Wednesday, November 28, 2012

*SHARO MILIONEA AZIKWA LEO MUHEZA NA MAMIA


 
 
 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 
 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkonona Msanii wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

Tuesday, October 30, 2012

*AZAM WAMWANGUKIA KOCHA WALIOMTIMUA, NI BAADA YA KUMTIMUA KOCHA MPYA ALIYECHAPWA 3-1 NA SIMBA

Kocha aliefukuzwa Boris Bunjak
Aliyekuwa Kocha wa Azam Stewart Hall
 KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.

Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.

Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu

Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.

Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).

Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.

Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine. 

Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
  

*GODFREY NA UPENDO WAMEREMETA

Bwana harusi Godfrey Mng'anyi akipozi kwa picha na mkewe, Upendo, wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanandoa hao walifunga ndoa yao katika Kanisa la Manzese. Bwana harusi ni mfanyabiasha na Bi Harusi ni mjasiliamali katika Ofisi yake ya Stationary.

Sunday, October 14, 2012

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA MAHUJAJI JIJINI DAR JANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka. Makamu alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni Oktoba 14, 2012 na kuzungumza na Mahujaj hao kuwaaga na kuwakabidhi  Misahafu kila mmoja kabla ya kuondoka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi  Misahafu, mmoja kati ya Mahujaj 150, wakati alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, 2012 kwa ajili ya kuwaaga Mahujaj hao walioondoka kuelekea Saud Arabia  mji Mkuu wa Makka, kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka.
 Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Sehemu ya Mahujaj kati ya 150 walioondoka jana kuelekea Saud Arabia mji Mkuu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka, wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana Oktoba 14, wakisubiri kupanda ndege kuanza safari hiyo. Mahujaj hao waliagwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. 

Tuesday, October 9, 2012

*MWANAFUNZI ALIYEFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE AKIWA WODINI


Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato hicho akiwa wadi namba 7B  katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo jana, baada ya kulazwa kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe ambapo hivi sasa anaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Saturday, October 6, 2012

*RICK ROSS ALIVYOPAGAWISHA USIKU WA SERENGETI FIESTA LEADERS CLUB

  Msanii wa muziki kutoka nchini marekani, Rick Ross, akishambulia jukwaa wakati wa Tamasha kubwa la Serengeti Fiesta, lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Mbali na msanii huyo pia walikuwapo wasanii kibao wa muziki wa Bongo Flava kutoka Bongo na nje ya Bongo.
 Msanii AT, akishambilia jikwaa na mnenguaji wake wakati wa tamasha hilo.
 Sehemu ya umati wa mashabiki wa Tamasha hilo, waliobahatika kujitokeza kushuhudia mashambulizi.
Sehemu ya mashabiki wakiburudika.

Tuesday, October 2, 2012

*THOMAS MASHALI KUKIPIGA NA BONDIA WA UGANDA SIKU YA NYERERE DAR


Na Mwandishi Wetu


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Bondia Medi Sebyala wa Uganda, litakalofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Mratibu wa Pambano hilo linalosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO, Regina Gwae, amesema mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Mashali anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vema nchini. 

“Huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda Ulaya, ukaikimbia Afrika Mashariki, hivyo tumeona tumpe pambano Afrika Mashariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa,” alisema Regina. 

Aliongeza kuwa, mazungumzo na bondia Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo ili ausaini baada ya kuupitia. 

“Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, huwezi kuacha kuwataja Mashali na Sebyala,” alisema Regina. 

Regina alisema wanataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala naye ni mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia mahiri nchini Fransis Cheka na Rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti. 

Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye kuvutia wakiwemo mabondia chipkizi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Jonas Segu,  mabondia wengine watakacheza utangulizi  watatangazwa baadaye watakaosindikiza mpambano huo.

 Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Friday, September 14, 2012

*UNICEF YALIPIGA JEKI JESHI LA MAGEREZA

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima (kulia) akipokea msaada wa kijamii kutoka kwa Mwakilishi Msaidizi wa kitengo cha  kuunganisha watoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa ( UNICEF) nchini  Paul Edwards (kushoto) leo jijini Dare es Salaam. Msaada huo una vitu mbalimbali kama vyandarua, magodoro, mito, taulo  na vifaa vya michezo.venye thamani ya shilingi ya dola za kimarekani 8,972. Kulia ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Fidelis Mboya, Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Pereira Silima, akizungumza machache baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Magereza waliohudhuria Hafla ya makabidhiano ya msaada  wa kijamii wa  Vifaa mbalimbali  kutoka UNICEF kwa watoto waliopo Magereza mawili ya watoto nchini Segerea na Ruanda (Mbeya), Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Slaam. 

Sunday, September 2, 2012

ROSE LUCAS ATWAA TAJI LA REDD'S KANDA YA MASHARIKI 2012


Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas, akipunga mkono baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia taji hilo kwa kuwashinda warembo wenzake 10 katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Nashera  'mji kasoro Bahari'.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas (katikati) akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake, mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi, baada kutangazwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo, Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
 
Washiriki wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa kuingia katika hatua hiyo. Kutoka kushoto ni 6. Zuhura Gora, 7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce Baluhi.
Warembo wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show yao ya pamoja ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo.
Wandaaji wa mashindano ya Mikoa iliyoleta washiriki wa Miss Kanda ya Mashariki wakitambiana huku Mwandaaji wa Mkoa wa Lindi, Ramadhan Shaha (katikati) akionesha ishara ya ushindi aitumiayo mkiambiaji wa Kimataifa wa Jamaika Bolt. Shaha alifanikiwa kutoa mshindi wa pili wa mashindano hayo. Wengine kushoto ni Mwandaaji wa Mtwara, Rajab Mchata, Mwandaaji wa Morogoro, Frank Ezekiel na kulia kabisa ni Mama Mchata.

