh 10,000 kwa vilivyobaki.
Redd’s Miss Singida naye anatarajiwa kupatikana leo katika shindano linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwenge.
Katika shindano hilo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazotolewa na Mzee Majuto, Mpoki na Ally Nipishe. Pia kutakuwa na shindano la Redd’s Miss Njiro, linalotarajiwa kufanyika leo.
Kinyang’anyiro cha kusaka warembo kinatarajiwa kuendelea kesho, ambapo kutakuwa na shindano la Redd’s Miss Dar City Centre, Redd’s Miss Mtwara, Redd’s Miss Pwani, Redd’s Miss Geita, Redd’s Miss Manyara na Redd’s Miss Rukwa.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

*BALOZI BISWARO AWAPA CHANGAMOTO STARS, ETHIOPIA

Na: Boniface Wambura, Addis Ababa

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Ametoa changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

“Watanzania tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga Morocco mabao 3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga. Tunataka kuwaona Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi mtanikuta kule,” amesema Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi kuichezea timu ya Yanga.

Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa Addis Ababa.

Balozi Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri.

Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga nacho Juni 3 mwaka huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu.

Wachezaji walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Wednesday, May 29, 2013

*ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN NCHINI CHINA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza suala kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi,zinazopelekea wageni wa aina tofauti kutembelea katika mji huo wa Beinjing nchini China.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi wa Maendeleo Omar Yussuf Mzee,akibadilishana Hati ya saini ya Mikataba ya uhusiano wa biashara na Naibu Waziri wa Biashara wa China Liu Cigui,baada ya kutilianan saini katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China akiwa katika ziara ya kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Mkewe mama mwamamwema Shein,katika viwanja vya Makumbusho ya Kihistoria nchini Nchini China pamoja na  ujumbe waliofuatana nao katika ziara ya kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kusoto) pamoja na ujumbe aliofuatana nao akiuliza suala kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi,zinazotembelea na wageni mbali mbali  katika Mji huo wa Beinjing nchini China,akiwa katika ziara ya Kiserikali ya siku saba. Picha na Ramadhan Othman,China.

*REDD'S MISS TANZANIA AWATAKA REDD'S MISS SINZA 2013 KULINDA HESHIMA

 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
***************************************
Na Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania 2012 ambaye pia ni Redds Miss Sinza, Brigitte Alfred amewataka warembo wanaowania taji la mwaka huu la kituo cha Sinza kutomuangusha  kwa kufauata nyayo zake katika shindano lililopangwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Meeda Club.

Brigitte alisema hayo juzi alipotembelea warembo wanaowania taji la mwaka huu katika kinyang’anyiro hicho kilichodhaminiwa na bia ya Redds Origional, Dodoma Wine, Clouds Media Group, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5.com na Sufiani Mafoto blog.

Alisema kuwa  warembo wa kituo hicho wanakazi kubwa ya kushinda taji hilo na baadaye Miss Kinondoni na Miss Tanzania kama yeye alivyofanya.

Alifafanua kuwa siri kubwa ya mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani hata yeye alifundishwa na matroni wa sasa, Mwajabu Juma na waandaaji ni wale wale.

“Sioni sababu ya kushindwa kufanya vyema katika mashindano haya, Redds Miss Sinza ndiyo inatetea taji la Miss Kinondoni na Miss Tanzania pia, hivyo macho ya wadau wote wa urembo yatakuwa kwenu na ndicho kitongoji kinachofunga mashindano ya ngazi ya chini, mnatakiwa kujituma na kuwafanya majaji kuwa na kazi ya ziada kumpata mshindi,” alisema Brigitte.

Alisema kuwa wadau wa masuala ya urembo wanaangalia Sinza mwaka huu itafanya nini baada ya mafanikio makubwa ya mwaka jana. “Sisi tumejenga  msingi mkubwa na kuleta heshima kwa wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla, nanyi mna jukumu hilo,” alisema.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na kiingilio ni sh 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 20,000 kwa viti vya VIP. Alisema kuwa wanakamilisha maandalizi ya burudani ya siku hiyo ambayo itakuwa ya aina yake.

BREAKING NEWZZ MSANII ALIYEDAIWA KUFARIKI DUNIA YU HAI M2 THE P

Marehemu Albert Mangwair akiwa na M2 the P.  

Taarifa za uhakika zilizothibitishwa kutoka nchini Afrika Kusini zinasema kuwa Yule Msanii M2 The P aliyekuwa na marehemu Albert Mangwair, aliyeripotiwa kufariki duni siku ya jana amezinduka rasmi leo mchana akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Afrika ya Kusini.

Akizungumza moja kwa moja kwa njia ya Simu kutoka nchini Afrika ya Kusini, Mtangazaji wa Redio Clouds, Millad Ayo, katika kindi cha Jahazi, alisema kuwa msanii huyo alionekana kupoteza fahamu na kuzimia kwa siku nzima kiasi cha kuripotiwa kufariki dunia siku ya jana.

Aidha alisema kuwa Msanii huyo leo asubuhi alizinduka na kufumbua macho na kujaribu kuinuka, lakini alishindwa na kurudi kulala, huku akitaka kujaribu kuzungumza na wabongo wenzake waliofika Hospitalini hapo bila mafanikio.

Hadi Millad anaripoti habari hii, bado msanii huyo alikuwa hai na akionyesha matumani, huku ikielezwa Hospitalini hapo kuwa Ripoti kamili ya kifo cha Manwair, itatolewa rasmi leo usiku.

P FUNK ATWEET NAKUSEMA HATAKI KUSIKIA TENA NYIMBO ALIZOREKODI YEYE ZA MAREHEMU MAGWAIR ZIKIPIGWA CLOUZ FM



Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.