Monday, August 20, 2012

Full Yanga 4-African Lyon 0, Msuva ang'ara


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima (kulia) akimsakata kiungo wa  African Lyon, wakati wa mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, inayotarajia kuanza hivi karibuni, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa Mabao 4-0. Bao la kwanza la Yanga, limefungwa na kipa wa African Lyon, Juma Abdul, aliyejifunga katika dakika 8, kipindi cha kwanza, bao la pili limefungwa na Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati, dakika ya 54, baada ya beki wa Lyon Semi Kessy, kumchezea rafu, Msuva katika eneo la hatari. Goli la tatu limefungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 72, kufuatia pasi safi ya Frank Dumayo na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 90+2, baada ya pasi safi ya Idrisa Rashid.
 Replay ya Penati iliyosababishwa na Simon Msuva (kushoto) akimsakata Beki wa African Lyon, Semi Kessy.
 Msuva, kapita, beki kazidiwa kaanza jitihada za ziada kumzuia kwa mkono.......
 Bado haitoshi aliona anazidi kuzidiwa, ikabidi atumie mkono na miguu kwa kumtega kwa nyuma.....
 Akaona isiwe tabu Heri lawama kuliko Fedheha.......akamaliza kazi ndani ya eneo la hatari la penati Boksi.....
 Mwamuzi wa mchezo huo akaamuru penati, hapa kipa wa African Lyon, akatoka kabla ya kupigwa mkwaju huo na Niyonzima na kupangua, mwamuzi huyo akaamuru irudiwe penati hiyo......
 Iliporudiwa, kipa huyu aliteswa kama hivi, Mpira kulia kwake yeye kushoto kwake.........Goooooooo!!!!! la tatu.
Goli lililoonekana kuzua utata kama inavyoonekana beki wa Lyon, akiokolea nyuma ya mstari....
Kocha wa timu ya Africa Lyon, Muargentina,  Pablo  Velez, akionekana kulalamikia jambo kwenye benchi la ufundi la timu yake  wakati timu yake ilipokutana na timu ya Yanga katika mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Kikosi cha timu ya Africa Lyon.
Kikosi cha timu ya Yanga. 

Saturday, August 18, 2012

Miss Tanzania aja na Filam ya Kisa cha kifo cha Kanumba

Miss Tanzania No. 3, 2009, Julieth William Lugembe nyota wa filamu mpya ya "Sister Julieth"

Miss Tanzania No. 3, 2009, Julieth William Lugembe (kushoto) na Sylvia Shally Miss TZ No.4 2009 ambao wamecheza filamu mpya ya "Sister Julieth"

MISS Tanzania Na.3 wa mwaka 2009, Julieth William amemshirikisha mrembo mwenzake aliyeshika Na.4 mwaka huo, Sylvia Shally, katika filamu mpya inayokwenda kwa jina la "Sister Julieth".

Filamu hiyo ambayo iko katika hatua ya uhariri inaelezea kisa cha kijana ambaye anatuhumiwa kumuua rafikiye wa kike wakati wakiwa peke yao chumbani na kesi mahakamani inamuelemea kijana huyo.

Sister Julieth, nafasi ambayo inachezwa na Sylvia, anakuja kama mzimu na kumtetea kijana huyo, ambaye anakumbana na upinzani mkali kutoka kwa mawakili wa upande wa mashitaka. 

Mrembo huyo aliyegeukia katika uigizaji, alisema hii ni filamu yake ya kwanza kucheza, kama ilivyo kwa Sylvia na kwamba ameitunga yeye mwenyewe.

Baada ya mwandishi kuhoji kama filamu hiyo inahusiana na tukio la marehemu Steven Kanumba aliyefariki wakiwa peke yao chumbani na muigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, aling'aka: "Aaah hapana. Hata kidogo. Ni kisa tofauti kabisa. Ni kisa kinachouhusisha mzimu unaokuja duniani kutoa ushahidi. 

"Ni kati ya filamu za hisia kali. Iko katika hatua ya uhariri na wakati wowote itatoka." 

Alisema katika filamu hiyo amewashirikisha pia wasanii wengine maarufu akiwamo Dude.

Katika shindano la Miss Tanzania 2009 ambalo Julieth alishika Na.3, Miriam Gerald aliibuka mshindi wa kwanza, Beatrice Lukindo alikuwa wa pili wakati nafasi ya nne ilishikwa na Sylvia na Sia Ndaskoi alikamilisha Top 5.

Thursday, August 16, 2012

Stars yatoka sare ya 3-3 na Botswana ‘Zebras’ kwao


 Mabeki wa Taifa Stars, wakimwangilia mshambuliaji wa Botswana ‘Zebras’ akifunga bao la tatu, wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Molepolole mjini Gaborone, jana.
Mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Botswana, ‘Zebras’ Oscar Neenga wakati wa mechi ya kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone Bostwana juzi na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Botswana, ‘Zebras’ Oscar Neenga wakati wa mechi ya kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone Bostwana juzi na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.
Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa leo (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.
Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa na Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd.
Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.
"Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
"Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza.
Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole," alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani kesho (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.